Mdahalo Azam Two: Wagombea ubunge jimbo la Kawe

Mdahalo Azam Two: Wagombea ubunge jimbo la Kawe

Msulibasi

JF-Expert Member
Joined
Dec 2, 2014
Posts
5,957
Reaction score
8,005
Nangalia hapa mdahalo Janeth Kaulizwa maswali amepaniki sana .Mdee ameelezea mafanikio aliyoyapata na changamoto zake na watu wamekubali. Janeth kaulizwa elimu yake kapanic zaidi hajajibu kasema elimu ni kujua kusoma na kuandika akaahidi kutaje elimu yake ila hajataja.

Kipi Warioba kaingia mtini hajatokea kwenye mdahalo.

-Mdee

amesadia eneo la Tanganyika parkers kurudi serekalini kutoka kwa Adamjee na mafisadi wakubwa wa ccm-mji mkubwa unajengwa pale sasa.

mgogoro wa chasimba na kiwanda cha saruji umeisha nilisalitiwa na wabunge wa ccm na waziri lakini tukalimaliza nguvu ya umma

vijana 4000 wa magereji waliokuwa wananyanyaswa Kinondoni swala hilo nimelifikisha wizarani mda si mrefu litakwisha. Akija Lowasa magereji yatapeta

kulikuwa na mgogoro wa kawe na jeshi kuhusu mipaka, nikawasiliana na waziri wa ulinzi na mambo yakaisha-makoooofiiiiiiiiiiiiiiiiiii

chama cha wananchi hakina hela wenye hela ni wananchi wanatoa kodi na wana haki ya kudai huduma.


Barabara ya mbezi kwa mnyika ilishashindikana sasa injengwa kiwango cha lami

tumejenga madaraja Goba ingawa barabara ya changarawe-makofiiiiiiiiiiiiiiiiiiiiiiiiiiiiii

mdee; tumetandaza mabomba wazo hili huko ya mm 600, 200 nk hata hivyo tumepiga pressure na bomba kuu la maji kuja DSM limefikia 90% na yakifika mabomba yapo tayari. Mgombea PPT maendeleo anamuunga mkono Lowassa wa UKAWA

mgombea wa chama cha Lifa Chipaka kasema anamuunga mkono Lowassa na anamlaumu mwenyekiti wake Lifa kwa kubaki kwenye bunge la katiba badala ya kuungana na UKAWA kadai hata mwenyekiti wake angegombea urais asingempa kura hata dunia iishe

yeah huyu dada wa ACT kaulizwa kuwa mbona ulikusanya 8000 kutoka kwa wakina mama hujazirudisha -amesema anafanyiwa siasa chafu na wanatakiwa kuangalia shepu yake kama ni ya mtu wa kuchukua 8000 za wanawake. Amedai mbunge hakuweza kusaidia kituo cha walimu lakini yeye ameweza kwa kutoa computer na printer anadai katoka CDM ndio maana wanamfanyia sisisa chafu ameshangiliwa na jamaa watatu wamevaa zambarau

Huyu Mboni anaongea mambo ya mgombea urais -kujenga fly-over,kununua boti nk .kasema atanunua treni kama ndege CCM imewapumbaza mnaona kila kitu hakiwezekani, haya mambo si ghali ataongea na wabunge wa ulaya ni easy tu watu wanavunja mbavu.

halima Mdee anaulizwa maswali -kwamba mbunge ameuza uwanja wampira hapo mbezi milioni 30-Halima anaulizwa na mkazi wa Mbezi juu uwanja wa jogooo.

halima,anajibu swali la kwanza juu ya hati za chasimba-anadai commitment ya kutoa ahadi ilitolewa na Lukuvi ambaye ni waziri wa serekali-ujumbe wako umefika na ni somo kwa wananchi juu ya ahadi za maccm.


kuhusu taarifa ya kazi zangu nilizofanya -nita tengeneza taarifa kama hicho kitabu ili kutoa mrejesho naomba uwe utaratibu wa viongozi wote tanzani

kuhusu foleni feeder roads barabara mchepuko tumesimamia za mchepuko anazitaja goba ,msewe kiwango cha lami


Uwanja wa mpira: Kata ya mbezi juu si eneo la makazi ni maalum kwa viwanda.Kuna eneo lilimilikishwa kwa mtu kihalali 2003 suala likawa mahakamani. eneo la viwanda likageuzwa eneo la makazi.ule uwanja umetumika kama uwanja wa michezo. lakini jamaa ana hati toka 2003. Kamanga mi sio mpigaji ningekuwa mpigaji ningekuwa bilionea anamwambia mtangazaji. anashauri kuwa wananchi wajiandikishe waombe ubatilishaji wa matumizi ya ule uwanja-asanteni wakuu
 
umeme..... umeme tanesco mnatufanya vibaya. toka jana umeme haurud hv hayo matengenezo bado ndugu zetu
 
Huyu wa ppt maendeleo anasema Kawe wanalima matikiti atajenga kiwanda cha kutengeneza juisi ya tikiti.
Atajenga fly over kwa kupata pesa toka ughaibuni
 
Huyu wa ppt maendeleo anasema Kawe wanalima matikiti atajenga kiwanda cha kutengeneza juisi ya tikiti.
Atajenga fly over kwa kupata pesa toka ughaibuni

Dah huyo kiboko ametisha
 
Huyu wa ppt maendeleo anasema Kawe wanalima matikiti atajenga kiwanda cha kutengeneza juisi ya tikiti.
Atajenga fly over kwa kupata pesa toka ughaibuni

Huyu katisha aisee
 
Mdee ameulizwa maswali magumu kayachomoa yote watu wamebaki kupiga makofi pwaa pwaa pwaa kweli ukawa wana wabunge wenye uelewa mkubwa sana.
 
Mkuu hamna kitu ,umeme unatusumbua na walisema kuanzia leo tungefurahia kuwa na umeme lakin mpaka muda huu ni giza tu

Poleni sana ila kwetu leo huku umeme upo...labda kesho watakata kama kawaida yao weekend
 
Mboni jiliwa eti nae ni mgombea ubunge!! Kazi ipo
 
Mboni jiliwa eti nae ni mgombea ubunge!! Kazi ipo

Kiukweli kabisa NEC sijui ni vigezo gani wanatumia kupitisha hawa wagombea yaani wengine kujieleza hawajui kabisa.
 
Back
Top Bottom