Nilifikiri ninachokiona kwenye Nigerian movies mgonjwa anapokataliwa kuhudumiwa mpaka malipo yafanywe kwanza ni maigizo tu, kumbe kwa mwenendo huu pengine hata Tanzania tutegemee hayo waziwazi, unapofika hospitali unaulizwa kwanza unazo pesa ngapi tuanze kukusikiliza? Actually nimeiona kwenye mahospitali tayari kwa aibuaibu, maana lazima ukate kadi kwa kiingilio ndo utamwona dokta ingawa serikali inatupigia makelele kwamba huduma bure hospitali za serikali. Kizazi cha nyoka kimeshazaliwa, tungojee kibaya zaidi hapo mbele kama hatujali.