Mchumba wangu kanisaliti!! Niko kwenye maumivu makali naombeni ushauri

Mtoto halali na hela

Mtoto halali na hela

JF-Expert Member
Joined
Aug 10, 2012
Messages
23,711
Likes
6,976
Points
280
Mtoto halali na hela

Mtoto halali na hela

JF-Expert Member
Joined Aug 10, 2012
23,711 6,976 280
Kubaliana na hali ndio ishatokea na hakuna cha kubadilisha ukweli uliokutana nao, Jifunze kutoumia tena itakusaidia mahusiano yajayo.
 
impongo

impongo

JF-Expert Member
Joined
Feb 18, 2015
Messages
5,648
Likes
3,552
Points
280
Age
33
impongo

impongo

JF-Expert Member
Joined Feb 18, 2015
5,648 3,552 280
Wakubwa zangu shikamooni, vijana wenzangu habari vipi?
Ndugu zangu, nipo serious sanaa katika ombi langu, nakuomba unipe muda wa kunisikiliza kidogo na unishauri kama inafaa.
Mimi ni kijana nina umri wa miaka 29, ni mwajiliwa serikalini idara ya Afya. Kuna binti nilianza nae uchumba 2017 mwanzoni yeye akiwa chuo flan cha afya, Mimi ni Mgogo yeye ni Mbulu ana miaka 24 sasa.
Tulianza mapenzi akiwa ameonesha msimamo wa kutoshiriki tendo lolote na mimi mpaka mwaka mmoja ulipopita ndo tukaanza kukutana kimwili. Ni binti ambae niliona huyu anafaa kuwa mke wangu kabisaa maana alikua ana msimamo sanaa hata kwa watu wengi waliokua wakimtongoza maana alikua ananionesha sms na calls zao, bas nikawa namshauri wajibu wewe ni mke wa mtu na unahitaji heshima, kiukweli nilijipa moyo hapa nimepata mke kweli kweli. Basi akamaliza chuo 2017 mwishoni nikamtaftia ajira ya kujishikiza mahali flani mkoa wa Mwanza. Sasa nikawa nimeongea na mtu mmoja awe anafatilia nyendo zake wakati mimi nipo mbali. Alipotimiza miezi miwili kazini nikapata taarifa kuna kabwana mdogo ka umri wa miaka 22 - 24 kanatembea nae hapo hapo alipopanga chumba, sikutaka kuamini, ikanibidi siku moja nifanye kusadiri kwenda kumtembelea kimya kimya bila taarifa, nikafika akanipokea vizuri. Ilipofika usiku nikamwambia sasa mpenzi unaweza kunihakikishia huku huna mchezo wowote mchafu wa kimahusiano? Akanijibu hapana kabisa mpenzi wangu naomba uniamini. Nikamuuliza, Je, unaweza kunipa simu yako nikague chochote? Akapata kigugumizi sanaaaaa, nikamuuliza Unanipenda na unajiamini? Akajibu ndio, nikamwambia bas naomba simu yako, akapata kigugumizi kizito sanaaa. Basi ikanibidi nichukue simu yake nipitie sms na whatsap, aseee niliyoyakuta ni mazito mnooooooo wallahi Nimepata simanzi kubwa sanaaa, ikanibidi niondoke usiku huo huo kwenda kutafta Lodge nikalala na kesho nikaondoka kurudi kazini. Mchumba wangu huyu nilikua nimeshafahamiana na ndugu zake baadhi na mama yake mzazi alikua ananijua kwa picha tu na alikua tayari karidhia niww mkwe wake kabla hata sijaenda kujitambulisha maana matendo niliyomfanyia mwane ni mwanaume mwenye malengo mazuri wazi wazi. Kinachoniuma zaidi ni kwamba nimetumia muda mwingi sanaaa kumjenga kiimani, kumjenga juu ya tabia za wanaume wenye tamaa, kiukweli niliamini huyu mwanamke sasa hakuna atakae weza kumshawishi maana hata mimi binafsi nilikua nimebadilika sanaaa kitabia sikuwa nnahamu na michepuko tena niliona sasa huu ni muda wa kutulia na mwanamke mmoja sina haja ya kutanga tanga na dunia ya leo. Ndugu zangu niko serious sanaaa, naombeni ushauri cha kufanya, mwanamke huyu alikua anatembea na kijana wa mwenye nyumba tena kwa kulala nae chumbani kwake karibu kila wiki. Mwanamke alionesha sanaaa kunipenda tulikua tunawasiliana kila siku zaidi ya mara 5 kila siku ya Mungu. Leo naona dunia imenigeuka, nina maumivu makali sanaaaa, niliplan nije kumtambulisha kwetu mwaka huu December, na kwao ningeenda kujitambulisha November ili mwakani Mungu akijaalia tufunge Ndoa. Wakuu, niko gizani, nina msongo wa mawazo, mimi ni jasiri sanaaa lakini nakuomba wewe ndugu yangu ushauri wako katika hili, nakuomba usinitukane wala kunikejeli maana utaniongezea majonzi makubwa.
Naamini thread yangu hii itawafunza na wengine watakao kumbwa na mkasa kama wangu.
ASANTE kwa Muda wako

