Mdude Nyagali atoa lecture ya road license kwa wasafiri

OKW BOBAN SUNZU

JF-Expert Member
Aug 24, 2011
33,457
2,000
Nilikuwa nikisafiri kutoka Smbuwanga mkoani Rukwa to Mbeya,.Nilipanda mabasi makubwa yanayofanya safari zake Sumbuwanga to Dar es salam.

Nilikaa karibu na dereva kuna dada mmoja alikaa nyuma yangu alianzisha mjadala kwa kuiponda bajeti ya serikali ya 2017-2018 kwamba haijazingatia maisha ya wananchi na badala yake inawaumiza wananchi kutokana na mfumuko wa bei unaopanda kila siku..Lakini dereva wa basi akaisifia bajeti kwa kuondoa mfumo wa kulipia keshi TRA Motor Vehicle road Licence moja kwa moja badala yake motor vehicle italipwa pale unaponunua mafuta ya gari yako kwa lita Tsh.40 itakatwa malipo ya road license.

Kwa kuwa nilikuwa nimekaa jirani na dereva nikamuuliza na maongezi yalikuwa hivi

MDUDE;; kuilipia motor vehicle kwa mfumo uliokuwepo awali na sasa kwa mfumo wa kutozwa Tsh.40 kila lita upi mfumo una unafuu?

DEREVA;;mfumo wa sasa una unafuu kwani kulipa 40 kila lita ni hela ndogo.

MDUDE;;; kwani kwa mfumo wa awali kulipia motor vehicle kwa gari basi kubwa kama hili ilikuwa shilingi ngapi?

DEREVA;;;kwa mabasi makubwa kama haya motor vehicle tulikuwa tunalipia (300,000) laki tatu kwa mwaka mzima.

MDUDE;;;je dereva unajua mfumo wa sasa kwa basi hii mtalipia shilingi ngapi.?

DEREVA;;sijui kaka lakini naamini haiwezi kuwa kubwa kuliko tuliyokuwa tunalipa awali laki 3 ni kubwa mno.wakati sasa tutakuwa tunalipia Tsh,40 arobaini tu kwa lita.

MDUDE;;Hii basi yenu inatumia lita ngapi kila siku kwa safari zenu mnazofanya za sumbuwanga to dar es salaam?

DEREVA;;Basi yoyote kubwa inayoanzia sumbuwanga kwenda dar kila siku inatumia lita mia nne (400 liters)

MDUDE;;Sasa chukua lita 400 unazotumia kila siku zidisha mara Tsh.40 tozo ya moto vehicle utapata pesa unayolipa motor viehicle kwa siku halafu chukua pesa hiyo ya motor vehicle unayolipa kwa siku zidisha mara siku 30 ili ujue kwa mwezi unalipa sh.ngapi halafu utazidisha mara miezi 12 ili ujue kwa mwaka unalipa shilingi ngapi halafu ulinganishe na hiyo laki 3 uliyokuwa unalipa awali.

DEREVA ;;Kwa kuwa naendesha gari naombeni abiria yoyote apige hesabu hii ili tujue lakini wewe uliyeleta wazo hili (mimi)usipige hesabu unaweza kutudanganya

Dereva hakutaka mimi ndio nipige hesabu kwa kuwa mimi ndiye niliyetoa wazo hivyo akatokea abiria mmoja aliyekuwa amekaa siti namba 4 nyuma ya dereva na akapiga hesabu na hesabu ilikuwa hivi.

Lita 400 x Tsh.40 ya malipo ya motor vihicle = Tsh.16,000/- kwa siku.
Inamaana mabasi yote makubwa yanayoanza safari zake sumbuwanga mkoani rukwa to dar es salaam yatakuwa yanalipia motor vehicle kwa siku Tsh.16,000/- elfu kumi na sita.

Sasa chukua shilingi 16,000/- zidisha mara siku 30 yani mwezi mzima 16,000 x 30 =480,000/-

Inamaana mabasi yanayoanzia safari zake sumbuwanga to dar es salaam yatakuwa yanalipa motor vehicle Tsh.480,000/- laki nne na themanini elfu kwa mwezi.

