Mchumi: TRA haiwezi kukusanya kodi ya Majengo

SeriaJr TW

JF-Expert Member
Oct 21, 2012
246
224
56b15694a6db2f749625f5b3402fe3bd.jpg

Mchumi na mtafiti wa uchumi amesema uamuzi wa Serikali kuipa Mamlaka ya Kodi (TRA) kazi ya kukusanya kodi ya majengo badala ya halmashauri za wilaya, utapunguza mapato hayo kutokana na upungufu wa rasilimali watu.

Akitoa maoni yake kuhusu bajeti ya mwaka 2016/17 iliyowasilishwa bungeni juzi, mchumi huyo, Simon Mapolu alisema TRA haitamudu kukusanya mapato hayo kwa ufanisi kutokana na kuhitaji mtandao mpana wa watumishi kuweza kufanya kazi zilizokuwa zikifanywa na halmashauri za wilaya, manispaa na majiji.

“Halmashauri za wilaya zina watumishi hadi ngazi ya mtaa kwa maana ya wenyeviti na watendaji wa mitaa au vijiji ambao wanatumika kufuatilia na kukusanya ushuru wa majengo, wakati TRA watumishi wao huishia ngazi ya wilaya na maeneo machache kwenye vituo maalumu,” alisema Mapolu.

“Wakati Sheria ya Kodi ya Mwaka 2004 inawafanya TRA kuwasubiria walipakodi wawafuate ofisini, mamlaka za halmashauri huwafuata walipa kodi ya majengo hukohuko waliko.”

Kuhusu ongezeko la kodi kwenye vinywaji baridi na vikali, mchumi huyo alisema ni kasumba inayolemaza wataalamu wa uchumi wa Serikali kufikiria kuongeza kodi kwenye bidhaa hizo kila mwaka badala ya kubuni vyanzo vipya.

“Kwa mfano, kiwango cha kodi kilichoongezwa kwenye vileo na vinywaji baridi kingekusanywa maradufu iwapo nguvu zaidi zingeelekezwa kwenye huduma za simu, kama miamala ya fedha kwa njia ya mtandao,” alisema Mapolu.

Alisema ukiacha miamala ya fedha, makampuni ya simu pia yanaingiza mamilioni ya fedha kupitia gharama za miito ya simu na runinga kwa njia ya mtandao ambayo haijakatwa kodi kwa kiwango kinachostahili.

“Kuna zaidi ya Watanzania 30 milioni wenye kumiliki namba za simu, hawa wakiweka muda wa maongezi ya Sh1, 000 kwa siku, makampuni hayo huingiza zaidi ya Sh3 bilioni kwa siku bila kutozwa kodi stahiki,” alisema Mapolu

Kuhusu Sh50 milioni zilizotengwa kwa kila kijiji kwa ajili ya mikopo kwa wanawake na vijana, mtaalamu huyo alisema ni lengo jema, lakini akaonya kuwa haiwezi kuleta tija iwapo hakutakuwa na mkakati thabiti na unaoeleweka.

Alisema fedha zilizotolewa na Rais wa Serikali ya Awamu ya Nne, Jakaya Kikwete na kubatizwa jina la “Mamilioni ya JK”, zilipotea kutokana na kutokuwepo na mfumo wa kuzifuatilia.

Mchumi: TRA haiwezi Kukusanya Kodi ya Majengo | MPEKUZI
 
Now here we go again. Kulipa kodi inabidi liwe swala la utashi. Kwa nini tulipe kodi kwa kulazimishana? TRA et al.......waweke mazingira ya kila mtu kulipa kodi ya jengo bila kushurutishwa. Ni swala la ubunifu tuu.
 
Kitendo cha kuandika hivi tu inaonyesha kabisa hauko tayari kulipa kwa hiyo nguvu lazima itumike
 
Ukitaka kuwabana wenye Nyumba wa mjini....hii kodi ijumuishe kwenye bili ya umeme,hawakuchengi,yaani kila mwezi akilipa umeme anakuta ka elfu mbili kanatakiwa ka property tax.....ishu ni kuzichanganya hizo mbili umeme na kodi ya jengo,but cha msingi lengo linafikiwa.....hiyo inaitwa mbuzi afe mzigo ufike....ila pia wanaweza kuwepo kundi la pili la wenye hati,magorofa,prime areas,hawa watakuwa na special rates kutegemeana na jengo lake na matumizi,tanesco wana mtandao mkubwa wa ku-bill kuliko taasisi yeyote ya umma ,may be na makampuni ya simu
 
Wapo watu au ofisi wanaotumia umeme bila kuwa na nyumba kama kukodisha frem ya duka, kukodisha chumba kwa ajili ya ofisi, wanaotumia umeme kwenye mabango ya matangazo nk. TRA itawatambuaje hawa? Kumbuka sheria ni kukusanya kodi ya majengo na siyo vinginevyo.
 
