Mchumi Zitto, mbona umesahau kuwambia hili wananchi kuhusu mabenki na makampuni ya simu?

Leak

JF-Expert Member
Feb 22, 2012
52,846
43,322
Wasalaa wanajamvi!

Wanajamvi, katika jambo lililozuwa mjadala leo baada ya bajeti kuu kusoma ni kuhusu serikali kupata gawio kwenye makato ya huduma zinazotolewa na benki na makampuni ya simu!
Mfano tumezoea unaweza kukatwa 1000 ukituma 5000 sasa kwenye 1000 serikali itapata gawio la 10%!

Mh Zitto umesahau kuwaambia wananchi kuwa makampuni ya simu hupata Tsh ngapi kwenye kila 1000? Mh Zitto, statement uliyotoa iliegemea upande mmoja kabisa as if serikali imeanzisha kitu kipya au inaanza kukamua wananchi!

Wanajamvi, kila mtu anajua kwamba kila unapouliza salio si bank au kwenye makampuni ya simu lazima ukatwe pesa. Je, serikali hupata gawio?

Kila unapotuma pesa kuna pesa unayokatwa, je serikali hupata gawio?

Kabla hutujazua mjadala wa TRA kupata 280 kwenye 1000, je mabenki yanapata na hupata Tsh ngapi?

Mh Zitto amekuwa mstari wa mbele kusema makampuni ya simu kuwa hayalipi kodi stahiki kila leo.Nilitegemea Mh Zitto ungewaambia watu kama Serikali imekuwa ikipata gawio au lah kwenye makato ya huduma wanazotozwa wananchi!

Wanajamvi, hivi ni haki makampuni ya simu na mabenki kupata gawio kwenye makato ya huduma wanazotupatia? Na si haki kwa serikali serikali kupata gawio kwa makato wanayoyafanya kwenye huduma wanazotoa?

Hivi serikali haina haki kupata 10% kwenye makato wanayofanya watoa huduma hawa?

Tunajua wanaweza kupandisha gharama lakini serikali haina haki kupata gawio kwenye makato wanayofanya?

Mh Zitto, naomba uwambie wananchi ni kiasi gani makampuni ya simu na mabenki wamekuwa yakipata na ni kiasi gani yatapata? Au wao hawana wanachopata? Kwanini serikali haina haki kupata gawio kwenye hayo makato?

Karibuni wana jamvi!
 
Mkuu hapa ishu fafanua hiyo 10% itakatwa kwa mtindo gani basi, hizo zingine siasa tu.!
 
Kama umesoma hapo juu utajua hiyo 10 ina katwa wapi mfano wewe ukikatwa 1000 kwenye buku serikali inapata 10% !
 
Porojo nyingi sana,
Unajaza server tu, ungeeleza kwa mistari miwili hiyo 10% inakatwa kwa utaratibu upi ingetosha.
 
UFAFANUZI!

Watu wengi wamestuka sana kusikia kuwa kuanzia tarehe 01 Julai 2016, kila utakapotoa fedha kwenye ATM au huduma za fedha kwa mitandao ya simu, TRA itachukua asilimia 10 ya pesa hizo.

Ukweli ni kuwa kodi hiyo ya 10% kwenye muamala wa simu au kutoa pesa kwenye ATM itakatwa kwenye gharama ya kutolea au kutumia na wala siyo kwenye pesa zako.

Mwanamtandao Gabriel Mwang'onda amefafanua kuwa 'kwa mfano ukitoa sh milioni moja gharama ya kutolea ni sh 7500, basi serikali wanakata 10% kutoka katika hiyo sh 7500 (sh 750) na siyo kwenye sh milioni moja'.

Ngoja tuwafafanulie hapa ili watu wasije kukimbia na mabegi kutoa hela zao kwenye mabenki.

Hata hivyo, uamuzi huu wa serikali unaweza kupelekea Benki na makampuni ya simu vipandishe gharama za kufanya miamala ya fedha na hivyo mzigo wa mwisho kuwekwa mabegani mwa mlaji (mlalahoi, mteja au mpokea huduma).

