KING KIGODA
JF-Expert Member
- Dec 28, 2018
- 3,982
- 3,242
We jamaa unapiga sana za mbavu duh!.Hivi kwa mujibu wa maandiko Yesu si ni mwana wa Mungu, vipi tena inakuwaje mnasema hana baba?
Mfano maandiko yanasema:
"Na kwa namna hii Mungu aliupenda ulimwengu hata akamtoa MWANA WAKE WA PEKEE ili kila atakayemuamini asipotee"
"Mahali pengine yanasema:
Baba mtukuze Mwanao na mwanao naye akutukuze....."
"Sehemu nyingine panasema, Huyu ni MWANANGU mpendwa niliyependezwa naye.."
Sasa ni andiko gani kwenye Biblia linasema Melkizedeki ana baba?
Kama Yesu ndiye Melkizedeki basi Yesu hana baba kwa hiyo dhana ya Kuwa Yesu ni mwana wa Mungu inavunjika
Na kama Yesu ni mwana Pekee wa Mungu basi Yesu siyo Melkizedeki maana Melkizedeki hana baba
Mkuu una hoja nzito sana aisee.Kama hiyo ndiyo hoja basi hata sisi tumekuwepo huko kwa Mungu kabla ya kuja duniani, kwa hiyo hata sisi hawa tunaowaita mama zetu ni njia tu ya kutuleta humu duniani.
HATA SISI HATUNA BABA WALA MAMA, HAWA TULIO NAO NI NJIA TU
Ecclesiastes 12:7
“Then shall the dust return to the earth as it was: and the spirit shall return unto God who gave it.”
Asante sana mkuu!.Hakuna mahali kwenye bible Yesu anatambulishwa kwa sifa ya uungu, hii ni theolojia ya kuunga unga tu kama hii ya kujaribu kumfananisha Yesu na Melkizedeki, lakini theolojia hiyo imebase kwenye logical inferences tu badala ya maandiko!, yaani imebase kwenye watu kuconnect dots badala ya kauli thabiti ya Yesu mwenyewe
Mathayo 24:36 Yesu mwenyewe kwa kauli yake anasema anasema, "hakuna ajuaye saa wala muda wa siku ile SI MALAIKA WALA MWANA AJUAYE ILA BABA PEKE YAKE (3“But concerning that day and hour no one knows, not even the angels of heaven, nor the Son,[a] but the Father only. ")
hili andiko peke yake linakuonyesha kuwa Yesu yuko limited in knowledge, hajui mambo yote na siri zote za ulimwengu huu, na hiyo peke yake ni ushahidi kuwa siyo Mungu
Mimi ndiyo maana huwa nakaa kimya tu.Maana wenzetu hata lugha huwa hawaizingati.Tatizo siyo waraka wa Waebrania, Tatizo ni uelewa wa waraka huo
Nyinyi mnautafsiri out of context kwa kuungaunga maana.
Ngoja Niquote Maandiko
SOURCE: https://www.biblegateway.com/passage/?search=Waebrania+7&version=SNT
Yesu Na Melkizedeki (Waebrania 7:11-17)
11 Kama ukamilifu ungaliweza kupatikana kwa njia ya ukuhani wa Walawi, kwa maana watu walipewa sheria kupitia kwao, ilikuwapo haja gani tena ya kuwepo kuhani mwingine, yaani kuhani kama Mel kizedeki, ambaye si kama Aroni? 12 Kwa maana yanapotokea maba diliko kwenye ukuhani, ni lazima pawepo na mabadiliko katika she ria. 13 Maana Bwana wetu ambaye ndiye anayesemwa katika mambo haya, alikuwa ni wa kabila lingine, na hakuna mtu katika kabila lake aliyewahi kuhudumu katika madhabahu. 14 Inafahamika wazi kuwa Bwana wetu alitoka katika kabila la Yuda, na Mose hakuwahi kusema lo lote juu ya makuhani kutoka katika kabila hilo. 15 Na hili tunalosema linakuwa wazi zaidi anapotokea kuhani mwingine kama Melkizedeki; 16 ambaye ukuhani wake hautokani na kanuni za ukoo wake, bali hutokana na uwezo wa maisha yasiyoharibika. 17 Kwa maana ameshuhudiwa hivi: “Wewe ni kuhani milele, kama wa Melkizedeki.”
