Mchungaji afungwa kwa ubakaji

Mchungaji afungwa kwa ubakaji

Status
Not open for further replies.

Kibo10

JF-Expert Member
Joined
Aug 20, 2013
Posts
11,278
Reaction score
8,868
Kiongozi wa kanisa moja nchini Zimbabwe amehukumiwa kifungo cha miaka 40 jela kwa kosa la kuwabaka wanawake watatu na kukutwa na vifaa vya kuchochea kujamiiana.

Kiongozi huyo, Martin Gumbura (57) wa Kanisa la RMG Independent End Time Message alitiwa hatiana katika makosa manne ya ubakaji kwenye mahakama ya mjini Harare. Gumbura ana wake 11 na watoto 30 na aliiambia mahakama kwamba alikuwa akitarajia kupata watoto 100 katika maisha yake.

Wake zake wote walikuwa wakihudhuria mahakamani hapo wakati wa kesi hiyo na walikuwa wakijumuika na watu wengine waliokuwa wakihudhuria makahamani hapo hadi siku hukumu ilipotolewa.

Alihukimiwa kifungo cha mika 50 jela lakini miaka 10 imepungizwa katika adhabu hiyo baada ya kuonyesha tabia njema wakati wa kesi hiyo.

Hukumu nyingine ya kifungo cha miaka minne jela kwa kukutwa na vifaa vya kuchochea kujamiiana itatumikiwa sambamba na hukumu hiyo ya kifungo cha miaka 40. Waendesha mashtaka waliiomba mahakama kwamba Gumburu anatakiwa ahukumiwe kifungo cha miaka 25 jela kwa kila kosa, lakini hakimu alieleza kwamba hana mamlaka ya kutoa hukumu ya kifungo cha muda mrefu namna hiyo.

Hakimu huyo alimwelezea Gumbura kama mbwa mwitu aliyevaa ngozi ya kondoo ambaye amekuwa akiwaghilibu waumini wa Kanisa hilo.

“Mahakama imejaribu kutoa adhabu ambayo itawatendea haki wote, malalmikiwa na walalamikaji. Mtuhumiwa hutu ni kama mbwa mwitu aliyevaa ngozi ya kondoo,” alisema.

“Msingi wa huduma ya Kanisa ni kumwabudu Mungu na si kuzini na mabinti na wanawake na kuwatishia kwamba kwa kutofanya hivyo watapatwa na balaa,” aliongeza hakimu huyo.

Alisema ni wajibu wa wachungaji na wasimamizi wa kanisa kujua kuhusu madhila yanayowakumba waumini wao, pia kujua udhalilishaji na unyanyasaji wa kijinsia unaowakumba wanawake na kutafuta namna ya kuukemea.

Awali Gumbura alikuwa akikabilwia na mashtaka tisa ya kuwalaghai na kuwabaka wanawake sita lakini alifutiwa mashtaka manne yaliyowahusisha wanawake watatu kutokana na kukosekana kwa ushahidi wa kutosha.

Hivi karibuni, mtu mwingine mjini Harare alihukumiwa kifungo cha miaka 290 jela kwa kosa la kuwadhalilisha na kuwabaka wanawake 13. Mtu huyo, Thomas Chirembwe (30) alitiwa hatiani kwa makosa 21 ya ubakaji na ujambazi wa kutumia silaha baada ya mfululizo wa matukio yaliyoutikisa mji wa Harare.

Kwa mujibu wa takwimu za polisi, zaidi ta watoto 400 walibakwa na wanawake 392 walinyanyaswa kijinsia mwaka 2013, ambapo wanawake walibakwa wakiwa njiani na watoto wengi walibakwa na majirani au watu wao wa karibu.
 
Ndio viongozi wetu wa dini wa dunia ya leo hii ni hatari sana, ee mwenyezi mungu tujaalie sisi waja wako kuweza kukuogopa na kujiepusha na mambo yasiokupendeza!
 
mchungaji martin naye alibakwa na hao wanawake kwakumpitia na vimin na vipedo.mbona wao hawakula miaka "is not fare
 
Dah amakweli dunia yetu inaelekea ukingoni yaani kiongozi wa dini kawa Shetani namna hiyo?
Wala sio eti anashida au amezidiwa lah.. niwazimu tuu,Wake 11 bado unataka tuu alafu eti anataka watoto 100 eti kabla haja hajafa sasa atawapatia huko huko Lupango K****e.
 
Lakini matukio haya mbona kilasiku yanatokea kanisani tu? Wenye dini yenu ichunguzeni vizuri imani yenu hiyo.
 
Dah amakweli dunia yetu inaelekea ukingoni yaani kiongozi wa dini kawa Shetani namna hiyo?
Wala sio eti anashida au amezidiwa lah.. niwazimu tuu,Wake 11 bado unataka tuu alafu eti anataka watoto 100 eti kabla haja hajafa sasa atawapatia huko huko Lupango K****e.
Kiongozi wa dini? Dini gani hiyo?
 
Lakini matukio haya mbona kilasiku yanatokea kanisani tu? Wenye dini yenu ichunguzeni vizuri imani yenu hiyo.

Jinai haina dini na sheria haina dini kule jela wapo mchanganyiko wa madhehebu mbalimbali
Tofati ni kuwa makosa ya kujamiana yamebeba uzito tofauti kulingana na tamaduni tofati kama ilivyo ulaji wa kitimoto.
 
Hiyo ni dini ya wabakaji, mashoga, wasagaji na uchafu wote usiotakiwa na M/Mungu ndiyo umejaa kwenye dini hiyo.
 
Mchangaji kaamua kutafuna kondoo wake.

Hivyo vifaa vya kuchochea ngono vikoje.

Mchungaji ana watoto 30 na wake 11.

CC: Mzito Kabwela, Matola.
 
Last edited by a moderator:
Wengine wanaowa mbwa wengine wanabaka,mapadri wengine wanahalalisha gongo sijui hii dini ya style gani,
Ukishaona dini kitabu chake kina editions kama vitabu vya akina Mankew au Todaro jua hapo hakuna kitu. Kuna genge la kupiga deal tu ya kufanya "maujuzi" ya kuwaibia watu.
 
Status
Not open for further replies.
Back
Top Bottom