Rai yangu kwa serikali ni kuongea na Benki Kuu (BoT) na vyombo vingine vinavyodhibiti masuala ya kifedha ili zipangwe gharama kikomo za ufanyaji miamala na kwamba benki au kampuni isitoze zaidi ya ukomo uliopangwa. Hilo lisipofanywa tutapokea tatizo kubwa na jipya na watu wataondoa pesa zao kwenye mabenki n.k.

Tusipoziba ufa, tutajenga.....
 
Ninawasiwasi na wewe ni another type ya Jessica
Hivi unataka nini zaidi wakati nimesha kwambia kuwa kuwa serikali inapata 10% kwenye kila pesa ya makato wanayo kata makampuni! Mfano kama wakikata 1000 serikali inapat 10% ya 100! Unataka nini tena?
 
Wasalaa wanajamvi!

Wanajamvi, katika jambo lililozuwa mjadala leo baada ya bajeti kuu kusoma ni kuhusu serikali kupata gawio kwenye makato ya huduma zinazotolewa na benki na makampuni ya simu!

Mh Zitto umesahau kuwaambia wananchi kuwa makampuni ya simu hupata Tsh ngapi kwenye kila 1000? Mh Zitto, statement uliyotoa iliegemea upande mmoja kabisa as if serikali imeanzisha kitu kipya au inaanza kukamua wananchi!

Wanajamvi, kila mtu anajua kwamba kila unapouliza salio si bank au kwenye makampuni ya simu lazima ukatwe pesa. Je, serikali hupata gawio?

Kila unapotuma pesa kuna pesa unayokatwa, je serikali hupata gawio?

Kabla hutujazua mjadala wa TRA kupata 280 kwenye 1000, je mabenki yanapata na hupata Tsh ngapi?

Mh Zitto amekuwa mstari wa mbele kusema makampuni ya simu kuwa hayalipi kodi stahiki kila leo.Nilitegemea Mh Zitto ungewaambia watu kama Serikali imekuwa ikipata gawio au lah kwenye makato ya huduma wanazotozwa wananchi!

Wanajamvi, hivi ni haki makampuni ya simu na mabenki kupata gawio kwenye makato ya huduma wanazotupatia? Na si haki kwa serikali serikali kupata gawio kwa makato wanayoyafanya kwenye huduma wanazotoa?

Hivi serikali haina haki kupata 10% kwenye makato wanayofanya watoa huduma hawa?

Tunajua wanaweza kupandisha gharama lakini serikali haina haki kupata gawio kwenye makato wanayofanya?

Mh Zitto, naomba uwambie wananchi ni kiasi gani makampuni ya simu na mabenki wamekuwa yakipata na ni kiasi gani yatapata? Au wao hawana wanachopata? Kwanini serikali haina haki kupata gawio kwenye hayo makato?

Karibuni wana jamvi!

Wewe haikuumi maana buku 7 unayopokea haikatwi kodi unapokea kwenye bahasha
 
UFAFANUZI!

Watu wengi wamestuka sana kusikia kuwa kuanzia tarehe 01 Julai 2016, kila utakapotoa fedha kwenye ATM au huduma za fedha kwa mitandao ya simu, TRA itachukua asilimia 10 ya pesa hizo.

Ukweli ni kuwa kodi hiyo ya 10% kwenye muamala wa simu au kutoa pesa kwenye ATM itakatwa kwenye gharama ya kutolea au kutumia na wala siyo kwenye pesa zako.

Mwanamtandao Gabriel Mwang'onda amefafanua kuwa 'kwa mfano ukitoa sh milioni moja gharama ya kutolea ni sh 7500, basi serikali wanakata 10% kutoka katika hiyo sh 7500 (sh 750) na siyo kwenye sh milioni moja'.

Ngoja tuwafafanulie hapa ili watu wasije kukimbia na mabegi kutoa hela zao kwenye mabenki.

Hata hivyo, uamuzi huu wa serikali unaweza kupelekea Benki na makampuni ya simu vipandishe gharama za kufanya miamala ya fedha na hivyo mzigo wa mwisho kuwekwa mabegani mwa mlaji (mlalahoi, mteja au mpokea huduma).

Rai yangu kwa serikali ni kuongea na Benki Kuu (BoT) na vyombo vingine vinavyodhibiti masuala ya kifedha ili zipangwe gharama kikomo za ufanyaji miamala na kwamba benki au kampuni isitoze zaidi ya ukomo uliopangwa. Hilo lisipofanywa tutapokea tatizo kubwa na jipya na watu wataondoa pesa zao kwenye mabenki n.k.