Ni dhahiri:
Kwa mujibu wa andiko hilo katika msitari wa mwisho nilioupigia msitari unaosema "WEWE NI KUHANI MILELE KAMA MELKIZEDEKI" inaonysha kuwa YESU ni YESU na MELKIZEDEKI ni MELKIZEDEKI ila wote wana Ukuhani wa Milele!.
Neno "Kama" limetumika kwenye hilo andika KULINGANISHA watu wawili, Nikisema Mtu X kama Mtu Y kwenye ishu Z maana yake siyo kwamba X ndiye Y bali hawa ni watu tofauti lakini wana role Z ambayo ni moja
KITU KIKISHAITWA "KAMA" MAANA YAKE KINAFANANISHWA (compared to) , KINAKUWA SIYO CHENYEWE HALISI!
Ni suala la lugha tu, Ukitaka kutumia logic yako kuungaunga visivyoungika basi bible unaweza kuitafsiri vyovyote unavyopenda na ikaleta justification zozote
Umekuja vizuri mkuu.Asante.Mkuu kwanza thanks for sharing with us hi kitu; miongoni mwa maada ambazo waumini wengi hua wanapata sana TABU basi ni story ya huyu mtu uliyemsema hapa, but kwa kusoma kwangu Biblia, huyu Melkizedeki ni mtu tu kama walivyo pata kua watu wengine, au niweke hivi, Melkizedeki alikua mtumishi wa Mungu kama walivyo pata kutokea wengine na hata waliopo( Yesu anabakia kua ndio kila kitu katika Imani ya Kikristo and may be na zingine ( huko kwingine sina interest nako cause sijasoma sana vitabu vyao) Kwenye huo mstari uliutaja, hebu rudi nyuma mstari 2, utaona imeanza hivi kwa kufungia mabano, "huyo Melkizedeki ( tafsiri ya jina lake kwanza ni mfalme wa haki, tena mfalme wa Salem, maana yake mfalme wa Amani; ...inaendelea kama ulivyo copy hapo then akafungia mabano. KWahiyo huyu mtu sio kwamba hakuana na baba wala mama na wala hakua mfalme wa milele bali, tafsiri ya jina lake ndio hiyo. Kwa mfano, jina Emmanuel (jina la kwanza kabisa la ahadi la Yesu ) tafsiri yake ni Mungu pamoja na nasi; Kwa hiyo mtu yeyote aitwaye Immanuel hata leo either ana amini katika Mungu au la, hiyo ndio tafsiri ya jina hilo, hivi unajaua jina Yusufu au Joseph kwa kingereza maana yake ni nini? Ni kwamba mtoa jina ana maana hivi, "God you may give me another son" Haijalishi wazazi wanao toa jina hilo Yusufu/Joseph kwa watoto wao kama na wao wanaomba Mungu afanye hivyo au laa but hio ndio maana yake. So huyu Melkizedeki na yeye jina lake ndio lina tafsiri hiyo but yeye hakua kuahani wa milele na ndio maana hapo hapo ulipotoa maandiko, inasema ni mfano wa….., kitu mfano wa… means sio halisi ila kimebeba kitu kingine.
Again, thanks for sharing na huo ndio mchango wangu
Kila kitu kimeisha hapa.Good job brother.Unachanganya mambo unaposema kuwa KRISTO NDIYE MUNGU
Mungu ni Mungu na Yesu ni Yesu
Yesu alimwabudu Mungu na wala Mungu hakumwabudu Yesu [" Akaenda kwenye bustani ya Gethsemane kuomba, Baba ikiwezekana kikombe hiki kiniepuke, siyo kama mimi nitakavyo bali wewe Utakavyo.."]
