mchumba wangu na demu wake wa zamani

mchumba wangu na demu wake wa zamani

Chamno nijinsi alivyomsave kwenye simu zake, moja kaandika jina kamili, kwingine anakojua nitaiona kwa urahisi kamsave mgosi moro, duh!!

mmmh! Hii nayo kali! Haya mama we subiri ukae uke wenza hao hawajaachana bado
 
Kwa nini usisubiri uolewe kwanza?
ili uwe na haki ya kulalamika?
so far now wote ni wachumba,mna haki sawa
labda hajafanya uamuzi a settle na yupi..
umemshauri vizuri beyond normal! hajui kama jamaa anaweza kubadili mawazo na kumuoa wa zamani? jamaa ni kiboko maana hataki kumpoteza wa zamani na hii inaonesha kuwa huenda hata huyu mupya hajamuingiza katika fikra zake moja kwa moja!
 
anaponiacha hoi ni pale nilipomwambia ampigie aongee nae nikisikia akagoma.
U deserve better than that,mwache tuu koz inaonekana yuko upande wa huyo mwengine na si wako
 
Pole sana dada.
Hiyo hali unayoiona sasa kwa huyo mchumba wako ni taarifa tosha kua hapo mko wengi au mtakua wengi. Sasa Mungu kesha kuonyesha kua unataka kuolewa na mume wa namna gani. Hapo akili kichwani kwako wanasema mapenzi hayana macho kama umempenda kiasi cha kushindwa kuona basi vumilia tu. Kumbuka kuna madhara makubwa sana mmoja wenu anapokua sio mwaminifu , ujue kua huyo mpenzi wake wa mwazo yeye bado anampenda na sijui kama ataweza kumuachilia.
 
Mh!mpenda ni sawa na kipofu yaani hata hapo uoni kuwa akupendi?
 
Hello wana Jr, nisaidieni kwa hili, naumia sana bado mchumba wangu ana mawasiliano na mwanamke wake wa wazamani,

nili

mpigia sim yule dada na kumhoji kijifanya sio mimi mlengwa ila mlengwa analalamika, dada yule akasema kwani yeye hana hiana aoe yeye atakuwa wa pembeni. kwanza mie matumizi napata ninashida gani? na kweli nilikamata msg za mpesa.

na bado anaendelea kuwasiliana, huyu mchumba anasema ati atamuacha taratibu, kwe
li hapo nifanyeje?
yan wanaume wote ndo wako hivyohvyo,tena ukikuta ana wawili tu ushangae
lakin mahusiano yao ya zaman hayavunjikagi
mimi mtu wa hivyo naomba laana juu yake
maana unajikuta wewe mwaminifu halafu yeye kiruka njia
sorry guys for saying ths..
 
Kama hawezi kuheshimu uchumba wenu unadhani ataiheshimu ndoa? Tafakari. majuto ni mjukuu.
 
kama unamwamini Mungu, fanya maombi ujue lipi lililo jema, otherwise utarudi tena hapa kulialia kama mtoto, hatutaki
 
Olewa mwaya hakuna mume wako peke yako. Kama unampenda mchumba wako olewa na mtaishi tu. kwani akiwa na huyu wapembeni shida inakupata wapi? Maisha ndio hayohayo ndugu yangu sinema ileile tu tofauti screen tu. Shaurilo

Sent from Samsung tablet
 
hahaha... hakuna kitu kama "ntamuacha taratibu", yani unaota kwelikweli... Ngoja uamke pameshakucha...
 
Hello wana Jr, nisaidieni kwa hili, naumia sana bado mchumba wangu ana mawasiliano na mwanamke wake wa wazamani,

nilimpigia sim yule dada na kumhoji kijifanya sio mimi mlengwa ila mlengwa analalamika, dada yule akasema kwani yeye hana hiana aoe yeye atakuwa wa pembeni. kwanza mie matumizi napata ninashida gani? na kweli nilikamata msg za mpesa.

na bado anaendelea kuwasiliana, huyu mchumba anasema ati atamuacha taratibu, kweli hapo nifanyeje?

Pole..
Hii inaitwa wait just a little longer...
Avant - Lie About Us ft. Nicole Scherzinger - YouTube
 
Fanya hivi, mvumilie tu, ila kuwa na akili kichwani mwako mama, na ww ukipata mwanaume mwenye mwelekeo, sepa, tena kata mawasiliano kabisaa kimya kimya hiyo no kugombana wala nn hata akikupigia simu no kupokea wala kujib msg zake. kukaa kimya kwako n jibu tosha kwake.
 
Hello wana Jr, nisaidieni kwa hili, naumia sana bado mchumba wangu ana mawasiliano na mwanamke wake wa wazamani,

nilimpigia sim yule dada na kumhoji kijifanya sio mimi mlengwa ila mlengwa analalamika, dada yule akasema kwani yeye hana hiana aoe yeye atakuwa wa pembeni. kwanza mie matumizi napata ninashida gani? na kweli nilikamata msg za mpesa.

na bado anaendelea kuwasiliana, huyu mchumba anasema ati atamuacha taratibu, kweli hapo nifanyeje?

Achana naye, ama vinginevyo ukubali kuwa mtu wa kuumia rohoni kwa muda wote wa maisha yako yaliyobakia hapa duniani. Huyo dada keshakuthibitishia kuwa huyo mchumba wako anaweza kuoa lakini yeye atakuwa wa pembeni. Unataka uthibitisho gani zaidi. Na huyo mchumba wako anapodiriki kukutamkia wazi kuwa atamwacha taratibu bado hujaelewa tuu? taratibu ndiyo muda gani? muulize je na yeye anakuruhusu wewe kuendelea na uliyekuwa naye hapo awali kabla hujakutana naye na umwambie utamuacha huyo wa awali lakini taratibu. Utakapopata maambukizi ndipo akili yako itafunguka
 
Usidanganyike na poyoyo wa JF hapa wanakuambia achana nae!!! Hakuna mwanaume asie na kimada! Yaani unataka kumwacha mwanaume wako kwa tishio la kimada chake cha zamani Kalagabaho....! Komaa nae, ongeza mapenzi kwake, usilete jeuri kabisa maana ndio utampa ticket
Wanaume tunapotoka nje bwana sio kwamba eti huku nitaenda jumla, najua kiota changu..... ninapas time tu Najua nyumbani ni nyumbani..........

Tena nikirudi nyumbani narudi na adabu zote....... napakatwa nanyweshwa juice Nani Kama mke bwana.....!
 
Hello wana Jr, nisaidieni kwa hili, naumia sana bado mchumba wangu ana mawasiliano na mwanamke wake wa wazamani,

nilimpigia sim yule dada na kumhoji kijifanya sio mimi mlengwa ila mlengwa analalamika, dada yule akasema kwani yeye hana hiana aoe yeye atakuwa wa pembeni. kwanza mie matumizi napata ninashida gani? na kweli nilikamata msg za mpesa.

na bado anaendelea kuwasiliana, huyu mchumba anasema ati atamuacha taratibu, kweli hapo nifanyeje?

Dada hapo huna mchumba/mume kama kweli anakupenda kwa dhati hawezi kukuambia kuwa atamuacha taratibu hata kidogo, badala yake wewe unaweza kuachwa taratibu.

Fikiria mara mbili juu ya mahusiano yenu hayo na uchukue uamuzi sahihi juu ya maisha yako.
 
Back
Top Bottom