Membe aanza kuweweseka, ni baada ya waliompa kichwa kuanza kumkimbia

Benmpo

JF-Expert Member
Mar 23, 2015
450
424
Hivi karibuni CCM imemvua uanachama kada wao Bernard Membe ambaye pia alipata kuwa Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Kimataifa katika serikali ya awamu ya tano. Uamuzi huo wa CCM umewaacha watu wengi midomo wazi, kwani wengi walidhani kuwa kwa hatua ambayo Membe alikuwa amefikia ndani ya chama ya kugombea Urais 2015 isingekuwa rahisi kufukuzwa kwake nadhani naye alifikiri hivyo. Ama kweli, CCM haina mkubwa.

Wiki chache zilizopita Membe alipoitwa na Kamati ya Maadili ya CCM, wapinzani walionekana kumpa kichwa huku wakitoa sababu nyepesi za kwamba anaitwa sababu anania ya kuwania Urais 2020, na kuwa iwapo CCM wangempa adhabu kutokana na sababu hiyo basi kwao milango ilikuwa wazi kumpokea. Hali hiyo ilimfanya Membe kuwa na mtazamo finyu juu ya tabia zake za muda mrefu ndani ya Chama ambazo zilikuwa zimechafua profile yake. Aliingia kwenye kamati ya Maadili akiwa na notion ya Urais tu kichwani mwake, akashangazwa kuhojiwa juu ya mambo ambayo ya kinidhamu yaliyotokea mwaka 2014, na kubaki kaduwaa na utetezi usio na mashiko.

Kauli ya Membe sasa kuwa yeye anajua kuvuliwa uanachama kumesababishwa na yeye kutaka kugombea Urais haina mashikio, kwani mapema baada ya kuhojiwa alikuwa mwenye furaha sana, na kueleza kuwa amepata wakati mzuri wa kushauri kuhusu mambo ya kitaifa na kimataifa. Ikumbukwe kuwa ndani ya CCM mgombea wa nafasi ya Urais haijawahi kuwa tatizo kwa miaka yote, kwani ni utamaduni wao kwa mtu kugombea kwa terms mbili mfululizo.

Cha ajabu ni kuwa wale waliokuwa wakimpa kichwa sasa hivi wameanza kumkimbia. Kumekuwa na mjadala mrefu hasa kwenye mitandao ya Kijamii, wa wanachama upinzani kuwatahadharisha viongozi wao kuwa wasije-jaribu kubadili gia angani tena kama walivyofanya mwaka 2015 hali iliyopelekea chama kupoteza mvuto kabisa. Hili linamfanya Membe aweweseke sana kwani hana pa kushika sasa, na muda wa uchaguzi ndio huo unakabia. Hata vitabu vya dini vishasema “Utii ni Bora Kuliko Sadaka”, Membe kaingia chaka.
 
Nyumbu ni wale waliokaliana uchi wakakuleta wewe duniani. Mods tukiwaita CCM majina ya wanyama mnatupiga ban, mimi nimeshapigwa ban zaidi ya mara sita kuwaita hawa mburula 'nguruwe' lakini wao wanatuita sisi nyumbu lakini hawaguswi.

Sent using Jamii Forums mobile app
Mimi mwaCCM yeyote hanisumbui kwa maneno yawe ya busara au ya kejeli. Akili zao karibia wote zinafanana, kwa hiyo usihangaike na wachumia tumbo ambao hawajui hata wanatetea nini!! Nawashangaa Mods kama kweli walikupiga ban kwa kuwaita Nguruwe jina lao halisi.

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Jasusi mbobezi hawezi kutishiwa nyau
Jitu ambalo limeshafanya mission za hatari kwa ajili ya Taifa hilinunadhani linaweza kutishiwa nyau?
SASA TUONE HUO UBOBEZI WAKE ANAENDA KUUTUMIA WAPI MAANA UNAKUWA NA NGUVU UKIWA NDANI YA MFUMO UKITOKA WEWE UNAKUWA KAQMA MHAINI TU
 
Sema membe hana ushawishi sana nje ya ccm kutolewa ccm Ni changamoto sana kwake kisiasa. Tofauti na lowasa Alikuwa anaushawishi maana alijijenga yeye Kama yeye.
 
Benmpo,

Waandamizi wengi wa Usalama ( System ) ni Watu makini ila pamoja na kwamba najua Membe nae ni zao lao ( wa huko huko ) lakini naona yuko tofauti nao mno Kifikra na namuona ni kama vile Mpuuzi fulani na mpenda Mipasho Mipasho kama Mwanamke na pia ana Ushamba mwingi.
 
Jasusi mbobezi hawezi kutishiwa nyau
Jitu ambalo limeshafanya mission za hatari kwa ajili ya Taifa hilinunadhani linaweza kutishiwa nyau?
Waliokwisha fanya misheni Kali wala hawajitangazi. Bali dunia inawajua.
Yupo Kitine, yupo Mahiga na wengineo wengi tu.
 
Back
Top Bottom