Yesu hajui muda wala Saa ya Siku ya Mwisho, Bali Mungu anajua[ Yesu alisema " Hakuna aijuaye saa wa la siku ile si malaika wala mwana bali BABA peke yake"]
Yesu alichosikia kwa Mungu ndicho alichofundisha na wala mafundisho yake hayakuwa kwa utashi wake [Yesu alisema "Nisikiavyo ndivyo nihukumuvyo na hukumu yangu ni ya haki...."]
Wote wanaomkubali Yesu, ni Mungu ndiye aliyemjaalia wampokee na wamkubali wala si kwa uwezo wake binafsi watu hao kupokea mafundisho yake [Yesu alisema "Baba ulionipa sikumpoteza hata mmoja"]
Yesu anatambua kuwa BABA ndiye Mungu wa pekee [Yesu alisema "Na uzima wa Milele ni huu, wakujue wewe Mungu wa KWELI na wa PEKEE na Yesu Kristo uliyemtuma"]
Yesu anakiri BABA ni mkuu kuliko yeye [Yesu alisema "BABA yangu ni Mkuu kuliko Mimi"]
Mungu wa Yesu ndiye Mungu wetu, Na Mungu huyo Yesu alipenda kumuita BABA (Yesu alisema "Ninakwenda kwa Baba Yangu naye ni Baba Yenu, MUNGU WANGU NAYE NI MUNGU WENU")
Utukufu wa Yesu ni BABA ndiye aliyempa wala Yesu hakujipa Mwenyewe [Yesu alisema "Baba Ningependa hawa ulionipa wawe nami nitakapokuwa, wauone utukufu wangu, Utukufu ULIONIPA kabla ya kuumbwa kwa dunia"]
Sasa wewe unaleta habari za Yesu kuwa Mungu wakati maandiko all the time yanakuonyesha kuwa kuna ALIYE JUU YA YESU KIMAMLAKA!
Au unataka kutwambia BABA ni Mungu Mkubwa mkubwa na YESU ni Mungu Mdogomdogo?
Kwa mujibu wa maandiko huwezi kumuequate FATHER (JEHOVAH) na SON (JESUS) yaani utakwama, maandiko hususan Kauli za Yesu mwenyewe zitakukatalia.
Tukubali tu kuna Mungu Mmoja ambaye YESU alikuwa akimuita BABA
Na tukubali tu kuwa Yesu alitumwa na Mungu kuwafunza watu wamjue BABA ili wapate Salvation
Na tukubali tu kuwa Yesu naye ana Mungu, na Mungu mwenyewe ndiye yule alikuwa akimuita BABA
Hili tatizo la kuconnect dots ndo limeharibu sana mafundisho halisi ya Kristo: Badala ya kutwaa mafundisho ya Kristo kama alivyofundisha, watu throughout centuries wakaanza kutengeneza nadharia kuwa "ooh, Yesu ndyo Baba lakini hakujifunua tu, Wengine wanasema hapana BABA na MWANA ni Separate entities lakini wote ni sawa(CO-EQUAL), Wengine wanasema BABA na MWANA ni Walewale tu ila kila mmoja ana role tofauti
Logic/Falsafa/ Nadharia na kuconnect dots kwa baadhi ya watu kumedilute na kupoteza muelekeo halisi wa Mafunzo aliyofundisha Kristo mwenyewe na kuyapeleka so far out of context!
Kristo mwenyewe anasema MY FATHER IS GREATER THAN I (Baba yangu yu Mkuu kuliko mimi), lakini wanakuja watu centuries later wanasema FATHER na SON ni CO-EQUAL and CO-ETERNAL!. hii CO-EQUAL wameipata wapi? wamejitungia wenyewe tu ili kuconnect dots kwao kuweze kumakes sense kwa mujibu wa akili zao za kupenda falsafa!
