Mchumba wangu mchawi

Mchumba wangu mchawi

Tetra

JF-Expert Member
Joined
Oct 5, 2012
Posts
1,526
Reaction score
771
Ndg wana Jf najitokeza leo,naombeni ushauri wenu,nimepata mchumba ambaye ni mzuri,mpole na tunaependana sana.LAKINI tatizo nina taarifa kutoka kwa wazee,kuwa kwao ni wachawi.NAOMBENI ushauri wenu,,najaribu kumwacha nashindwa maana nampenda,,nisaidieni
 
ndege wanaofanana huruka pamoja
hata hao wazee wako ni wachawi ndo maana wakajua na wa mwenzio wachawi
usikubali
 
sasa kama kwao wachawi ,yeye inamhusu vipi?

mbona wapo watu kwao walokole na wao ni micharuko?
 
Hapo na wewe jifunze uchawi ili muende sawa!
 
Ndg wana Jf najitokeza leo,naombeni ushauri wenu,nimepata mchumba ambaye ni mzuri,mpole na tunaependana sana.LAKINI tatizo nina taarifa kutoka kwa wazee,kuwa kwao ni wachawi.NAOMBENI ushauri wenu,,najaribu kumwacha nashindwa maana nampenda,,nisaidieni

Pole sana...Muache halafu uende kuoa mlokole mcharuko halafu ujute. Kama kwao wachawi unaogopa nini sasa...Komaa tu acha uoga ndugu.....Ukiona vipi jiunge nao.
 
LIMBWATA Lilishakukoleaaaa! Umewekwa kwenye chua, umeenea na umetuliaaa! Hutikisiki, imebakia kupulizwa kila asubuhi na jioni!
 
Kama umesikia kuwa kwao na huyo mwanamke ni wachawi basi wewe kuwa karibu na Mungu wako na utaona nguvu yao yote inakwisha na maisha yako na ya umpendae yatakuwa sawa,usiamini sana katika uchawi kwani ukimtegemea Mungu hakuna nguvu itakayomshinda.
 
mkuu lara 1 thanx kwa kicheko hyo post umemaliza bhaaaaassss
 
Last edited by a moderator:
Wazee wako ni walokole?

Walionipa taarifa ni wazee ambao wanaijua familia yao yaani watu wa pembeni ya huo ukoo na si wazee wa upande wangu.KUHUSU ulokole,wazee wangu msimamo wa dini ni wa wastani
 
1. umesikia hujahakikisha
2. kwao ni wachawi, sio YEYE NI MCHAWI
THERE IS NO POINT 4 U TO STOP LOVING THE GIRL :behindsofa::behindsofa::behindsofa:
 
Wewe hadi sasa una maamuzi gani?
Japo ujapata ushahidi hila umeambiwa tu!

Walionipa taarifa ni wazee ambao wanaijua familia yao yaani watu wa pembeni ya huo ukoo na si wazee wa upande wangu.KUHUSU ulokole,wazee wangu msimamo wa dini ni wa wastani
 
Keep on touch... Mapenzi ya kweli yana nguvu kushinda chochote duniani, afterall umesema kwao ndiyo wachawi...(siyo yeye)! Then jitahidi kumpenda Mungu!
 
Similar Discussions

Back
Top Bottom