Tusipoziba ufa, tutajenga.....

Hivi huoni kama kuna double taxation kwenye haya makampuni?

Mfano. Hayo makato ni moja ya chanzo cha mapato ya kampuni za simu. Na hayo makampuni yanalipa kodi kutokana na mapato yao ya jumla ikiwa ni pamoja na hayo makato.
Sasa kulipa 10% na hapo hapo waje kulipa kodi nyingine ni sawa na double taxation.
 
Hivi unataka nini zaidi wakati nimesha kwambia kuwa kuwa serikali inapata 10% kwenye kila pesa ya makato wanayo kata makampuni! Mfano kama wakikata 1000 serikali inapat 10% ya 100! Unataka nini tena?

Na mawakala wanapata nini baada ya hiyo 10%?
 
Hivi huoni kama kuna double taxation kwenye haya makampuni?

Mfano. Hayo makato ni moja ya chanzo cha mapato ya kampuni za simu. Na hayo makampuni yanalipa kodi kutokana na mapato yao ya jumla ikiwa ni pamoja na hayo makato.
Sasa kulipa 10% na hapo hapo waje kulipa kodi nyingine ni sawa na double taxation.
Hebu twambie huwa wanalipa kodi kwa kila huduma wanayo toa? Hasa makampuni ya simu? Serikali haina haki ya kupata gawio kwenye makato wafanyayo?
 
Hivi unataka nini zaidi wakati nimesha kwambia kuwa kuwa serikali inapata 10% kwenye kila pesa ya makato wanayo kata makampuni! Mfano kama wakikata 1000 serikali inapat 10% ya 100! Unataka nini tena?
Jibu swali la MSSA ALAIN
 
Kodi ya mishahara
Katika kodi inayokatwa katika mishahara (P.A.Y.E), imepunguzwa kutoka asilimia 11 mpaka tisa kwa wafanyakazi wanaopata mshahara wa kuanzia Sh 170,000 lakini hauzidi 360,000. Kwa wanaopata zaidi ya 360,000 lakini haizidi 540,000, watakatwa Sh 17,100 pamoja na asilimia 20 ya kiasi kinachozidi Sh 360,000.

Kabla ya hapo walikuwa wakikatwa Sh 20,900 na asilimia 20 ya kiasi kinachozidi Sh 360,000.

Wanaopata zaidi ya Sh 540,000 lakini haizidi Sh 720,000, watakatwa Sh 53,100 pamoja na asilimia 25 ya kiasi kinachozidi 540,000.

Kabla ya hapo, walikuwa wakikatwa Sh 56,900 na hiyo asilimia 25 ya kiasi kilichozidi 540,000. Kwa wanaopata zaidi ya Sh 720,000 wao watakatwa Sh 98,100 pamoja na asilimia 30 ya kiasi kinachozidi Sh 720,000.

Kabla ya hapo, walikuwa wakikatwa Sh 101,900 pamoja na asilimia 30 ya kiasi kilichozidi Sh 720,000.
 
Mh Zitto, naomba uwambie wananchi ni kiasi gani makampuni ya simu na mabenki wamekuwa yakipata na ni kiasi gani yatapata? Au wao hawana wanachopata? Kwanini serikali haina haki kupata gawio kwenye hayo makato?
Mhe. ZZK kasaheleza yake na kwa utafiti wake na wewe mkuu kwa nini usifanye tafiti ukaja na wanachopata na mchanganuo wako?Yaani kila kitu unataka utafuniwe?Huu muda wa kuandika haya yote kwa upana ungejikita katika kujua mabenki yanapata Tshs ngapi n then ungemchallenge Mhe. ZZK
 
Hebu jiulize mawakala wamekuwa wakipata sh ngapi kabla ya 10%? Na je serikali haina haki ya kupata gawio?
Mkuu wewe ndio mada yako hii ulipaswa kueleza hayo yote ulikuwa na haraka gani ya kuandika haya?ZZK anasoma kabla ya kuandika bro na wewe jitahidi kusoma au ndio bajeti ya chereko chereko?
 
Back
Top Bottom