Mei Mosi 2018: Rais Magufuli atapandisha Mishahara miradi mikubwa ya Serikali ikikamilika, Mwaka jana alinukuliwa Vibaya

Fuatilia comments zangu. Siku zote naangalia msingi wa hoja na wala sio chama wala maslahi yangu binafsi. Nipo kati na kati, sina mrengo wa kisiasa. Mimi kwangu taifa kwanza.
Dhana ya utaifa ilisha pitwa na wakati.
Popote duniani, waweza ishi.
Hili mipaka tumejiwekea tu sisi wanadam.

Miradi butu inayoumiza wananchi huku ukiwanyonya wafanyakazi na wananchi vilevile ni kuwatia umasikini na ukilema.

Wewe kama ni mtumishi, utakuwa wapata ziada ya fedha nje ya mshahara, watumishi wanatapika maji.

Wengi ufanisi utapotea, ni kulipua tuuu
 
Kumbe ucheleweshaji wa kesi kwa mahakama ya kazi kunamkera Rais. Katika hotuba yake leo ameahidi kwamba analijua tatizo hili na ndiyo maana ameteua majaji wapya kumi.

Hakika mahakama hii imeemelemewa maana ni mahakama yenye majaji wawili tu nchi nzima yaani Lilian Mashaka na Aisha Nyerere.

Si kwamba majaji hawa wawili hawana uwezo. Hapana. Wana uwezo mpana na haitashangaza mmoja wao au wote wawili siku moja ukasikiwa wamepandishwa kuwa majaji Mahakama ya Rufaa.

Kinachosumbua ni kwamba kesi za ajira zimekuwa nyingi na kuna wanaosema kwamba Mahakama ya Kazi ndiyo ya pili kwa wingi wa kesi nyingi ikifuatiwa na ile ya Ardhi.

Katika hali hii, mtu anayejijua hana haki ataipenda kwa sababu mkosa haki mbinu yake ya kwanza mahakamani huwa ni kuhakikisha anachelewesha kesi ndipo zije mbinu zingine.

Hivyo, kama kuna uonevu wowote kazini, unashindwa kuushughulikia kwani hata ukienda Mahakamani, utshinda kesi lakini ukweli ni kwamba utatumia si chini ya miaka mitatu. Kwa kifupi ni kwamba Mahakama ya Kazi ilikuwa imeshaanza kutokuwa tegemeo.

Siyo kwamba wanahongwa. Bali kesi zinachelewa kiasi cha kukatisha tamaa.

Tunalieleza hili kwa sababu kila mmoja huku mitandaoni ni mfanyakazi, hivyo kila mmoja wetu ni mtuhumu au mtuhumiwa mtarajiwa wa hii Mahakama ya Kazi.

Hata ukichapa kazi vipi, usidhani uko salama. Bado yanaweza kutokea mazingira wenzako wakakuonea wivu na majungu wakakusababisha ukaacha au kufukuzwa kazi kwa uonevu (harrasment).

Sasa katika hali hii, mkombozi au tumaini pekee ilikuwa ni Mahakama ya Kazi (High Court Labor Division). Lakini kama hali ndiyo ile iliyopo la ucheleweshaji wa kesi basi serikali lazima ijue kwamba morali na uzalendo utakosekana.

Hebu tafakari, serikali inapenda kila mmoja awe mzalendo sehemu yake ya kazi. Sasa jiulize, hivi ukiwa mzalendo sana kwenye sehemu yako ya kazi utaishia wapi? Je, utapendwa na mabosi wako? Je, utachukiwa na mabosi wako?

Kw amfano, wafanyakazi waliokuwa kwenye madini wakiona makinikia yakisafirishwa, unadhani hawakuwa wazalendo wakaangali tu yanaibiwa?

Tulihoji wafanyakazi wale wanakuambia makinikia yameibiwa huku wakiona tena wanasema yalikuwa yanalindwa na bunduki ya SMG.

Sasa tukawahoji wafanyakazi wale kwamba kwa nini hakumuwaambia mabosi wakmba wanaharibu uchumi, wakajibu, unataka nifukuzwe kazi, utanilisha wewe?

Wafanyakazi wale wanasema kweli. Hali ni hivyohivyo popote unapofanyia kazi. Mwajiri kama anakwepa kodi na unaona, je, utamwambia kwamba nilipe mshahara wangu vizuri lakini usikwepe kodi. Je, unaweza kufanya hivyo?

Huwezi. Kwa nini? Kwa sababu utafukuzwa kazi. Halafu ukishafukuzwa kazi, serikali haitambui kwamba uligombana na mabosi wako kwa sababu ya uzalendo na kuupigania uchumi wa taifa ili.

Basi, ahueni ingekuwa inakuja kama Mahakama ya Kazi itafanya kesi yako iishe haraka. BAdala yake Mahakama ya Kazi utachelewa kupata haki yako, ingawa utaipata.

