Ni kijana 29 na kuendelea.
Ni muajiriwa serikalini lakini pia nimejiajiri.
Naomba nilete mkasa wangu wa yaliyonikuta ambayo mpka sasa naumia na nashindwa wapi nianzie.
NILIPITIA HABARI HUMU KUHUSU KUTOOA WANAWAKE WASOMI,
bila kufikira sana niliamua kumuacha mchumba wangu ambae yuko mwaka wa mwisho Chuo, ambae nilimedumu nae toka sina kitu hadi kuajiriwa na yeye alikuwa mstari wa mbele kunishauri mpaka mali nilizonazo naweza sema asilimia kubwa ni mchanganuo wake. Tulipanga Mungu angejaalia mwezi wa tisa tufunge pingu za maisha.
Kiukweli nakiri nilikuwa mtu wa kufatilia sana hiyo mada hata vijiweni na hata ofisini tukiwa tunapiga stori na washkaji mada yangu ilikuwa hiyo sana.
Nakumbuka ilikuwa weekend ambapo mchumba wangu huyo alikuja kunitembelea baada ya mimi kutoka safari ya kikazi Kigoma.
Nilipomuona nilichukia sana maana akili yangu tayari nilikuwa nishaitune kuwa sitaweza kuwa nae sababu yeye msomi.
Jioni ilipofika yeye ndie aliyeniuliza kulikoni nipo hivyo ndipo nilipoanza kumwelezea kuwa sitaweza kuwa nae sababu sitaweza kumuoa kwa kuwa yeye ni msomi.
Kiukweli aliumia sana nakumbuka hakulala kabisa usiku kucha alilia sana.
Asubuhi yake aliwahi sana kuamka, aliniandalia kila kitu cha kuvaa maana nilikuwa naenda kwenye miradi yangu, baada ya chai aliniaga kuwa anaondoka na aliniomba kuwa tusitishe mawasiliano ili impe urahisi wa kuzoea hali ile.
Kiukweli tuliachana kwa amani sana hata familia niliyokuwa naishi nayo haikujua nini kinaendelea kati yetu.
Ikumbukwe kuwa huyu msichana nilimpenda na nitampenda hadi kufa kwangu kwani upendo wake na tabia yake ni wa hali ya juu.
Msichana aliyejielewa sana na alikuwa mvumilivu mno pia alikuwa mshauri wangu sana kwenye biashara zangu hadi nafikia maisha haya.
Muda ulipita kama mwezi sijamtafuta na wala hakunitafuta japo kwa upande wake wapo rafiki zake walinilalamikia sana kwa uamuzi, hasa walilamika jinsi rafiki yao anavoumia, kiukweli sikuwajali niliendelea na yangu.
Nikawa nimepata kibinti fulan hivi nilipokuwa nimeenda likizo basi nikaongea na familia yake na kufuata taratibu zote nikamchukua nikaja nae Dar japo nakiri sikufunga nae ndoa nilimchukua kienyeji tu niliwaza baadae ndio nifunge nae ndoa.
Kiukweli ilipelekea hadi baadhi ya ndugu zangu baadhi kutowasiliana na mimi kwa kitendo nilichomfanyia yule msichana, hata baadhi pia ya washikajj zangu walinionya sana kutokana na kule tulipotoka na yule msichana.
Baada ya miezi miwili hivi mambo yangu yalikuwa yakienda ovyo sana kila mahali, mpka ikafikia nilifilisika miradi yangu yote na kubaki nikitegemea mshahara kwani biashara zilikuwa haziendi kabisa.
Kiukweli maisha yalibadilika sana kibaya zaidi huyu mke niliyemchukua kijijini amebadilika tabia amekuwa ni mtu wa masaluni na nilishawahi mfuma na mshikaji Tena wa mtaani.
Nilishangazwa sana hasa ukiangalia hata miez sita hatujamaliza amekuwa mt wa pombe na yeye tabia take si nilivyotegemea.
Nawaza sana jamani najuta najuta mimi mpka hivi sasa nina wiki nimemrudisha kwao.
Ninaumia kupita maelezo. Aibu aliyonitia ni ya karne. Kila nakopita nasemwa mimi..
Najuta jamani nimetenda dhambi ya kuumiza moyo wa mwanamke aliyenipenda kwa dhati, aliyenivumilia kwa yote, mwanamke aliyejiheshimu.
Naamini kabisa sidhani kama ntampata kama yeye. Nimeamini akili za kuambiwa ongeza na zako sikulitambua hilo!
Niko njia panda sielewi pa kuelekea najipeleka tu. Naamini wapo watakajifunza kupitia mimi.
MWANAMKE TABIA.....NIMEAMINI..
(Naomba mnisamehe niliowakera ila naumia nahisi kama laana hivi).