Sasa ili kupata hesabu ya mwaka kwa kuwa awali mfumo huu ulikuwa unalipwa kwa mwaka unazidisha Tsh.480,000 malipo ya motor vihicle ya mwezi zidisha mara miezi 12 ya mwaka mzima 480000 x 12 = 5,760,000 milion tano laki saba elfu 60 kwa mwaka mzima wa malipo ya motor viehicle ya basi moja kwa mabasi yanayotoka sumbuwanga kwenda dar es salaam.pesa ambayo inatosha kununulia gari ndogo aina ya passo kwa matembezi ya familia.Lakini umelipa road license aahaaa serikali ya wanyonge

Nikamuuliza dereva kuwa kati ya laki 3 uliyokuwa unalipa awali kwa mwaka na hii milion 5 utakayoanza kulipa sasa kwa mwaKA mzima ipi kubwa?Dreva hakunijibu chochote ila alimuambia kondakta anirudishie elfu 14 pesa niliyokuwa nimelipa nauli kutoka sumbuwanga to songwe.Na wakati nashuka stand dada aliyeanzisha mada ya kuiponda bajeti amenipa elfu 10 ameniambia nikanywe soda nimenunua maini hapa nataka nikatengeneze mchemsho na viazi mviringo hivi.

Ushauri ninaowapeni ni usishabikie kitu usichokijua ila ninachoshukuru ni kwamba magari ya serikali ambayo hayajawahi kulipa motor vihicle road license kuanzia halmashauri mpaka ikulu yale ma-land cruiser VX,V8 mashangingi nayo yataanza kulipa kwa bajeti ya mwaka huu ni mwendo wa kuisoma namba tu

Tuonane 2020.

Mdude nyagali.
 

wegman

JF-Expert Member
Jan 8, 2016
1,131
2,000
Dude Limeamshwa , Hili swala kuna watu inakula kwao na kuna watu wanafaidika nalo sema tu sababu hela yenyewe inalipwa indirect ndio maana kwa juu juu haliumizi kichwa ila ukilichambua kiundani kama hivyo juu hapo kuna watu wanaumia bila kujua, ila ndio hivyo tuchape kazi maisha yasonge.
 

Zanzibar Spices

JF-Expert Member
Jul 14, 2013
7,381
2,000
Chadema itawafutia kodi zote na nchi itaendeshwa kwa hela za Richmond...Chagua CDM 2020 kwa uongozi wa kusadikika.
Hahaha,hili ndio wanalotaka
Chama chenyewe wachumi wao vimeo,hata budgets zao mbadala huwa zimekaa ki Tom and Jerry.
 

mycall

JF-Expert Member
Dec 17, 2014
848
500
Kwa kuwa bado ni mapendekezo, wabunge wasituangushe ,sh 40 kwa litre ni nyingi sana ! Waishauri Serikali hii ya wanyonge iwe sh.5 kwa litre.
 

ureni

JF-Expert Member
Jun 14, 2011
1,263
1,250
sijaona kitu cha kushangaza hapo ila mtoa mada ndio anashangaza,Jaman mlitaka wenye mabasi wasilipe kodi kila mtu atachangia kodi kadiri anavyotumia barabara ni vema kabisa ilivyowekwa kwenye mafuta ili kila mtu achangie tupate maendeleo kwa haraka naona watu hawataki kabisa serikali ipate kodi kwa nin lakini?maendeleo tutapataje?yaani mnazuia serikali isipate kodi hapo hapo utasikia watu wanataka maendeleo watz waajabu sana
 

Cute shy

JF-Expert Member
Apr 27, 2015
1,151
2,000
Dude Limeamshwa , Hili swala kuna watu inakula kwao na kuna watu wanafaidika nalo sema tu sababu hela yenyewe inalipwa indirect ndio maana kwa juu juu haliumizi kichwa ila ukilichambua kiundani kama hivyo juu hapo kuna watu wanaumia bila kujua, ila ndio hivyo tuchape kazi maisha yasonge.
haka kahela kangu ngoja nikanunue kakiwanja kuliko nijifirisi kwa gari
 

wegman

JF-Expert Member
Jan 8, 2016
1,131
2,000
haka kahela kangu ngoja nikanunue kakiwanja kuliko nijifirisi kwa gari
Kama unataka nunua ka mizunguko ya hapa na pale nunua tuuh mkuu usiogope panga la kulipia Mil 5 kwa mwaka alitokupata ila kiwanja ndio muhimu KWANZA.
 

Toa taarifa ya maudhui yasiyofaa!

Kuna taarifa umeiona humu JamiiForums na haifai kubaki mtandaoni?
Fanya hivi...

Umesahau Password au akaunti yako?

Unapata ugumu kuikumbuka akaunti yako? Unakwama kuanzisha akaunti?
Contact us

Top Bottom