Sent using Jamii Forums mobile app
Sasa wewe unapenda Mbulu si ulipotea njia hao ni take away

Kunguru hafugiki ulinisumbua bure pole sana

Sent using Jamii Forums mobile app
 
impongo

impongo

JF-Expert Member
Joined
Feb 18, 2015
Messages
5,648
Likes
3,552
Points
280
Age
33
impongo

impongo

JF-Expert Member
Joined Feb 18, 2015
5,648 3,552 280
cc12

cc12

JF-Expert Member
Joined
Jan 26, 2013
Messages
995
Likes
229
Points
60
cc12

cc12

JF-Expert Member
Joined Jan 26, 2013
995 229 60
duuuh demu anamtaro alafu mmekean ahadi manina na uboya wangu wa chuga uo falamba sijafanyi pole sana mkuu karibu ukubwaniii sasa
 
Internal

Internal

JF-Expert Member
Joined
Feb 23, 2017
Messages
2,598
Likes
2,328
Points
280
Age
49
Internal

Internal

JF-Expert Member
Joined Feb 23, 2017
2,598 2,328 280
Kuamini mwanamke tena Mbulu(huwa ni wazuri sana kwa sura)) ni sawa na kuamini unaweza tembea juu ya maji ukavuka bahari bila kuzama.

Ushauri:
Hauna makubaliano yoyote na Dunia hivyo haiwezi kukugeuka, huyo mchumba wako fanya kama hamjawahi kukutana maana ulivyoondoka usiku huo alimuita dogo wakamalizia usiku wote huku mchumba akisema achana naye tufanye yetu.

Sent using Jamii Forums mobile app
 
G.T.L

G.T.L

JF-Expert Member
Joined
Jul 15, 2012
Messages
313
Likes
175
Points
60
G.T.L

G.T.L

JF-Expert Member
Joined Jul 15, 2012
313 175 60

Asante mkuu wangu

Sent using Jamii Forums mobile app
 
manizzle

manizzle

JF-Expert Member
Joined
Apr 29, 2015
Messages
3,488
Likes
3,840
Points
280
manizzle

manizzle

JF-Expert Member
Joined Apr 29, 2015
3,488 3,840 280
Unamlia yamini mwanamke? Akikuambia ndio anamaanisha hapana. Chochote akifanyacho jibu ni opposite. BTW, huwezi kuwa na mwanamke mmoja kama mama mzazi

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Mchumia Rungu

Mchumia Rungu

JF-Expert Member
Joined
Apr 26, 2013
Messages
1,194
Likes
385
Points
180
Mchumia Rungu

Mchumia Rungu

JF-Expert Member
Joined Apr 26, 2013
1,194 385 180
Sijasoma habari. Lakini kichwa cha habari kinanisukuma niseme "heri uchumba uvunjike kuliko ndoa". Tatizo la siku hizi, mkiwa wachumba mnajihalalishia kuwa mme na mke mpaka mambo ya ndoa. Hapo ndipo panapokupelekea upate maumivu. Maumivu ni stahiki ya ujinga wako.

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Ushimen

Ushimen

JF-Expert Member
Joined
Oct 24, 2012
Messages
19,764
Likes
27,310
Points
280
Ushimen

