Comred Mbwana Allyamtu
JF-Expert Member
- Jun 28, 2016
- 351
- 866
MEJA GENERAL FRED EMMANUEL GISA RWIGYEMA BABA WA TAIFA NA MUASISI WA TAIFA JIPYA LA RWANDA, "KWA KILE KILICHOITWA KUREJESHWA KWA WATUSI KATIKA NCHI YA AHADI 'KANANI' (RWANDA)"
Na Comred Mbwana Allyamtu.
Rwigema alizaliwa kwa jina la Emmanuel Gisa alizaliwa Aprili 10, 1957 na kufariki dunia - 2 Oktoba 1990 Rwigema alikuwa ni mwanachama mwanzilishi na kiongozi (charismatic) wa kikosi cha watusi katika ukombozi wa nchi ya Rwanda kilicho julikana kama Rwanda Patriotic Front (RPF), nguvu za kisiasa na kijeshi aliyokuwa nayo ndio iliyompa nguvu hasa kwa jamii ya Watusi wa Rwanda walio ishi uhamishoni, jamii kubwa ya Watusi wakiwa na watoto wao na watu wengi walilazimishwa kuondoka nchini Rwanda baada ya vita ya mwaka 1959 iiyojulikana kama ''Vuguvugu la Kihutu katika Mapinduzi matakatifu" katika hatua hii Rwigema akiwa mtoto wa miaka 2 na familia yao walikimbilia Uganda kama wakimbizi.
Rwigema alizaliwa mwaka 1957 katika mji wa Gitarama uliopo kusini mwa Rwanda, ilipofika Mwaka 1960 yeye na familia yake walikimbilia Uganda na kufikia katika makazi ya kambi ya wakimbizi katika mji wa Nshungerezi uliopo katika jimbo la magharibi la Ankole Karibu kilomita 273 na jiji la Kampala kufatia Mapinduzi ya kikundi cha Kihutu kilichokuwa kikiungwa mkono na utawala wa Rais wa kwanza wa Rwanda Gregory Kayibanda na chama chake cha PREPEHUT hali iliyopelekea Mapinduzi ya 1959 yaliopelekea kuondolewa kwa mfalme wa Rwanda Mwami Kigeri V.
Baada ya Rwigema kumaliza shule ya sekondari mwaka 1976, alikwenda Tanzania baada ya kufanya mawasiliano na Salim Sareh aliokuwa akiishi nchini Tanzania Chini ya uangalizi wa TISS (idara ya usalama wa Tanzania) ikumbukwe kuwa kipindi hicho Tanzania ilikuwa ikiratibu utalatibu wa kumuondoa madalakani IDD Amin Dada. Na hivyo Rwigema akajiunga na kikosi cha Front for National Salvation (FRONASA), kikundi cha waasi kiilicho kuwa kinaongozwa na Yoweri Museveni, na ndugu wa rafiki yake Salim Saleh. Ni katika hatua hii Rwigema alianza kujiita Fred Rwigema.
Baadaye mwaka huo, Fred Rwigema aliamua kusafiri hadi Msumbiji kwa msaada wa Mwalimu Nyerere na idara ya TISS na hatimaye kujiunga na kikosi cha FRELIMO ambao walikuwa wanapigana kwa ajili ya ukombozi wa Msumbiji waweze kuitoa mikononi mwa Mreno na ikumbukwe kuwa wakati huu Ureno ilikuwa imepandikiza vikaragosi vyao kupitia waasi wa Renamo. Na Ilipofika Mwaka 1979, alilejea tena Uganda na kuamua kujiunga na kikosi cha waasi cha Uganda National Liberation Army (UNLA), ambayo pamoja na ushilika wa majeshi ya Tanzania majeshi ya JWTZ na waasi hao waliiteka Kampala mwezi Aprili 1979 na kumfurumisha (ousted) dikteta wa kijeshi wa Uganda "Field Marshal" Idi Amin.
Baadaye Rwigema aliamua kujiunga na kikosi kilicho anzishwa na Museveni katika kikundi cha National Resistance Army (NRA), ambao walipigana vita vya msituni dhidi ya serikali ya Milton Obote. Baada ya NRA kushinda vita hiyo NRA waliteka nguvu katika nchi ya Uganda na kuikomboa mwaka 1986, Rwigema akateuliwa kuwa naibu Waziri wa Ulinzi.
Kama ilivyo kwa legendary wengine Rwigyema alikuwa akipenda sana mchezo wa soka na pia alikuwa na upendo mkubwa kwa watu kitu kilichopelekea yeye kuwa maarufu katika mji wa Kampala, Mara kadhaa kwamba alipokwenda kuangalia mpira kwenye Uwanja wa Nakivubo umati wa watu bila kumpa (ovation) walisimama juu ya mlango kutaka kumuona. Pamoja na sifa ya kuwa shujaa na tactical katika ujanja wa mapigano ya mstuni alikuwa mara kwa mara katika mstari wa mbele katika mapambano kaskazini mwa Uganda wakati wa offensives ya serikali mpya dhidi ya mabaki ya utawala wa Obote na makundi ya wataka madaraka na mfululizo wa makundi ya waasi yaliyo kuwa yanajitokeza.