Ndugu zangu, je katika hali kama hii, utarudia mchezo wa kuwa mzalendo? Hapana. Utaishia kufanya wanachofanya wenzako. Wenzako watafanya utumbo, tena utumbo unaoiumiza nchi, na wewe itabidi uige tu kuvumilia au na wewe ufanye utumbo ili ulinde ajira yako.

Mtu anaweza kuweka pingamizi (PO) ambalo anajua halina nguvu lakini anajua pingamizi litachukua si chini ya miezi minane. Baada ya PO ndipo inakuja kesi ya msingi inayochukua si chini ya miezi mingine minane hata kama atashindwa.

Huyu tayari ameshafurahi kesi kuchelewesha kwa miezi 16. Athari za kucheleweshwa kesi ni mbaya zaidi kwa mwenye haki na ni furaha kwa anayejijua hana haki.

Hapo ndipo tulipofikia. Inawezekana serikali na Mahakama ya Kazi hili hawajaliona. Sasa leo Rais Magufuli kaliongelea hili kwamba anatambua kuna tatizo la kuchelewesha kesi za ajira.

Mitandao ilipaswa kulijadili hili kwa sababu kila mmoja ataguswa. Tena kipindi hiki vyuma vimekaza kila mmoja ni mhanga unaweza kuathirika na Mahakamani haki ukachelewa kuipata kiasi kwamba unapoipata haina faida tena.

Kama Rais anaona kwamba ameteua majaji kumi, hatudhani kama watapelekwa Mahakama ya Kazi. Tunaamini msongamano uko hata mikoani na makahakama zingine. Rais ikibidi ateue majaji wengine kumi.

Pale Mahakama ya Kazi panahitajika majaji kama saba hivi. Sasa wanapobaki majaji wawili tu, matokeo yake ndiyo haya.

Pamoja na kuw ana hao majaji wawili tu, bado hutokea tatizo jingine analoliweza Mungu tu.

Yupo pale Jaji mmoja mara kadhaa kesi zake zinaahirishwa kwa sababu ya kuumwa au kuhudhuria matibabu hospitalini. N jaji mchapakazi kwelikweli, muadilifu kwelikweli lakini ni kweli pia amekuwa akisumbuliwa na maradhi.

Hata ukimuona unaona dalili za kusumbuliwa maradhi na sanasana unamhurumia tu. Ukimkosa kwa sababu kaenda hospitali, kesi zke zote za siku hiyi zinaahirishwa wakati mwingine kwa miezi miwili. Jaji mgonjwa!

Hatuwezi kuendelea namna hii. Tunasisitiza, pale Labour Court pawe na majaji kama sita hivi siyo wawili tu. Majaji wawili hawawezi kusimamia kesi za ajira za nchi nzima.

Tunashukuru Rais Magufuli kuliona hilo ni tatizo na akalitaja mbele ya Sikukuu ya Wafanyakazi. Tunasubiri Jaji Mkuu alione hilo ni tatizo, tunasubiri Mahamakaa ya Kazi nayo ilione hili ni tatizo.

Na watanzania mitandaoni, tulione hili kuwa ni tatizo na kulipigia kelele. Tumesema, hata ukiishi kitakatifu vipi, bado kila mmoja wetu ni mtuhumu au mtuhumiwa mtarajiwa hivyo tushinikize haki ipatikane mapema tuwe na imani zaidi na Mahakama ya Kazi (Labour Court)
 
Dhana ya utaifa ilisha pitwa na wakati.
Popote duniani, waweza ishi.
Hili mipaka tumejiwekea tu sisi wanadam.

Miradi butu inayoumiza wananchi huku ukiwanyonya wafanyakazi na wananchi vilevile ni kuwatia umasikini na ukilema.

Wewe kama ni mtumishi, utakuwa wapata ziada ya fedha nje ya mshahara, watumishi wanatapika maji.

Wengi ufanisi utapotea, ni kulipua tuuu
Swala la hali ngumu sipingi, ni kweli hali ni ngumu kwa hakika. Mimi pia nina hali ngumu, mshahara haumalizi mwezi, wategemezi wengi n.k. Mimi sio kwamba yote anayofanya Rais namuunga mkono, yapo mengine simuungi mkono kama swala la ununuzi wa ndege na mengine. Swala lililopo ni je tujiongezee mishahara halafu mambo mengine yatakayotupeleka mbele kama taifa tuyaache? Nani atatufanyia hayo tutakayoyaacha?. Mataifa ya wenzetu yalipiga hatua kwa kusacrifice baadhi ya mambo, haikuwa rahisi, they went through pain ndio maana hata leo watu wanatamani kwenda kuishi kwao.

Kwa ujumla tangu nimeanza kazi mshahara wangu haujawahi kukidhi mahitaji yangu na wategemezi wangu. Siku zote nipo na shortage japo zipo nyakati huwa nakuwa na surplus lkn within 3 months the surplus gets depleted. Ukombozi wa mtumishi wa umma hautapatikana kwa nyongeza ya mshahara bali kutafuta namna nyingine ya kujiingizia kipato nje ya ajira yake
 
Mkiraluliwa ndiomnakumbuka kuungana, mkirushiwa mfupa kama mbwakoko ni cherekochereko na kuungana hakupo.
 