Ushimen

JF-Expert Member
Joined Oct 24, 2012
19,764 27,310 280
Wakubwa zangu shikamooni, vijana wenzangu habari vipi?
Ndugu zangu, nipo serious sanaa katika ombi langu, nakuomba unipe muda wa kunisikiliza kidogo na unishauri kama inafaa.
Mimi ni kijana nina umri wa miaka 29, ni mwajiliwa serikalini idara ya Afya. Kuna binti nilianza nae uchumba 2017 mwanzoni yeye akiwa chuo flan cha afya, Mimi ni Mgogo yeye ni Mbulu ana miaka 24 sasa.
Tulianza mapenzi akiwa ameonesha msimamo wa kutoshiriki tendo lolote na mimi mpaka mwaka mmoja ulipopita ndo tukaanza kukutana kimwili. Ni binti ambae niliona huyu anafaa kuwa mke wangu kabisaa maana alikua ana msimamo sanaa hata kwa watu wengi waliokua wakimtongoza maana alikua ananionesha sms na calls zao, bas nikawa namshauri wajibu wewe ni mke wa mtu na unahitaji heshima, kiukweli nilijipa moyo hapa nimepata mke kweli kweli. Basi akamaliza chuo 2017 mwishoni nikamtaftia ajira ya kujishikiza mahali flani mkoa wa Mwanza. Sasa nikawa nimeongea na mtu mmoja awe anafatilia nyendo zake wakati mimi nipo mbali. Alipotimiza miezi miwili kazini nikapata taarifa kuna kabwana mdogo ka umri wa miaka 22 - 24 kanatembea nae hapo hapo alipopanga chumba, sikutaka kuamini, ikanibidi siku moja nifanye kusadiri kwenda kumtembelea kimya kimya bila taarifa, nikafika akanipokea vizuri. Ilipofika usiku nikamwambia sasa mpenzi unaweza kunihakikishia huku huna mchezo wowote mchafu wa kimahusiano? Akanijibu hapana kabisa mpenzi wangu naomba uniamini. Nikamuuliza, Je, unaweza kunipa simu yako nikague chochote? Akapata kigugumizi sanaaaaa, nikamuuliza Unanipenda na unajiamini? Akajibu ndio, nikamwambia bas naomba simu yako, akapata kigugumizi kizito sanaaa. Basi ikanibidi nichukue simu yake nipitie sms na whatsap, aseee niliyoyakuta ni mazito mnooooooo wallahi Nimepata simanzi kubwa sanaaa, ikanibidi niondoke usiku huo huo kwenda kutafta Lodge nikalala na kesho nikaondoka kurudi kazini. Mchumba wangu huyu nilikua nimeshafahamiana na ndugu zake baadhi na mama yake mzazi alikua ananijua kwa picha tu na alikua tayari karidhia niww mkwe wake kabla hata sijaenda kujitambulisha maana matendo niliyomfanyia mwane ni mwanaume mwenye malengo mazuri wazi wazi. Kinachoniuma zaidi ni kwamba nimetumia muda mwingi sanaaa kumjenga kiimani, kumjenga juu ya tabia za wanaume wenye tamaa, kiukweli niliamini huyu mwanamke sasa hakuna atakae weza kumshawishi maana hata mimi binafsi nilikua nimebadilika sanaaa kitabia sikuwa nnahamu na michepuko tena niliona sasa huu ni muda wa kutulia na mwanamke mmoja sina haja ya kutanga tanga na dunia ya leo. Ndugu zangu niko serious sanaaa, naombeni ushauri cha kufanya, mwanamke huyu alikua anatembea na kijana wa mwenye nyumba tena kwa kulala nae chumbani kwake karibu kila wiki. Mwanamke alionesha sanaaa kunipenda tulikua tunawasiliana kila siku zaidi ya mara 5 kila siku ya Mungu. Leo naona dunia imenigeuka, nina maumivu makali sanaaaa, niliplan nije kumtambulisha kwetu mwaka huu December, na kwao ningeenda kujitambulisha November ili mwakani Mungu akijaalia tufunge Ndoa. Wakuu, niko gizani, nina msongo wa mawazo, mimi ni jasiri sanaaa lakini nakuomba wewe ndugu yangu ushauri wako katika hili, nakuomba usinitukane wala kunikejeli maana utaniongezea majonzi makubwa.
Naamini thread yangu hii itawafunza na wengine watakao kumbwa na mkasa kama wangu.
ASANTE kwa Muda wako

Sent using Jamii Forums mobile app
INAPO TOKEA UMEACHWA:-

1. Epuka kulipiza kisasi, mwachie Mungu na kubali yote yaliyotokea na kuruhusu yapite.
Unapoachwa ni kama adhabu fulani hivi kwani akilini mwako utajiona kama huna thamani na kuanza kujitoa kasoro kwa kujiuliza maswali kibao mfano sikumridhisha, sina mvuto na mambo mengi utafikiria.
Kipindi hiki unashauriwa kufunga mlango kabisa kwa ex wako tena ikubali hali hiyo ikupite ili ukaribishe maisha mengine ya furaha huku ukimuomba Mungu sana.

2. Epuka kusikiliza nyimbo za huzuni au kubembeleza.
Baada ya kupigwa chini na mpenzi wako, epuka kusikiliza nyimbo za huzuni au mapenzi zenye kubembeleza hizi zitakufanya ufikirie majanga yaliyokukuta badala yake sikiliza nyimbo za kufurahisha zenye kuchezeka na zenye kukufanya ujione wewe ni mshindi muda wote na mwenye furaha.