JIBU LANGU NI KWAMBA KWENYE MAANDIKO FUATA KWANZA KAULI YA YESU MWENYEWE ILIYO CLEAR KABISA KABISA ISIYO NA MAWAA KABLA YA KUAFUATA KAULI AU OPINION YA MTU YEYOTE HATA KAMA MTU HUYO NI MWANAFUNZI WA YESU AU ANAYEDAI KUTOKEWA NA YESU NJIANI AKIELEKEA DAMASCUS (PAULO)
Ngoja nikuulize, hivi wewe kwa mtizamo wako maneno aliyoyasema Paulo, James, Petro au mtu yeyote yakikinzana na maneno halisi ya Yesu yapi unayapa precedent?. Maneno ya nani yanakuwa Final Finito?
Kwa mfano, ukisoma bible vizuri utaona mara kadhaa James ambaye ni mwanafunzi wa Yesu, aliyeishi na Yesu na ni ndugu wa Yesu akigombana mara kibao na Paulo juu ya mafundisho ya Paulo, James analalamika kuwa Paulo analeta baadhi mafundisho mapya na si yale aliyoyafundisha Yesu mwenyewe hususan mafundisho ya kuendelea kuheshimu Sheria za torati vs kuachana na sheria hizo!
Kwa mfano James anatofautiana na Paulo kwenye suala la nani mwenye kuhesabiwa haki, Paulo anasema kwenye Warumi 4:1-5 kuwa mtu anahesabiwa haki kwa IMANI yake na si Matendo yake, akaenda mbele kutoa mfano wa Abrahamu kuwa alihesabiwa haki mbele ya Mungu kwa Imani yake na si matendo yake japo matendo yake mazuri ni kitu cha kujivunia yeye binafsi.
James akamjibu Paulo kwenye James 2:24 kuwa Imani bila MATENDO imani hiyo Imekufa!, James akaenda mbali kutoa mfano wa kwenye agano la Kale juu ya yule kahaba Rahabu aliyewapoteza wapelelezi waliokuja kupeleleza katika nchi yao kwa kuwadanganya njia, na kwa kitendo cha kufanya hivyo tu huyo kahaba akahesabiwa haki!
Kwa hiyo Unaona hawa ni watu wawili wenye mawazo tofauti juu ya kuhesabiwa haki mbele ya Mungu kwa hiyo point yangu ni kwamba, kwa kuwa hata wao wana mitizamo inayokinzana juu ya mambo ya Mungu Sembuse Mmoja apingane na Kauli ya Wazi ya Yesu Mwenyewe?
Yesu kajiita Mtu, Kasema wazi kuwa na yeye pia ana Mungu anayemwabudu, Kasema BABA yake ni Mungu wake na pia ni Mungu wetu THEN baadae atokee mtu mmoja anayeitwa Paulo au Yeyote yule kisha aseme "Jamani eeeh Hapana, Yesu naye ni Mungu", anatoa kauli opposite kabisa na Yesu mwenyewe, mimi nasema Kauli ya kusikiliza hapo ni KAULI YA YESU MWENYEWE, HAWA WENGINE WAMETOA OPINION YAO TU!, OPINION YAO ITAKUWA NA UZITO IKIFANANA NA MAFUNDISHO YA KRISTO MWENYEWE ,IKIENDA AGAINST NAYE SISI TUNACHUKUA MANENO YA KRISTO NDO YANAKUWA FINAL!
Acha kukimbia ukweli wewe.Wewe nafikiri kaanzishe mada yako maana naona hauelewi misingi ya hii dunia kuumbwa.
Haujui muunganiko wa maagano yote mawili.
Hapa tunanyonya ilimu kwa wabobezi.
Sasa ilimu hii itapotea ukiendelea kufanya huo upotoshaji wako wa kukariri neno moja moja.
