Meck Sadiki: Viongozi waliopewa madaraka wajipime wakiona hawawezi kuendana na kasi ya Rais wapishe

Ghazwat

JF-Expert Member
Oct 4, 2015
23,718
66,266
Aliyekuwa Mkuu wa Mkoa wa Kilimanjaro, Said Meck Sadiki, amesema ameamua kuondoka Serikalini baada ya utumishi wa muda mrefu na anakwenda kupumzika mkoani Mwanza huku akiwa mfugaji wa samaki.

Aidha, Sadiki alisema pia kulingana na afya yake, anahitaji kupisha vijana wadogo wamsaidie Rais Dkt. John Magufuli kulingana na kasi yake kwani yeye ameepuka kumkwaza Rais wakati wa utekelezaji wa majukumu yake kama mkuu wa mkoa.

Uamuzi huu wa kupumzika nilimuomba rais muda mrefu sana, na nikirudi Kijijini nitaendelea na ufugaji wa samaki maana nilishaandaa bwawa la kufugia, nitaendelea nalo huku nikiwaza jambo lingine la kufanya," alisema.

Sadiki alisema hayo jana wakati wa mahojiano maalumu na Habari leo kuhusu sababu zilizochangia kumuomba Rais Magufuli kuacha kazi yake ya ukuu wa mkoa wa Kilimanjaro.

"Namshukuru Rais kuridhia ombi langu, nimetumikia Serikali tangu mwaka 1999 nikiwa mkuu wa wilaya na baadaye mkuu wa mkoa kuanzia mwaka 2005 hadi sasa ninapoondoka mwenyewe..nimeona ni wakati muafaka kumweleza aliyeniteua kuwa nahitaji kupumzika nikiwa na akili timamu na afya njema", alisema.

"Kama kiongozi muungwana lazima ifike mahali ukiri kwamba wapo vijana wenye uwezo mzuri na kasi ambayo inaendana na serikali ya awamu ya tano.. mimi nilishatekeleza wajibu wangu na mchango kwa serikali yangu, sasa inatosha, tupate mawazo na michango ya wengine", alisema.

Sadiki ambaye amekuwa mkuu wa mkoa wa Kilimanjaro tangu Machi 13,2016 alipoteuliwa na Rais Magufuli, alisema siyo vibaya kwa kiongozi kujitathimini na kuwaachia wengine kama atabaini kasi yake ya utendaji kazi imeanza kupungua.

Chanzo: HabariLeo
 
kasi au chini ya carpet kuna issues,sawa kila la heri mzee

Mkuu just take it kwamba mzee amestaafu. Kwenye viinchi vyetu vya kimaskini hatujazoea kuona watu wanaachia madaraka wenyewe. Lakini kama umejiandaa kwa nini uwe muoga? Mwache mzee akapumzike afuge samaki, acheze na wajukuu zake, aka-catch up na marafiki zake wa zamani ambao bado wako hai.. nk.

Juzi nilisoma mahali UK watu wanaanza kujiandaa na maisha ya kustaafu at the age of 27!

Mzee Sadiki all the best katika maisha yako mapya ya huku uraiani.
 
Back
Top Bottom