Mechi ya Yanga vs Namungo Nkane hakucheza,Siyo match fixing?

Ni Yanga na Biashara. Of course, hiyo ni aina ya fixing asee. Kuna michezo mingi ya kihuni inafanyika katika football ya nchi hii.
Inakuaje hebu elezea maana hata kinyume chake pia ni sahihi, what if hawakumpanga wakihofia kua atacheza kinazi (chini ya kiwango) kuhofia kuwaadhibu waajiri wake watarajiwa?! Lakini pia huoni kua tayari kisaikolojia akili ya dogo iko Yanga halafu umchezeshe against waajiri wake watarajiwa unadhani atakua na utulivu kweli uwanjani?! Kwa mtizamo wangu kutomchezesha ni bora zaidi kuliko km angecheza, maana ingetokea hata amesababisha penalty au red card lazima napo ingeonekana ni match fixing
 
Hakuwa majeruhi na hakupangwa kwenye mechi ,leo kasajiliwa na Yanga,kama siyo match fixing ni nini?
Yanga vs Biashara ,siyo Namungo
Ndo maana tunakataa mmiliki wa timu awe mdhamini wa ligi.
Mkuu mimi binafsi sijakuelewa point yako unaweza ukawa na point nzuri lakini unashindwa kuiweka sawa. Weka sawa ni nini unamaanisha? Hakupangwa kwenye mechi ipi?
 
wazee wa match fixing
Soka kama imekukataa iache siyo lazima ushabikie soka. Katika hali ya kawaida mchezaji anayesajiliwa timu B toka timu A kabla ya kukamilisha taratibu tunaona sehemu nyingi hachezi dhidi ya timu anayokwenda kama mechi iko karibu. Iliwahi kutokea kwa Wayne Roon alipotoka Everton kwenda Man Utd. Pia Waingereza waliwahi kuweka kanuni hata mchezaji aliyesajiliwa kwa mkopo hachezi dhidi ya timu mama siku zikikutana.
Hebu kueni ili muonekane mna busara.
 
Inakuaje hebu elezea maana hata kinyume chake pia ni sahihi, what if hawakumpanga wakihofia kua atacheza kinazi (chini ya kiwango) kuhofia kuwaadhibu waajiri wake watarajiwa?! Lakini pia huoni kua tayari kisaikolojia akili ya dogo iko Yanga halafu umchezeshe against waajiri wake watarajiwa unadhani atakua na utulivu kweli uwanjani?! Kwa mtizamo wangu kutomchezesha ni bora zaidi kuliko km angecheza, maana ingetokea hata amesababisha penalty au red card lazima napo ingeonekana ni match fixing
Achana na huyo kolo hajui kitu kuhusu kabumbu
 
Ni Yanga na Biashara. Of course, hiyo ni aina ya fixing asee. Kuna michezo mingi ya kihuni inafanyika katika football ya nchi hii.
Mimi hata siwaelew wewe na mleta uzi. Match fixing ni pale ambale match hupangwa matokeo kabla ya mechi kuchezwa. Huyo mchezaji laiti Kama angechezeshwa ndipo kungekuwa na hiyo hoja. Hata ulaya ipo hiyo mchezaji wa timu A akiwa anawaniwa na timu B na wapo kwenye hatua ya makubaliano, basi siku ya mechi baina ya timu A na B hapangwi. Na hata mara nyingine wanaweza wasimpange kabisa katika mechi zote zilizosalia ili kuizoesha timu kucheza bila uwepo wa huyo mchezaji.
 
Soka kama imekukataa iache siyo lazima ushabikie soka. Katika hali ya kawaida mchezaji anayesajiliwa timu B toka timu A kabla ya kukamilisha taratibu tunaona sehemu nyingi hachezi dhidi ya timu anayokwenda kama mechi iko karibu. Iliwahi kutokea kwa Wayne Roon alipotoka Everton kwenda Man Utd. Pia Waingereza waliwahi kuweka kanuni hata mchezaji aliyesajiliwa kwa mkopo hachezi dhidi ya timu mama siku zikikutana.
Hebu kueni ili muonekane mna busara.
Mkuu hebu ona kitu kidogo kama icho mtu hawezi kukielewa anakurupuka kuandika uzi hapo vipi ataweza kuelewa sheria ya offside kweli??
 
Soka kama imekukataa iache siyo lazima ushabikie soka. Katika hali ya kawaida mchezaji anayesajiliwa timu B toka timu A kabla ya kukamilisha taratibu tunaona sehemu nyingi hachezi dhidi ya timu anayokwenda kama mechi iko karibu. Iliwahi kutokea kwa Wayne Roon alipotoka Everton kwenda Man Utd. Pia Waingereza waliwahi kuweka kanuni hata mchezaji aliyesajiliwa kwa mkopo hachezi dhidi ya timu mama siku zikikutana.
Hebu kueni ili muonekane mna busara.
Katika siku ambayo jamaa kaonesha ukiazi ni leo. Jamaa katoa boko na hiyo ni hali ya kawaida sana kutokea kama moyo umejawa na chuki maana kazi kutafuta sababu tu. Dabil Yanga msimu huu wamekufanya uwe na gubu
 
Back
Top Bottom