Anzisha mada wenzako kina faiza wakufuate.
Kwa hiyo mama yako ni surrogate.
Mama Maria ndio mama na Yesu.
JIBU LANGU NI KWAMBA KWENYE MAANDIKO FUATA KWANZA KAULI YA YESU MWENYEWE ILIYO CLEAR KABISA KABISA ISIYO NA MAWAA KABLA YA KUAFUATA KAULI AU OPINION YA MTU YEYOTE HATA KAMA MTU HUYO NI MWANAFUNZI WA YESU AU ANAYEDAI KUTOKEWA NA YESU NJIANI AKIELEKEA DAMASCUS (PAULO)
Ngoja nikuulize, hivi wewe kwa mtizamo wako maneno aliyoyasema Paulo, James, Petro au mtu yeyote yakikinzana na maneno halisi ya Yesu yapi unayapa precedent?. Maneno ya nani yanakuwa Final Finito?
Kwa mfano, ukisoma bible vizuri utaona mara kadhaa James ambaye ni mwanafunzi wa Yesu, aliyeishi na Yesu na ni ndugu wa Yesu akigombana mara kibao na Paulo juu ya mafundisho ya Paulo, James analalamika kuwa Paulo analeta baadhi mafundisho mapya na si yale aliyoyafundisha Yesu mwenyewe hususan mafundisho ya kuendelea kuheshimu Sheria za torati vs kuachana na sheria hizo!
Kwa mfano James anatofautiana na Paulo kwenye suala la nani mwenye kuhesabiwa haki, Paulo anasema kwenye Warumi 4:1-5 kuwa mtu anahesabiwa haki kwa IMANI yake na si Matendo yake, akaenda mbele kutoa mfano wa Abrahamu kuwa alihesabiwa haki mbele ya Mungu kwa Imani yake na si matendo yake japo matendo yake mazuri ni kitu cha kujivunia yeye binafsi.
James akamjibu Paulo kwenye James 2:24 kuwa Imani bila MATENDO imani hiyo Imekufa!, James akaenda mbali kutoa mfano wa kwenye agano la Kale juu ya yule kahaba Rahabu aliyewapoteza wapelelezi waliokuja kupeleleza katika nchi yao kwa kuwadanganya njia, na kwa kitendo cha kufanya hivyo tu huyo kahaba akahesabiwa haki!
Kwa hiyo Unaona hawa ni watu wawili wenye mawazo tofauti juu ya kuhesabiwa haki mbele ya Mungu kwa hiyo point yangu ni kwamba, kwa kuwa hata wao wana mitizamo inayokinzana juu ya mambo ya Mungu Sembuse Mmoja apingane na Kauli ya Wazi ya Yesu Mwenyewe?
Yesu kajiita Mtu, Kasema wazi kuwa na yeye pia ana Mungu anayemwabudu, Kasema BABA yake ni Mungu wake na pia ni Mungu wetu THEN baadae atokee mtu mmoja anayeitwa Paulo au Yeyote yule kisha aseme "Jamani eeeh Hapana, Yesu naye ni Mungu", anatoa kauli opposite kabisa na Yesu mwenyewe, mimi nasema Kauli ya kusikiliza hapo ni KAULI YA YESU MWENYEWE, HAWA WENGINE WAMETOA OPINION YAO TU!, OPINION YAO ITAKUWA NA UZITO IKIFANANA NA MAFUNDISHO YA KRISTO MWENYEWE ,IKIENDA AGAINST NAYE SISI TUNACHUKUA MANENO YA KRISTO NDO YANAKUWA FINAL!
Mkuu umemuelewa vizuri.Kaona uzi ni mzuri roho imemuuma akaamua alete tafakari zake za kipuuzi.takbirrrr ..
Pale muislam utapotaka kuonekana unajua vyote Qur-an na Bible.
Yako Qur-an mkuu, bible huelewi na ndio maana points zako ni kakariri kama mlivyozoea kukariri qur-an.