3. Epuka kuita mahusiano yako ni magumu (Complicated).
Watu wengi hususani wanawake wanapoulizwa na wanaume kuhusu status zao za mahusiano asilimia kubwa majibu yao nina mtu lakini tumezinguana, majibu ambayo huwafanya waumie kisaikolojia hii ni kutokana na kujiona kuwa umri unaenda na bado hawajapata mtu wa kuishi nae.
Hiki kitu huwapata wanawake kwani huwa ni wagumu sana kuruhusu mioyo yao kusahau mapema vitu kutoka kwa ex wako nakumbuka mwaka 2014 Amber Rose alivyomwagana na WizKhalifa alikuwa akilalama kila siku mitandaoni akiamini hiyo itampunguzia machungu kumbe ndiyo kwanza ilimzidishia machungu.

4. Epuka kumsema vibaya ulieachana naye.
Mwenza wako anapoamua kuondoka na kwenda kwa mwingine usiwaambie marafiki zako kuhusu mabaya yake kwani itakufanya uonekane mtu mbaya bila wewe kujua, utaharibu mwonekano wako, na tabia yako, ukisema vibaya kuhusu yeye, pia na wewe utaonekana mkosaji, maana wakosaji ndio huongea mabaya kwa wale ambao hawakufanikiwa.

5. Epuka kutuma meseji za bahati mbaya,au kumfuatilia ex wako kwenye mitandao ya kijamii.
Epuka kutuma meseji za kujitekenya mwenyewe SMS kama oooooh!! samahani, pole, nimekosea. habari yako, sikuwa namaanisha kukutumia wewe. yote ya nini? punguza kuongea nae ikibidi acha hadi akutafute maana kitendo cha kummtafuta utakuwa unaongeza chumvi kwenye jeraha lako mwenyewe.
Kwasasa kutokana na utandawazi ni vyema ukampa tofali (Block) hii itakufanya umtoe kichwani kirahisi kwani kitendo cha kumfuatilia mitandaoni kitakuumiza zaidi hebu fikiria wewe usiku mzima hujalala kutokana na maumivu ya kuachwa halafu asubuhi unaingia tuu Instagram unakutana na picha ya ex wako kaposti picha ya Mwanamke/Mwanaume mzuri halafu kaweka emoji ya vikopa kopa hapo lazima urudi kitandani uendelee kulala.

6. Epuka kujibadilisha mwonekano wako.
Hii inawahusu sana wanawake kwani hao ndiyo wahanga wakubwa kwa hili, Wanawake wengi wakishaachika huanza kujibadilisha muonekano kwa kuamini kuwa muonekano wao wa zamani haukuwa mzuri ndiyo maana waliachika.
Wengi hubadili mavazi,ngozi, Makalio kuweka tatoo nk. kwa lengo la kuwavutia wanaume bila kufikiria madhara yake, mwanamke usidanganyike na chochote kile kufanya hivyo ni kupoteza muda tuu focus kwa kufanya mambo ya maendeleo kama biashara na ujasiriamali kwa maendeleo yako ya baadae.

7. Usikumbuke yaliopita mkiwa pamoja.
Tafuta kitu cha kufanya ili kukuweka bize muda wote, wakati mwingine soma vitabu vya namna ya kufanya ili kupata maendeleo,Angalia tamthilia mbalimbali ,isipokuwa za mapenzi achana nazo. tafuta marafiki wazuri wa kutoka nao na kufurahi pamoja. usikumbuke ya nyuma, jinsi mlikuwa mnafanyaje, labda sasa anafanyaje na mwingine, achana na hayo mawazo.
Hayatakusaidia badala yake utaumia. ukikaa muda wa kutosha fungua akili yako kwa ajili ya mambo mengine yanayostahili maisha yako. lakini ukirudisha mawazo ya nyuma sio tu utaumia bali hata wale wanaokuzunguka watashindwa kukusaidia.

8. Usianzishe mahusiano mengine kwa kukurupuka.
Watu wengi wakiachika kwenye mahusiano basi hukimbilia kutafuta chaka jipya ili kumuonesha ex wake kuwa na yeye anapendwa kumbe hajui hata huyo aliyempata kwa muda mfupi watadumu nae kwa muda mfupi na kujikuta akiachwa kila uchwao.
waswahili wanasema ukiwa na furaha sana usichukue maamuzi na hata ukiwa na hudhuni usifanye hivyo kwani busara hutoe kwa wakati cha kufanya tulia muombe Mungu hayo mengine utafanikiwa tuu.
Natumaini kwa wewe ambaye bado unaugulia maumivu ya kuachwa ukizingatia haya utakuwa umepata mwanga wapi kwa kuanzia na kurudisha furaha na tabasam iliyokuwa imepotea.
 
Nashukuru sana mkuu, nitazingatia maneno yako

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Forum statistics

Threads 1,263,083
Members 485,791
Posts 30,142,024