Mkuu Katiba tunayo!
Mkuu katiba tunayo na uhuru tunao. Tunaweza safiri nchi yeyote tunayotaka na kufanya biashara yeyote ile tunayo taka hata kuwa mjasilimali.

Uhuru wa kuiba fedha za umma na kupiga madili ya fedha za umm hapo uko sahihi hatuna, kama huo ndiyo uhuru unao maanisha.

Sisi watanzania tumeamua kufanya kazi kujenga Taifa letu. Nyie wavivu na wezi wa fedha za umma nendeni na bakini huko mliko. Endenden kuwa bebea maboxi wazungu wenu.

Manyanyaso mnayo yapata huko mliko nasikitika hamyaoni, isipokuwa maendeleo yetu mnayazima. Lakini mkoa kusini ujinga wa wazungu.

Msidanganyike! Wazungu hawawataki nyie na wala hawawathamini kama binadam wenzao. Mbwa wao anathamani kubwa kuliko manyani sisi na malimbukeni wao.

Lakini mkifa msituombe michango ya kuwarudisha kwenu. Si mnadai hatuna uhuru. Sasa mtaiachaje miili yenu izikwe kwenye nchi ambayo inawanyanyasa raia wake?
 
Kwa kweli sijutii katika kura zangu tatu,kutoipa CCM hata kura moja.Ni kama nilipata maono.Maana kwa hakika wengi walioisupport 2015 hivi sasa wanajutia.Kwani hakuna kitu kibaya kama kukubali kuwa kibaraka.TUSUBIRI MIRADI MIKUBWA IKAMILIKE.Kama kawaida ripoti za uongo zitaendelea kutamalaki kwa maslahi ya kuwafurahisha viongozi wa Taifa hili.Lakini kwa hakika,matokeo hasi hayataacha kujitokeza katika utendaji kazi wa Taifa hili@kudorora kwa sekta ya elimu nk.Mungu Ibarika Afrika,Mungu Ibariki Tanzania.Ni imani yetu ipo siku historia ya mienendo na matendo yao itawahukumu.NASI TUTAPATA MWELEKEO WA KWELI TUNAOUTAKA.KILA KITU KINA MWISHO WAKE.ALUTA CONTINUA!
 
Kuishi kwa mazoea......Mei mosi si sikukuu ya kuongeza mishahara.
Ni labour Day
Naam ni kweli, mazoea ndio yanatutesa kwasababu kwa miaka mingi ndio imekuwa ikitumika kama siku maalum ya kutangaza nyongeza ya mshahara au kupunguza kodi.
 
Speaking in self can as well mean in person..or first person.

As a leader who is in power out of vote from many. Its ridicule to speak in oneself as the people who put you to that authority would feel betrayed.

Saying

I

I THINK

I WISH

I SUGGEST

I BELIEVE

ON MY SIDE ...ON MY SIDE ...ON MY SIDE...

KWANGU MIMI ...KWANGU MIMI...KWANGU MIMI...

Its a pure feature that tells u decide from yourself..and NOBODY can come your WAY.

We witnessed this today.. At the critical point when workers expected a difference..rather they ended a pain in arsss..

The colours dislayed today utter that Guy ..is PURE DICTATORIAL.

Why does he think that he is the ULTIMATE...

JESUS DIDNT BEHAVE THAT WAY.

WHY IS HE OVER RULLING!??
 
Kama nchi tutafanikiwa tu,pale ambapo viongozi wa Taifa hili wataacha kuchanganya siasa na mambo ya msingi.MWENYE MASIKIO NA ASIKIE.
 
Uhakiki umeisha,sasa tunapisha miradi ya maendeleo.Swali la kujiuliza kama wafanyakazi,ni moja tu.Je,miradi ya maendeleo ikishakamilika tutapisha nini???HAKIKA HII NI NCHI YA VIWONDER!
 
"Mheshimiwa Rais nakuomba hao wanaokushauri kuliliwa shida na wamama kwenye mikutano waamuru waache. Haiingii akilini, kila mkutano mkubwa uliliwe na mmama. Kwanini wababa wasikulilie? Kwanini wasiende kwa wateule wako? Wanakuchafulia image. Kuna protocal za kukufikia. Hizo kiki si saizi yako. Wewe deal na masuala nyeti, mf kabajeti ka ndege moja ka zaidi ya Billion 220 ukikaleta kwetu wakulima, tutakuonesha wonders. Hizo ndege sie wakulima wa magimbi tunaishia kuziona angani ila ndio hao wanyonge unaojinadi kututetea!

Kwa kuwa u msikivu, natumai sitawaona hawa wamama 'feki' wakikusumbua tena. Hizo sanaa waachie wachungaji wetu wa mazingaombwe wapatie sadaka za wasiojielewa"

Asante baba!
 
Back
Top Bottom