Mchwa anapokaribia kufa huota mbawa....

Mchwa anapokaribia kufa huota mbawa....

maggid

JF-Expert Member
Joined
Dec 3, 2006
Posts
1,084
Reaction score
1,251
Ndugu zangu.

KUNA miongoni mwetu tumemsoma mwanafasihi Shaaban Robert. Kuna mahali kwenye kitabu chake ‘ Kusadikika’, Shabaan Robert anamwelezea mchwa anayekaribia kufa.

Kwamba huota mbawa. Hukiacha kichuguu . Yumkini ataruka juu sana. Atakwenda mbali. Lakini, huko angani hufika mahali, mbawa hupukutika. Mchwa ataanguka chini. Mbali na kichuguu.

Hapo, mchwa hukabiriwa na hatari kubwa. Hawezi kuruka tena, na yu mbali na kichuguu. Na kichuguu ni taasisi. Hivyo, mchwa anaweza kuliwa na kinyonga, au hata chura. Na akinusurika na wawili hao, aweza kukanyagwa na unyayo wa mwanadamu, au hata tairi la baiskeli. Mchwa atakufa.

Naam, mengine tuyafanyayo hupelekea maanguko yetu. Hata kama mwanzoni huonekana kutupaisha juu angani.

” Nafikiri, ndio maana naishi”- Anasema mwanafalsafa Rene Descartes.

Na maarifa ya Sayansi yanatusaidia kuyabaini mahusiano kati ya dunia tunayoishi na mazingira yanayotuzunguka. Hiyo ni falsafa ya kivitendo. Ndio iliyo bora kuliko ile dhanifu- Speculative.

Mengine yanayotokea katika jamii ni ya dhahiri kabisa. Ni ukweli. Na jambo la kweli hata likifanyiwa hila, basi, hatimaye hila hushindwa.

Maana, hila na ghilba huuchelewesha tu ukweli kuweza kudhihiri, lakini, kamwe haviwezi kuuzuia.

Ni Neno La Leo.
Maggid.
MjengwaBlog :: Habari, Picha, Matangazo na Matukio
 
Unamaanisha Kifo cha Maccm au?
 
Ujasomeka mkuu,jaribu kufafanua ulikuwa unamaanisha nini?
 
Ngoja niwanong'oneze wakuu, anamaanisha hiviii, kifo cha "mchwa chadema" eti kimekaribia! jamani huyu jamaa si atakuwa muongo?
 
Fasihi za kiccm...ujinga ujinga tu, si ukanywe hata pombe kuliko kuleta hadithi za akina wasira hapa...eti chadema itakufa baada ya miezi 6, mara chadema ni wahuni...ujinga ujinga tu, miaka 50 mko madarakani lakini bado majinga majinga tu...
 
Ni kweli Shaaban Robert alikua na upeo mkubwa sana wa kuona mbali maana kwenye kitabu chake cha kusadikika kuna sehemu anamzungumzia mjumbe wa kaskazini mwenye nywele za kung'aa kama dhahabu na ambaye anaamini kwamba ana akili kuliko wana kusadikika wote na ambaye anaondolewa na mwanasheria ila anamkebehi ila hali hajui sheria hata kidogo.
sasa utaona utawala wetu ulipofikia na utajaribu kumtafuta mjumbe wa kaskazini wa disaini hiyo.
 
Anguko la ccm

Sent from my BlackBerry 9300 using JamiiForums
 
Ni kweli Shaaban Robert alikua na upeo mkubwa sana wa kuona mbali maana kwenye kitabu chake cha kusadikika kuna sehemu anamzungumzia mjumbe wa kaskazini mwenye nywele za kung'aa kama dhahabu na ambaye anaamini kwamba ana akili kuliko wana kusadikika wote na ambaye anaondolewa na mwanasheria ila anamkebehi ila hali hajui sheria hata kidogo.
sasa utaona utawala wetu ulipofikia na utajaribu kumtafuta mjumbe wa kaskazini wa disaini hiyo.

unajua waandishi wa zamaniwalikuwa na akili na kuona mbali sana,huyo mjumbe wa kaskazn na nywele nyeupe yupo,katoroka kchuguuni,karuka mbawa zimekatika sasa anajisafisha kwa kina mijusi,vyura,wamsaidie hasikanywage na baiskeli 20015.
 
Huyu mleta uzi kwa kujikomba ndio mwenyewe hapo amefikiri lakini kwa vile akileta ujinga wanaJF huwa wanamzaba za uso anashindwa kujiweka wazi sikuhizi mnafiki mkubwa
 
ccm ndio muchwa uliokatika mbawa kwani hakina sera wala dira; kama kina dira kisingeajiri nepi na mwingulu ambao bado wako kwenye foolish age: matokeo yake kila siku uzushi mpya na mbinu za kigaidi: ona walivyomungiza mchina wa watu, sasa anajuta kuifahamu Tanzania maana kibarua chake kipo hatarini
 
Ndugu zangu.

KUNA miongoni mwetu tumemsoma mwanafasihi Shaaban Robert. Kuna mahali kwenye kitabu chake ' Kusadikika', Shabaan Robert anamwelezea mchwa anayekaribia kufa.

Kwamba huota mbawa. Hukiacha kichuguu . Yumkini ataruka juu sana. Atakwenda mbali. Lakini, huko angani hufika mahali, mbawa hupukutika. Mchwa ataanguka chini. Mbali na kichuguu.

Hapo, mchwa hukabiriwa na hatari kubwa. Hawezi kuruka tena, na yu mbali na kichuguu. Na kichuguu ni taasisi. Hivyo, mchwa anaweza kuliwa na kinyonga, au hata chura. Na akinusurika na wawili hao, aweza kukanyagwa na unyayo wa mwanadamu, au hata tairi la baiskeli. Mchwa atakufa.

Naam, mengine tuyafanyayo hupelekea maanguko yetu. Hata kama mwanzoni huonekana kutupaisha juu angani.

Labda jambo moja ambalo Shaaban Robert hakutaja kwenye kisa cha mchwa ni kwamba huyo mchwa anayepukutika mabawa na kukaribia kufa anaweza asife bali akakutana na mchwa dume waakanzisha kichuguu kingine na akawa malkia.

Huyo mchwa anajua kuruka kuna risk, lakini pia kunaweza kukaleta faida kwa yeye kuwa malkia kama vile tu mchwa aliyemtaga yeye kwamba naye alipaa, akapukutika mabawa lakini hakuliwa bali alikuja kuwa malkia.

Ndio maana hadi leo mchwa hawajaisha na vichuguu vinaongezeka, kwa kuwa si mchwa wote wanaishia kuliwa na vyura au vinyonga, wapo wanaokuwa malkia.

Mchwa mwoga na abaki ndani ya kichuguu, ambako hatakiwi tena na atakufa tu.
 

Similar Discussions

Back
Top Bottom