Ilipo fika Februari 6, 1988, alifanywa kuwa Meja Jenerali na kuteuliwa kama kamanda naibu wa jeshi la National Resistance Army (NRA) katika jeshi la Uganda wakati huo alikuwa anajulikana kama Meja jenerali Fred Rwigema. Na Ilipofika Oktoba 1, 1990, Rwigyema aliamua kuanzisha vuguvugu za kulejea nyumbani kwa Watusi wote waliokuwa wakiishi uhamishoni ndio alianzisha vuguvugu la kurejea Rwanda kwa kuamua kuunda kikundi cha waasi kikundi hicho kiliitwa Rwanda People Front ( RPF) na aliongoza majeshi ya RPF katika vita ya kwanza kabisa dhidi ya serikali ya Rais wa Rwanda wa kipindi hicho Ndugu Habyarimama Juvenal ingawa baadhi ya wachambuzi hudai kwamba msaada mkubwa wa kikundi cha RPF ulitoka Uganda kufadhili kikundi hicho cha waasi na nguvu ya Uganda isingetolewa bila yeye Rwigema.
Hata hivyo mapigano yalikuwa makali sana baada ya serekali ya Habyarimana kupokea msaada wa kijeshi kutoka serekali ya Mobutu huko Zaire, Kikosi cha Mobutu kilivuka mpaka wa mji wa Goma na Gisenyi kuja kujibu mashambulizi dhidi ya uvamizi wa waasi wa RPF. Ikumbukwe kuwa Habyariman alikuwa ni mtoto wa ubatizo wa Mobutu seseseko Kuku Ngwendu Wazabanga Raisi wa mda mrefu wa kongo-DRC iliokuwa ikijulikana kama Zaire wakati huo. Siku iliyofuata yani Katika siku ya pili ya mapambano, Rwigyema alipigwa risasi kichwani na kufa, inadaiwa kuwa pamoja na tamaa ya wapiganaji wa RPF kutaka kupora mali na vitu wakati wa mapigano kuliwafanya kushindwa vibaya vita kitu kilichochangiwa na utovu wa maadili ya jeshi.
Pamoja na hilo Kuna ubishi kuhusu hali halisi ya kifo cha Rwigyema taalifa rasmi iliyotolewa Kigali na serikali ya Rwanda, kupitia toleo liotolewa na zilizotajwa na mchunguzi bwana Gérard Prunier katika historia aliyoitoa mwaka 1995 katika kitabu chake juu ya maisha ya Meja jenerali Fred Rwigema, alieleza kuwa ni kwamba "Rwigyema aliuawa na risasi kupotea". Katika kitabu chake baadaye huyo, Prunier alisema kwamba kuna uwezekano mkubwa kuwa Rwigyema aliuawa na subcommander wake aliyeitwa Peter Bayingana, kufuatia hoja juu ya mbinu na tamaa ya kuongoza kikosi.
Baada ya kifo cha Rwigema ndipo Paul Kagame ambaye sasa ni rais wa nne wa Rwanda aliongoza kikosi hicho kama mkuu wa kijeshi wa RPF na baadae kuwa mkuu na amiri jeshi mkuu wa Rwanda Patriotic Army (RPA) mpaka ushindi ulipopatikana mwaka Julai 1994 kufuatia kumalizika kwa mauaji ya kimbari, ambayo karibu watu milioni moja wengi wao Watusi waliuawa .
Fred Rwigyema ni mmoja wa mashujaa wa taifa la Rwanda hata hivyo mwili wake ulizikwa katika makaburi ya "Heroes Cemetery" ( makaburi ya mashujaa) mjini Kigali. Na siku ya kifo chake yani 2/10.. Ya Kila mwaka ni siku ya mapumziko nchini Rwanda. RWIGYEMA Hutajwa kama mkombozi na mtetezi wa vuguvugu la utaifa nchini Rwanda na serekali ya kagame humtazama kama Baba wa taifa na muasisi wa taifa lipya la Rwanda.
NB:
Kwa taalifa zaidi juu ya historia ya Rwanda kuanzia mwaka 700 AD mpaka utawala wa Poul Kagame Rejea makala yangu :"Je Rwanda iko salama baada ya kumalizika vita ya kimbali?"...
Ndimi: Comred Mbwana Allyamtu.
copy rights reseved
written by Comred Mbwana Allyamtu
•Napatika kwa mawasliano
Comred Mbwana Allyamtu
Kwa Tanzania
+255679555526.
+255765026057.
Kwa Rwanda
+250733153930
+250788214234
Kwa DRC
+243 977 860 824
Kwa Msumbiji (Mozambique)
+27 874791033.
Email- Mbwanaallyamtu990Gmail.com