Mdahalo wa katiba St Augustine university

televisheni Gani Itarusha Tuone tulio mbali? Saa ngapi?
 
Thread bado hajakamilika tunaomba taarifa kamili. Kuhusu wasemaji wakuu, tv itakayorusha kama kuna mpango huo nk. Tafadhali!
 
Star tv na rfa wanarusha live kuanzia saa 3. Nipo ukumbini nitawaarifu yote yatakayojiri hapa. Mdaharo umeandaliwa na LHRC.
 
Kuna ucheleweshwaji wa muda kidogo bado mpaka sasa mtoa mada hajajulikana na mgeni rasmi bado hajaingia ukumbini. Mada kuu tajwa ni "UKIUKWAJI WA HAKI ZA BINADAMU NA KATIBA MPYA" Je wadau kama nitapata fursa, ni maswali gani ya msingi niulize kwa niaba ya wale wote ambao hawajatata nafasi ya kuhudhuria mahali hapa.
 
Mwendesha mdaharo ni Paul Mabuga yule mtangazaji wa star tv. Mtoa mada ni profesa Maina toka LHCR. Naomba muwe tayari kwa kuona kwa star tv na radio SAUT.
 
Naaam mdahalo ndo umeanza: mada kuu ni hz:
1. Rasilimali na katiba mpya.
2. Muungano na katiba mpya.
Mtoa mada ni prof Chris Maina Petter kutoka UDSM/ZLSC pamoja na
Dr. Makulilo wa udsm.
 
Wazungumzaji wakuu ni Adv Francis kiwanga(mkurugenzi wa LHRC),Adv Harold Sungusia(mkurugenzi wa maboresho ya sheria),Rev. Dr. Charles kitima(makamu mkuu wa chuo SAUT),Prof. Chris Maina,Dr Makulilo
 
Naona mkuu wa kitivo cha sheria Dr kilangi anawakalibisha wageni
 
Dr kitima anasema utamaduni wa kukataa kuachiana madaraka ndiyo unaosababisha makelele
 
Prof Maina "haki za rasilimali hazipo kwenye katiba,anasema tuliangalie hili kwenye katiba mpya,mikataba yote inayohusu rasilimali iwekwe wazi kwa wananchi
 
mambo ya kuzingatia:
1. Kuwepo kwa katiba mbili ya Zanzibar na ya jamhuri.
2. Kuongezeka kwa mambo ya muungano.
3. Manufaa na hasara za muungano.
 
Back
Top Bottom