Nonda, inabidi uangalie jambo hili kwa uwiano. Tanganyika inamuona ZNZ kama mshiriki wa muungano na kutazama mazingira yaliyopo kiuchumi, kiutamaduni na kisiasa.
Kiuchumi siku zote Tanganyika imeangalia ZNZ kwa udogo wake na pengine kujiuliza watu milioni 1.5 ni sawa na wakazi wa Ilala, hivyo ni rahisi wao kuchanganyika na Tanganyika bila kuiathiri Tanganyika ingawaje kinyume chake kina ukweli.
Utakapokaa meza moja na ZNZ na kuwaambi wachangie bajeti sawa ya nchi au ya muungano ni kukosa fikra.
Tanganyika inaona ni rahisi ku-accomodate ZNZ katika soko la biashara na ajira tofauti na itakavyoiangalia Kenya au uganda. Ni hakika si ZNZ tu hata nchi kama Burundi na Rwanda zinaangaliwa kwa jicho hilo.
Mathalani, kisisa, inajulikana kuna Warundi na Wanyarwanda wengi sana wanaishi bila bughudha ili mradi tu wanazingatia taratibu za nchi. Wote kama WZNZ ni wafaidika wa Tanganyika bila kuathiri Tanganyika kwasababu ya ukubwa na population. Lakini pia Tanganyika inafahamu vema ZNZ kisiasa.
Kiutamaduni ZNZ ina bahati sana kwasababu ipo karibu sana na Tanganyika kuliko nchi nyingine. Hata Uarabuni MZN hathamiwi kama anapokuwa Tanganyika. Aghalabu utasikia nenda kwa mpenda au Yakhe na wamejaa kila kona ya nchi hii. Pamoja na mambo mengine ya kijamii mwingiliano wa lugha na dini vimesadia sana.
Kwa mantiki hiyo Mzanzibar anaoenekana kama ndugu zaidi Tanganyika kuliko raia wa nchi nyingine ya ukanda huu.
Tatizo limeanza kujitokeza huko nyuma pale ZNZ walipoona wao ni bora zaidi kuliko Tanganyika na wana upper. Unakumbumbuka walianza na kuweka vikwazo vya Passport. Hapo Tanganyika ikaona undugu ni wa mashaka na kuwaambia WZNZ waje kwa passport. Hilo tu lilikuwa ujumbe tosha na wzn walinywea. mpaka leo
ZNZ imekua inalalamika hata pasipo na mashiko cha kushangaza hakuna maendeleo yanayotokana na wao kujiona bora zaidi au kuendeleza chuki na ubaguzi sifa za awali za wale wanotajwa na vitabu vitakatifu kuwa kama unafiki.
Kelele za sisi si koloni, wimbo wa taifa, bendera, chama cha mpira, CHANEZA, tunaibiwa kodi TRA, tunataka hela zaidi tusomeshe watoto wetu, hatulipi umeme n.k. Kibaya zaidi kuanza kuwachoma moto Watanganyika na kuweka sheria za kuwabana wao na si raia wa nchi nyingine, zimewaamsha Watanganyika wengi waliokuwa hawajali sana uwepo wa ZNZ.
Tanganyika haiwezi kuwafukuza wznz kwa kuona hawa ni ndugu zetu kwa mambo mengi, wanatutegemea, tumewakaribisha na tunawagharamia kama wao wanaona kuna walakini hewala warejee kwao.
Ndiyo wanasema znz ikitaka chochote ruksa hata leo wakiondoka katika muungano radhiaya marwidhaiyatan.
Maana ya haya ni kuwa kama umeamua kubeba mizigo nani atakukataza.
Ukarimu wa Tanganyika ni kwasababu hakuna cha kupoteza na ZNZ wanaodhani wanapoteza basi waamue.
Pia ina maana kuwa hakuna sababu ya kumchoma mznz moto wala kumuita malaya, jambazi n.k kama wanavyofanya wznz kwa kujua udhaifu wa ZNZ hasa katika ustaarabu.
Njia ya kuwafukuza wznz ni ya kisayansi tu ambayo ni kuweka masharti muhimu katika mambo yanayowagusa.
Kwa bahati nzuri Wznz wanaingia katika mtego huo. Ukiomba Tanganyika maana yake umefunga milango.
Tanganyika itawaangaliwa Watanganyika kama ZNZ inavyowaangalia watu wake.
Ukitaka mkataba Tanganyika itauliza unaweka nini mezani? mkataba wa nini. Kama hakuna mkataba, serikali 3 ua mbili maana yake ZNZ kwaherini. Kunasababu ya kumfukuza mtu hapo?
In other words, stay if you want, go if you decide.ZNZ wanaweza kuondoka any time na ni haki yao.
Je, umeona jinsi walivyobadilika ghafla. Abiria wanaomba nahodha abadili uelekeo. Serikali 3, mkataba, Uswiss, EU, Muungano wa New York na Cuba n.k.
Ni nani anayeng'angania muungano, yule anayedai serikali 3, mkataba wa Hawaii na Ghana au yule anayesema hey, please make up your mind otherwise pack and go!
Kwa muktadha huo Tanganyika haina sababu ya kuwafukuza Wznz. Inabana kidogo tu watasalimu amri kama walivyosalim wakati wa Passport, kama wanavyosalim sasa kwa kudai serikali 3 au mkataba wa Haiti na Congo.
Hakuna sababu wa kutoa povu, ni kukaza uzi kidogo tu. Seif keshatambua ugumu, Ali Salehe anajua, Ahmed Rajab la haulaa!! huyu ndiye amejisalimisha kabisa anasema tujadili aina ya muungano, kiburi na uchochezi wa kuvunja kwisha.
Sasa kunasababu ya kumfukuza mtu anyesema chonde chonde! Wakitaka waondoke, wakikubali wawe na nidhamu na kusema kwa kutumia mdomo na kichwa. Wadai wanachostahili na wakatae wasichostahili.