Mei Mosi, sikukuu ya watumwa Tanzania

Mei Mosi, sikukuu ya watumwa Tanzania

TAWA

JF-Expert Member
Joined
Jun 23, 2013
Posts
3,674
Reaction score
1,572
Kila mwaka tarehe 01/05 tunaadhimisha tunayoita ni sikukuu ya wafanyakazi hapa nchini na duniani kwa ujumla.

Lakini uhalisia ni kwamba sikukuu ya wafanyakazi haiendani na uhalisia wa hali ya wafanyakazi hapa nchini, tunatumia gharama kubwa kuandaa sherehe za wafanyakazi, mabonanza na tafrija kedekede utadhani hao wafanyakazi wanaishi maisha ya kifalme.

Wito wangu kwa viongozi wa kisiasa hasa CCM kutotumia siku hii kutimiza matakwa yao ya kisiasa kama vile kujitangazia nia za ubunge na udiwani.

Serikali ya chama cha mapinduzi lazima ifahamu wafanyakazi wa umma wa nchi hii wanaishi maisha ya kitumwa sana, mishahara yao ni midogo sana kiasi kutomudu kuishi vizuri.
 
mkuu povu lote hili la nin?kwan huwez kuikumbusha serikal yako kwa utulivu?labda kwa vile hukipendi chama,je,unahisi hii nchi ikichukuliwa na watu wa tengeru shida za wafanyakazi zitaisha?
 
mkuu povu lote hili la nin?kwan huwez kuikumbusha serikal yako kwa utulivu?labda kwa vile hukipendi chama,je,unahisi hii nchi ikichukuliwa na watu wa tengeru shida za wafanyakazi zitaisha?

Wewe[MENTION] laki si hela[/MENTION] si utumi tu jina lililozoeleka unamwogopa nani kwani
 
Kumekua na utamaduni wa kuadhimisha mei mosi kila mwaka kwa wafanyakazi na kualika mgeni rasmi ambae huwa ni mkuu wa nchi,kama ilivyokawaida siku ya kesho wafanyakazi wanatarajia kufanya hivyo lakini wafanyakazi hao wanamambo mengi ambayo hayajatekelezwa na serikali,kwa mfano kada ya walimu ambao wanakilio cha cha muda mrefu cha mazingira magumu ya kazi,mishahara duni,kutokupandishwa madaraja,malimbikizo ya mishahara n.k,lakini pia sekta zingine kama afya pia wanakero chungu nzima lakini leo hii wanahimizwa kuadhimisha mei mosi kwa furaha na mbwembwe wakati madai yao hata siku moja hayajawahi kusikilizwa hivyo hakuna umuhimu wowote wa kusherekea siku hiyo maana haina tija hata kidogo.
 
Ni kweli sikukuu hii sijaona umuhimu wake bado, labda wanaofahamu watujuze..
 
So long as mmekumbatia mfumo wa kibepari, working class lazima muendelee kuwa watumwa. Na ndo maana ACT inakuja na majibu sahihi ya kilio chako.
 
bila hata aibu mkwere anatangaza kupunguza asilimia moja ya PAYE na bado anapigiwa makofi na kura wafanyakazi watakipa chama chake.Wafanyakazi jitambue muvadirike!!
 
Kumekua na utamaduni wa kuadhimisha mei mosi kila mwaka kwa wafanyakazi na kualika mgeni rasmi ambae huwa ni mkuu wa nchi,kama ilivyokawaida siku ya kesho wafanyakazi wanatarajia kufanya hivyo lakini wafanyakazi hao wanamambo mengi ambayo hayajatekelezwa na serikali,kwa mfano kada ya walimu ambao wanakilio cha cha muda mrefu cha mazingira magumu ya kazi,mishahara duni,kutokupandishwa madaraja,malimbikizo ya mishahara n.k,lakini pia sekta zingine kama afya pia wanakero chungu nzima lakini leo hii wanahimizwa kuadhimisha mei mosi kwa furaha na mbwembwe wakati madai yao hata siku moja hayajawahi kusikilizwa hivyo hakuna umuhimu wowote wa kusherekea siku hiyo maana haina tija hata kidogo.

Umuhimu upo ndugu, kesho ilibidi ------ akatumikiwe ila badala yake tutakua tunapumua tukifanya na mipango ya kujikwamua kutoka kwenye wimbi linalotuzonga wengi la kuchumia tumbo.. kazi ufanye wewe, pesa anatengeneza mwenzio!! hii sikukuu ingekuwa hata kila mwezi
 
Ukitaka kusikilizwa hama toka kwenye kundi la kuajiriwa, ukajiajiri! Kuthubutu hutaki, toka uko unasoma unawaza jambo moja tu, Wapi nitapata kazi??!! Ukipata kazi, hauwaz hata mwezi mmoja mbele kila unachopata unatumia, nani amesema kuna maslahi ya kutosha kwenye ajira? kadiri unavyoendelea kupata ndio utakavyotumia... Uhuru wa kweli wa kiuchumi,muda uko kwenye ajira binafsi, kwa hiyo kabla ya kulalamika hutendewi haki, jiulize wewe unajitendea haki kwa kuwa na mipango thabiti yenye kutekelezeka ili kujiondoa kwenye kundi la wasiotendewa haki??? kama hapana, basi we mtumwa na utatumwa sana!
 
Mleta mada yupo sahihi, ni utumwa ama hakika watu hawajitambui wanaangamia kwa kukosa maarifa.
 
tanzania kuna vichaa ambao hawajielewi kila siku ni kuitukana serikali
 
Kwa kutazama tu maisha ya hao wanaojiita wafanyakazi utagundua kuwa hawana sababu ya kusheherekea siku hii kwa kuwa uhalisia wa maisha yao unawatupa mbali na dhumuni la sherehe hizo....kinachowatia watu upofu ni kuwa hizo sherehe zimewekwa mwanzoni mwa mwezi ambapo wavuja jasho wengi bado wa hela ya kula..hivyo kusahau kabisa shida zao.....
 
A clear and logical presentation
 
Back
Top Bottom