Mchungaji wa EAGT awaonya wanaokwepa kodi ya serikali

Mchungaji wa EAGT awaonya wanaokwepa kodi ya serikali

diana chumbikino

JF-Expert Member
Joined
May 29, 2018
Posts
428
Reaction score
368
ulipaji.jpg



MCHUNGAJI Kiongozi wa Kanisa la Evangelisim Assembless Of God Tanzania (EAGT) Ipagala, Evanc Chande, amewaonya wafanyabiashara, wakulima na waumini wa dini mbalimbali wanaokwepa kulipa kodi ya serikali na kusema kuwa kitendo hicho ni dhambi mbele za Mungu.

Chande alitoa onyo hilo katika ibada maalum ya kumshukuru Mungu iliyofanyika kanisani hapo kwa lengo la kuwaombea waumini wa kanisa hilo wakiwamo wafanyabiashara, wakulima na wanafunzi, ili kufanikiwa kwenye shughuli zao za kiroho na kimwili kwa kipindi cha mwaka 2019.

Ibada hiyo ambayo iliambatana na shukrani mbalimbali za kumshukuru Mungu kuvuka salama mwaka uliopita na kuingia mwaka mpya, mchungaji huyo alisema, serikali imekuwa ikihimiza ulipaji wa kodi, hivyo ni muhimu kutekeleza badala ya kuingia kwenye dhambi ya kukwepa kulipa. Alisema kuwa ni aibu kwa wafanyakazi, wakulima na waumini ambao wanamcha Mungu, kukwepa kulipa kodi ya serikali kwa kuwa kwa kufanya hivyo watakuwa wakiliibia taifa na kusababisha kushuka kwa maendeleo ya nchi,

“Lakini kwa kuwa kodi ni jambo la kimungu Yesu aliweza kuwajibu kwa kusema “Iko wapi hiyo sarafu baada ya kumwonyesha aliwauliza hii sarafu ina sura ya nani nao wakamjibu kuwa ina sura ya Kaisali akawajibu cha Kaisali mpe Kaisali na cha Mungu mpe Mungu,” kwa maana hiyo kodi ni agizo kutoka kwa Mungu,'' alisema Mchungaji Chande.

Kuhusu uadilifu, mchungaji huyo aliwataka waumini wa kanisa hilo ambao wapo maofisini na kwenye maeneo mengineyo katika ajira mbalimbali kuhakikisha wanafanya kazi kwa misingi ya uaminifu na kujituma. Mchungaji huyo pia alisema kuwa mwaka 2019 kwa upande wao utakuwa wa mabadiliko makubwa sambamba na kuhakikisha wanaiombea amani ya nc
hi kutochezewa na kuilinda kwa gharama zote. Akizungumza na wanafunzi wa vyuo vikuu aliwataka kusoma zaidi huku wakiepukana na vishawishi vya kuanzisha migomo.
 
Huko Ni Kujipendekeza Kwa Kaisari, Mambo Ya Kaisari Aachiwe Kaisari Mwenyewe
 
Angeeleweka kama na kanisa lake linalipa kodi.
 
Wachungaj waskuhizi Wahuni tu,

Sasa Kama pesa ni ya Kaisari

Kwann huwa wanatutaka tumtolee Mungu wetu Zaka kwa kutumia pesa ya Kaisari?

Simple Logic

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Pastor anasisitiza watu walipe Kodi wakati yeye mwenyewe na Kanisa lake hawalipi Kodi.

Huu ni upuuz wa kiwango cha Makinikia


Sent using Jamii Forums mobile app
 
Back
Top Bottom