Now here we go again. Kulipa kodi inabidi liwe swala la utashi. Kwa nini tulipe kodi kwa kulazimishana? TRA et al.......waweke mazingira ya kila mtu kulipa kodi ya jengo bila kushurutishwa. Ni swala la ubunifu tuu.
Toka lini waTZ wote walilipa kodi bila shuruti. Kodi inatakiwa sasa na ni lazima ikusanywe sasa, hakuna muda wa kuweka mazingira mazuri wakati tunahitaji kodi sasa. Lazima kwa sasa watu wapelekeshwe wakati wataalamu wakiendelea kujipanga kuweka haya mazingira ya kulipa kodi bila kulazimishwa.
 
Wewe unalipa kodi......naona unasema "watu" huku unajitoa wewe kama vile unalipaga kodi
 
Ukitaka kuwabana wenye Nyumba wa mjini....hii kodi ijumuishe kwenye bili ya umeme,hawakuchengi,yaani kila mwezi akilipa umeme anakuta ka elfu mbili kanatakiwa ka property tax.....ishu ni kuzichanganya hizo mbili umeme na kodi ya jengo,but cha msingi lengo linafikiwa.....hiyo inaitwa mbuzi afe mzigo ufike....ila pia wanaweza kuwepo kundi la pili la wenye hati,magorofa,prime areas,hawa watakuwa na special rates kutegemeana na jengo lake na matumizi,tanesco wana mtandao mkubwa wa ku-bill kuliko taasisi yeyote ya umma ,may be na makampuni ya simu

Hapo umeweka assumption kuwa kila nyumba ina umeme....tuambie utakusanya vipi kwenye nyumba zisizo na umeme?
 
Mi naona mifumo hii imelemaa lakini kuna uwezekano wa kulipa kodi kwa kuzingatia mazingira halisi mfn maduka madogomadogo ya rejareja yangekua yanalipa ushuru kwa serikali za mitaa kila cku labda 500 au 1000 wangekua wanakusanya kwa mwaka hela nyingi sana ila TRA wanasubiri wapelekewe laki 2 kwa mwaka na biashara zetu za kuganga njaa lini nitskusanya nishike keshi mkononi duka hilo hilo lilipie chuo st joseph chuo hicho kifungwe na serikali bila kujali km nilipeleka pesa pale kimsingi ni mfumo uliolemaa shida sio wananchi!!
 
shida ya viongozi walio kwenye nafasi wanaogopa kuandaa mpango mkakati ulio bora wakukusanya mapato
 
Ni kujipanga tu....kila kitu kinawezekana.
Hizi kodi inaonyesha zilikuwa zinawanufaisha watu wengi sana,ukiona jiwe limerushwa kwenye giza na kuna mtu katoa ukulele ujue limempata.Anyway tuwe wavumilivu tutazowea tu,kila mtu ale kile anachokistahili.
 
Ukitaka kuwabana wenye Nyumba wa mjini....hii kodi ijumuishe kwenye bili ya umeme,hawakuchengi,yaani kila mwezi akilipa umeme anakuta ka elfu mbili kanatakiwa ka property tax.....ishu ni kuzichanganya hizo mbili umeme na kodi ya jengo,but cha msingi lengo linafikiwa.....hiyo inaitwa mbuzi afe mzigo ufike....ila pia wanaweza kuwepo kundi la pili la wenye hati,magorofa,prime areas,hawa watakuwa na special rates kutegemeana na jengo lake na matumizi,tanesco wana mtandao mkubwa wa ku-bill kuliko taasisi yeyote ya umma ,may be na makampuni ya simu
mkuu mimi ndo sijakuelewa au?, naona inaweza kuhamishia kodi hiyo kwa wapangaji badala ya mmiliki wa jengo lenye umeme.
 
Back
Top Bottom