Mchumba wa rafiki yangu ametoa mimba

God bell

JF-Expert Member
Joined
May 13, 2011
Posts
590
Reaction score
211
Za jiona wana MMU. Labda nianze hivi. Kuna dawa wanatumia baadhi ya wanawake za kutolea mimba pindi wanapojigundua wana ujauzito. Hawa wanawake wanakuwa hawana hofu ya Mungu kwani kitendo kama hicho ni cha mauji. Unaua kiumbe kisicho na hatia. Huyu rafiki yangu alikuwa na mchumba wake wakipendana sana, siku anampeleka kwao wazazi wa kijana walipomona walimkataa katu katu hadi kijana akachanganyikiwa (sijui ni mila za kwao) wakati huo bint wa watu tayari alikuwa mjamzito wa mwez 1. Namejua hili jambo manake nilikuwa rafiki yao wa karibu na walikuwa wananishirikisha baadhi mambo yao. Baada ya jamaa kuona mchumba wake amekataliwa ikabidi ampe ukweli kwamba haitakuwepo ndoa tena. Bint akajaribu kumkazia jamaa amwele ukweli kama kuna tatizo ajirekebishe, jamaa akamwambia ''wazazi wamesema nikikuoa nitapata laana kwa kuwa wameshanikataza''. Bint kuona hivo akanitaarifu nikajaribu kuongea na jamaa kadri nilivoweza lakini ikashindikana. Baada ya wiki moja yani jana bint akanipigia sm akaniambia 'shemeji nimeamua kuflash ile mimba, siwezi kutunza mimba nizae mtoto asiekua na malezi ya baba'. Nimesikitika nikamuliza umefanyaje?akanijibu nimeamua kunywa dawa nikaflash kiumbe chake, nitamuomba Mungu anisamehe. Hadi nimejiuliza ni dawa gani hizo wanazotumia? Je wanajiamini nini hawa wanawake juu ya kifo? Inauma sana!
 
Pole sana. Lakini jamaa kwanini anamtambulisha mtu baada ya kumpa mimba? Halafu naye anakuwa upande wa wazazi akijua mwenzie mjamzito?!

Kukataliwa hakumpi mtu nafasi ya kutoa mimba maana hiyo mimba walishiriki wote kuiandaa, hivyo kosa ni lao wote huyo kiumbe hana kosa lolote.
 
Hivi ni bora kutunza mtoto bila baba ama ni bora kutoa mimba?
 
Dah ni uvivu tu wakufikiri mbona watoto wengi tu wamelelewa na mama peke yao. Hiyo dhambi ya mwanamke unless walikubaliana.
Angezaa then adai malezi ya mtoto,
What if kaolewa kazaa then mwanaume kafariki ataua watoto au?
 
Kutunza uhai ni jukumu la kila mtu! mtu anasema atamuomba mungu amsamehe huku anajua ameua, Mungu hasamehi kosa bila mkosaji kujutia! unafanya then unapanga ntasamehewa mwambie anajidanganya yampasa ajute kuua kiumbe cha Mungu kwanza!!!!!!!!!!!!!!!
sijaona mchango wa urafiki wako kuhusu kutunza uhai wa hicho kiumbe kilichotolewa wewe ulikazania ndoa tu!!!!!!!!!!!
 
Hivi ni bora kutunza mtoto bila baba ama ni bora kutoa mimba?

Bora kutunza mtoto bila baba,sioni sababu ya ulazima mtu kutoa mimba. Hata kama unahali ngumu kiuchumi unampeleka hata ustawi wa jamii. Halafu hakua na haja ya kutoa wakati kijana yupo na angeweza kuliongelea hilo jambo kwenye familia sidhani kama wasingeikubali damu yao na kuitolea matunzo hata kwenye sheria angeweza fika endapo wangeleta ukaidi juu yamtoto.
 
Hivi ni bora kutunza mtoto bila baba ama ni bora kutoa mimba?

Mi kama mwanaume siwezi nikakubali mtu atoe ujauzito wangu. Mbona wapo single mothers ambao wapo na furaha with their kids.
Mi ninao marafiki zangu wawili wasichana/wanawake wana watoto wa umri wa kuanza shule ya msingi sasa hivi, wananiambiaga "my ......(kids name) is the best thing i have ever had in my life"

Waliotoa mimba huishia kuwa kichekesho kwa tunaojua. Na tanawasamehe hawa single mothers kwa urahisi na kusahau makosa yao lakini sio wale walioshusha injini thamani yao inakuwa imeshuka sana.
 

Mkuu bint amenipa taarifa baada ya kukitoa hicho kiumbe. Anajua wazi angeniambia kabla ningemzuia kufanya hivo.!
 
Ni rahisi sana kwa kosa moja kuzaa kosa jingine...

Binafsi nilichokigundua hapo ni hii tabia ya baadhi ya makabila wazazi kuingilia suala zima la uchumba wa watoto wao. Kuna makabila flani flani wazazi wanataka watoto wao waolewe/kuoa kabila lao tu na si vinginevyo
 
Binafsi nilichokigundua hapo ni hii tabia ya baadhi ya makabila wazazi kuingilia suala zima la uchumba wa watoto wao. Kuna makabila flani flani wazazi wanataka watoto wao waolewe/kuoa kabila lao tu na si vinginevyo

Mambo ya kizamani sana hayo. Halafu kwa staili hiyo nishaona jamaa mtaani kwetu dada zake wakimharibia maisha kwa kumchagulia mtu wanaemtaka wao wakamponda binti jamaa aliyemchagua sababu ya kabila lake kwamba ni wahuni.
Mshkaji akapewa mke na dada zake miaka mitatu haikupita ndoa juu ya mawe wana mtoto ndoa haikaliki tabu tu kwa mtoto.
 
Familia zingine ni janga la kitaifa
 
Pls don't judge...u have not been in her shoes,kukataliwa na wakwe mnaona ni jambo dogo?mnajua hali yake kiuchumi na kimaisha kwa ujumla??!!..
Mtoa mada,this is time u have to prove ur friendship na sio kuja kuyatangaza MMU,yashatokea,she is frustrated,BE THERE FOR HER,
 
daa!kiukweli waliotoa mimba huwa napenda xana na wenyewe wafe palepale!
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…