Bible inahitaji uelewa chini ya uongozi wa Roho mtakatifu, sasa mkuu wewe sijui unaongozwa na nini katika kuielewa Bible wakati hata huyo Roho mtakatifu muhuamini.
Melkizedeki hakuwa "Kuhani Mkuu" bali "Kuhani wa Mungu aliyejuu sana". Kumbuka wakati huo Mungu aliye juu sana hakuwa amefunuliwa kwa Musa na wala Ukuhani haukuwepo. Lakini tunadokezwa tu kuwa huyu Melkizedeki tayari alikuwa anamtolea sadaka El Elyon (Mwenye Enzi)
Swali zuri sana; itabidi turudi kwenye text yenyewe. Lakini kiufupi ni kuwa Ibrahim alimpa heshima kubwa Melkizedeki na ndio pointi ya baadaye kwenye Waebrania. Kuwa kama Ibrahim alitoa fungu la kumi kwa Melkizedeki ina maana kiwadhifa au hadhi Melkizedeki alikuwa juu yake.
Hili ni swali zuri. Na hapa ndio wengi wanachanganyikiwa. Je, Yesu alikuwepo kabla ya Bikira Maria; au alianza kuwepo baada ya kuzaliwa? Dokezo kidogo ni kuwa katika ile inayojulikana kama "Sala ya Kikuhani" ya Yesu kwenye Yohana 17 tunakutana na ombi hili kwa babake "Na sasa Baba, nitukuze mbele zako kwa ule utukufu niliokuwa nao kabla ya kuwekwa misingi ya ulimwengu" (Yoh. 17:5). Na mistari kadhaa chini anasisitiza hili (Yoh. 17:24). Ukisoma mistari hiyo lazima ujiulize? Yesu alikuwepo kabla ya misingi ya ulimwengu? Na kama alikuwepo kuzaliwa kwake na Bikira Maria basi kuna maana gani?
Habari za masiku wanajukwaa wote, leo ningependa tujadili watu mysterious kwenye vitabu vyetu vya dini kama ilivyo kawaida yetu. Hivyo twendeni pamoja ili tusolve mystery hii, kubwa ya yote tuongeze tu maarifa na kujibu maswali ambayo yameonekana magumu kwenye vitabu hivi.
Niweke rai mapema pamoja na kwamba inaongelea mtu wa kwenye imani zetu ila mada hii isijengwe kidini yaani kukashifiana bali ijikite kwenye mrengo wa kuelemishana. Karibuni
UTANGULIZI
Melchizidek anaongelewa kwa mara ya kwanza ndani ya Biblia kwenye kitabu cha mwanzo 14:18 ambapo baada ya Abraham kutokea vitani alikutana na Mfalme wa eneo la Salem (Jerusalem ya leo) ambapo alimbariki na Adam alimpa kikumi cha kila alichokuwa nacho wakati huo.
Kwahiyo kitabu cha mwanzo kinamueleza kama MFALME WA SALEM na kuhani wa Mungu YAHWEH
View attachment 1176929
AGANO JIPYA
Upande wa agano Jipya Melchizedek anaelezwa kuwa ana uhusiano ma Yesu.
Waebrania 5
6 kama asemavyo mahali pengine,Ndiwe kuhani milele Kwa mfano wa Melkizedeki
Zaburi 110:4, Waebrania 5:10,6:20 zote zinaeleza kuwa Yesu ni kuhani kwa mfuatano na huyu melchizedek. Ikumbukwe Makuhani wengi wamepita hapo kati na Yesu ametokea kwenye uzao wa Abraham sasa iweje afananishwe na melchizedek na sio kuhani yeyote yule??
Je huyu melchizedek ni nani hasa?
