Mchumba wangu ananitesa jamani

wakora

Member
Joined
Jun 18, 2013
Posts
47
Reaction score
18
Wana JF naombeni msada wenu nifanye nini,

Mchumba wangu niliyempenda sana, ghafla kakata mawasiliano na mimi nikimpigia simu hapokei sms hajibu na hakuna chochote kibaya nilichomfanyia, kibaya zaidi anafahamika kwenye familia yangu, ofisini kwangu mpaka marafiki wote wanajua nilikuwa na mahusiana nae.

Sasa najiuliza ntawambia nini hasa familia make tayari nshamtambulisha nahisi ntaonekana sijatulia hasa kwa wazazi wangu.

Huyu jamaa alifanya nikarisk kazi yangu nikawa naaga naenda kumuona mdogo wangu kumbe naenda Arusha kumuuona yeye by that time alikuwa anafanya masters yake pale Nelson Mandela.

Kwa sasa kamaliza yupo Dar sina mawasiliano nae anachofanya sijui na hata ikitokea nimepiga simu akipokea ananijibu kwa hasira as if tumegombana.

Jamani naumia sana na nilimpenda kwa dhati na yeye analijua lakini sjui ni shetani gani kampata.

Naombeni ushauri wenu jamani.
 
Kumpenda asiyekupenda,utatumia gharama nyingi kutafuta kisichokuwepo.Mshukuru Mungu tulia atatokea mwingine.Si umfuate nyumbani kwao?au ofisini?Au ndio yale mahusiano ya kukutana barabarani,hujawahi kufika kwao?
 
Pole sana kwa yanayokusibu mapenzi yanauma sana jamani. I can feel wat your going through cause it has happened to me too somehow!hapa kuna aidha vitu viwili kimojawapo ni kwamba kuna kila dalili kuwa huyo mchumbaako hakutaki tena yaani anashindwa tu kukwambia na la pili ni kwamba labda yupo busy anahitaji nafasi kwahio mpe muda atajirudi tu!kuwa positive kama unajua hujamkosea chochote hamna ugomvi basi mpe muda..Jaribu Pia kujiuliza kipi kimebadilika kati yenu inawezekana kuna vijitabia au matendo umeanzisha vinamkera ujirekebishe!
 
habari hizi wadogo zangu nawashauri muwe mnazipeleka kwenye yale magazeti yenu ya uduku sijui udaku,
not here,au mnataka na sisi huku JF tuseme
''TUMECHOKA SASA...MKIENDELEA TUTAWAPIGA TU........[BAN]
 
we ni ke au me

Ukisoma vizuri statement moja kwa moja utajua ni Girl kaandika,
Evidences:
See highlighted red:
Wana JF naombeni msada wenu nifanye nini, mchumba wangu niliyempenda sana, ghafla kakata mawasiliano na mimi nikimpigia cm hapokei sms hajibu na hakuna chochote kibaya nilichomfanyia, kibaya zaidi anafahamika kwenye familia yangu, ofcn kwangu mpaka marafiki wote wanajua nilikuwa na mahusiana nae sasa najiuliza ntawambia nini hasa familia make tayari nshamtambulisha nahc ntaonekana cjatulia hasa kwa wazazi wangu, huyu jamaa alifanya nikarisk kazi yangu nikawa naaga naenda kumuona mdogo wangu kumbe naenda arusha kumuuona yeye by that tym alikuwa anafanya masters yake pale nelson mandela kwa sasa kamaliza yupo dar sina mawasiliano nae anachoanya cjui na hata ikitokea nimepiga cm akipokea ananijibu kwa hasira as if tumegombana yani jamani naumia sana na nilimpenda kwa dhati na yeye analijua lkn cjui ni shetani gani kampata,.
Naombeni ushauri wenu jamani,..

Mara nyingi wasichana ndo huwatambulisha haraka marafiki zao wa kiume kwa Familia, marafiki zake wa kike na kutangaza ofsini ili wafanyakazi wenzie wasije vamia mali yake....

Pia wanaume wengi hawaogopi kwamba ataiambia nini familia, ataonekana hajatulia, hii inaapply zaidi kwa wasichana.

Mwanaume hawezi kumwita mchumba wake wa kike "Huyu Jamaa".

Hope umepata majibu hapo; Huyo Dada anasubiria ushauri wako tafadhali.....msaidie!!!
 


Pole mdogo wangu, mwanzoni huwa inauma lakini ukishajiachilia unakuwa huru. Hakuna mapenzi hapo labda kama unataka kudanganywa. Maana huwa tunaambiwa wanawake tunapenda kudanganywa.
Mwenzako yalishanikuta kama yako, nikaumia kama wewe lakini nasonga mbele, maisha lazima yaendelee. Siku moja utampata yule atakayeupooza mtima wa moyo wako. BES STRONG.
 
pole dada inaonekana jamaa ammepata anayemhitaji.....kubali matokeo hunahaja ya kuendelea kumtafuta jipe moyo utamsahahu songa mbele
 
Waswahili wanasema "Dalili ya mvua ni mawingu" hapo huna chako usisubiri kutusiwa na mwanamke mwenzio kwa kuwa king'ang'anizi. Najua inaumiza ila haya ndio makwazo ktk maisha na ndio maana kuna usemi "Ukimwona nyani mzee ujue amekwepa mishale mingi" nawe huna budi kuchukulia hili kama mshale na umeshaukwepa toka nduki(kimbia). cc wakora
 
you only think of other people eti wazazi,marafiki watakufikiriaje,

kuna watu tulipendwa,Pete viganjani tukawekewa,kwa wazazi tulitambulishwa

na bado tukaachwa Solemba.Move on its easier said lakin once you know the

rules of this game u will surely move ON bila hata kuambiwa..........
 
Na wewe jifanye upo busy na mambo yako usimtafute kwa njia yoyote ile hapo ndipo utatambua uwepo wako na mpaka apo kama bado anajifanya kichwa ngumu jua huna chako.
We songa mbele ukija mwingine muadd
 

Similar Discussions

Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…