UTATA ZAIDI
Utata zaidi unaibuka pale ambapo muandishi wa kitabu cha waebrania (ambaye mpaka leo hafahamiki ni nani) anaandika haya
Waebrania 7
3 hana baba, hana mama, hana wazazi, hana mwanzo wa siku zake, wala mwisho wa uhai wake, bali amefananishwa na Mwana wa Mungu); huyo adumu kuhani milele.
Tunaambiwa huyu ''Jembe'' hakuwa na baba wala mama na anaishi milele hata sasa???
Ukisoma sura yote inamsifia mtu huyu wa ajabu (mysterious) na kusema licha ya ukuu wa Abraham kama Baba wa wayahudi ila haoni ndani kwa huyu Melchizedek!!
Book of Enoch
Muandishi wa kitabu hiki anajaribu kutupa mwanga kidogo kuhusu utata huu. Ukisoma Enoch 2 sura ya 71 inaeleza kuwa Kuhani Nir (Kaka yake Nuhu) alikuwa na mke ambaye hakulala naye toka alipoteuliwa na Mungu kuwa kuhani. Siku moja anagundua mke wake ana mimba, hivyo ukazuka ugomvi mkubwa mwishowe yule mama akapata presha akaanguka akafa, sasa cha ajabu walipotaka kuizika maiti haraka haraka ''kuua soo'' Wakashangaa mtoto ametoka tayari!!!. Yaani maiti imezaa!!!
Hivyo ikawa concluded kuwa kazaliwa bila baba wala mama.
Ikumbukwe alizaliwa kabla ya gharika, hivyo ili unabii utimie kuwa atakuwa kuhani wa makuhani wote ikabidi Malaika Gabriel amchukue na kumficha bustani ya Eden hivyo akapona gharika na akarudishwa baada ya gharika kupita.
HITIMISHO
Katika pekua pekua zangu sijakutana kabisa na maandiko yeyote kwenye biblia na pseudepigrapha (vilivyoachwa) ambacho kinagusia mwisho wake zaidi vyote vinasema anaishi milele ingawa havisemi wapi ama lini aliacha kuwa mfalme wa Salem.
Sasa wajuvi wa Historia na Dini mtusaidie je mtu huyu alikua nani hasa??
Pia kma alikuwa mkuu kuliko Abraham na amefananishwa na Yesu kwanini hajaongelewa sana kwenye Bible??
Je historia yake ni ipi??
Je mwisho wake ni upi hapa duniani? Au bado anaishi na sisi kwa sura tofauti?
Karibuni....
.Melkizedek anatajwa kuwa ni mungu alievaa umbo la mwanadamu.
Ukimgusa Paulo tutakuweka kwenye dustbin na hutakuwa na hoja yenye mashiko tena,,,hoja yako imefeli sasa umehamia kwenye baseless argument za watu flani wanaomchukia Paulo kwa sababu ya akili ndogo na ilio opposite.Pia unaharibu uzi mzuri wa Ndugu yetu ambae katulia akaandaa uzi wa uhakika.Kama huna hoja usiudhi watu humu.
Usiogope kumgusa yeyote katika wafuasi wake isipokuwa KRISTO mwenyewe, maana Injili aliifundisha yeye!, wengine wamerokodi tu au wameitafsiri na tafsiri yao si lazima iwe sahahi!
Wanafunzi wa Yesu kama vile James na Peter wenyewe walimkosoa Paulo Vikali juu ya baadhi ya mafundisho yake
Ilifikia hatua hadi James akamjibu Paulo kwa kutumia lugha kali sana ambayo kwa viwango vya sasa unaweza kusema alimtukana, haya yote yamo ndani ya Bible, Kwa hiyo siyo kweli kuwa mafundisho ya Paulo yalikuwa untouchable, na wanafunzi wa Yesu waliyaquestion pia, sembuse sisi?
unahitaji kusoma maandiko na historia ya mambo ili uweze kuelewa. Usikubali kumezeshwa Dogma/Doctrines za mathinkers, msome KRISTO wewe mwenyewe umuelewe!.