Mchumba ninayekaribia kumuoa simuelewi

Huyo hakufai usioe kwa kumlizisha mtu oa kwa mapenzi yako.
 
yaelekea wewe ni msafi kupitiliza na kwa mimi wanaume wa jinsi hiyo huwa ni wasumbufu sana kwa wapenzi wao ama inawezekana wewe ni bahili sana sasa kutaka mkale chips anakukomoa tu, jirekebishe upande wako halafu na yeye mueleze ukweli lakini pia usifanye haraka kutangaza ndoa. mpaka sasa naamini hamuendani!
 
The secretary mi hapo sioni matumaini ya mtu kubadilika. Unadhani mama yake alomlea toka utotoni na hakumfundisha kuwa msafi na mchapakazi; ataweza leo hii kumpa crash program eti kisa kapata mchumba. Hao wazazi wamemlea hivyo alivyo na kuna possibilty kubwa hawaoni hizo kasoro anazolalamikia jamaa. Si unajua like mother like daughter.


 

kaunga hata kama wakiajili majukumu ya mwanamke ndani ya nyumba lazima ayatimize yani hata kufua nguo za mmewe waajili mtu! msaidizi anakuwepo na uwajibikaji nao unakuwepo ndo maana muda mwingine tunalaumu wanaume kwa kuwa na nyumba ndogo kama masuala yenyewe ndo haya hebu imagine ndo wamepata mgeni ataenda kununua chips.yeye akae naye ampe makavu laivu bila chenga kwa kweli namchukia mwanamke mvivu ukute hata kupika hajui
 
Na asikudanganye mtu kuwa utakuwa na msaidizi maisha yako yote. Mi kuna siku nimerudi home house girl ananambia amepigiwa simu baba yake yuko hoi. Hapo kama huwezi kufanya kazi (kama kilema) inakuwa vipi???

Pili hizi nyumba unazokuta zinatoa harufu si kwamba hazina house girl ila house girl wa mtu mchafu jua fika naye ataunda trela ukizingatia kuwa wengi wametoka nyumba za udongo vitu vingi ni vigeni kwao. Mwalimu (mother house) ndo hivyo mchafu...yeye usafi atajifunzia wapi???


 

kweli tena haya masuala ya mtoto kupelekwa boarding akirudi hafundishwi wajibu wake unaponza na aibu kwa mzazi pale mtoto atakapoolewa huu usasa usio na kipimo ni tabu tupu
 

hakuna usafi uliopitiliza ila ni uchafu uliopitiliza nampongeza kwa usafi wake na kugundua kasoro za huyo dada mi nawashauri wa kaka kabla ya kuoa wawe wanafanya test ya hivi
 
hapo unahitaji kufanya maamuzi magumu ......uchafu khaa nyumba itakuwa haifai hapo mpo 2 ikifikia kuwa na watoto utakuta pampers kwenye vyombo kwa uvivu
 
Kichwa kinauma.

Pole sana kaka usiendelee kuumiza kichwa we unafaa kuwa mme kweli leta mdada wa kufanya kazi wa siku moja halafu akimaliza shughuli msifie mbele yake kwa kukejeli mwambie naomba mfundishe mchumba wangu kazi akileta mizengwe hapo ndo pa kuanza kumpaka
 

hivi upo serious na ukisemacho? kama hakuna haja ya mwanamke kujua hayo yote kwani huyu housegirl yeye si mwanamke .kwa hiyo dobi ndo atamfulia hadi nguo za ndani? hawa wasaidizi ndo wamfanyie usafi hadi ndani binafsi mi hata kufuliwa nguo zangu na mtu yoyote haiwezekani labda kama ni mgonjwa hata mafundisho ya dini yanakemea uchafu na uvivu na kuonyesha wajibu wa mke katika familia
 
Maoni yenu ninayafanyia kazi. Nitakaa nae chini kwa upole na kwa lolote nitaleta kilichojiri mnipe ushauri zaidi. I'm so confused.
 
Maoni yenu ninayafanyia kazi. Nitakaa nae chini kwa upole na kwa lolote nitaleta kilichojiri mnipe ushauri zaidi. I'm so confused.

pole kwa kuchanganyikiwa kuwa mwangalifu anawez kubadilika kwa kutaka ndoa baada ya hapo akarudia tabia yake hiyo ukachanganyikiwa zaidi
 
unajua shida ya kuishi na jitu lenye maneno ya kejeli wewe? Mbona mwenzio anakuvumilia na udhaifu wako?

Ukitaka mwanamke/mwanaume perfect muumbe wa kwako, la sivyo maisha ni kuvumiliana.....

Kuhusu kufua simple si wote mna kazi changeni laki nane nane mmnunue mashine ya kufulia....

Zungumza nae kuhusu kupika (ila mmmh huyo nae uvivu kapitiliza hata kupika??????) je anarudi amechoka sana?

Kama kuna wanawake watu wazima kwao zungumza nao, waketi nae na kumfundisha majukumu ya mke kwenye nyumba.....

Na kama mna uwezo wekeni house girl, maana kumbuka wewe unafanya kazi yeye anafanya kazi, mkirudi ofisini wewe unachukua remoti na yeyeaingie jikoni kupika, aoshe vyombo, asafishe nyumba, uwanja, apige pasi mwisho ya siku atachoka ashindwe kukupa unyumba urudi hapa na thread mpya......

Swali la nyongeza, mnaporudi ofisini unamsaidia kazi? Au wewe miguu juu mwenzio ahenyeke?
 

Ajirekebishe halafu awe mchafu au?...
 

mkuu, watu wote hawapo sawa! sasa unataka kuniambia asiyejua kupika au kufua haolewi? halafu nani amuoe? we mwenyewe ushasema unadharau, hasira nk nk... unadhani nani anapenda kuolewa na mtu mwenye tabia kama zako??? Hapo hamna cha dini wala nini, ingekua unafuata dini basi wewe unatakiwa kula kwa jasho na yeye atulie nyumbani kukufulia nyumba kubwa , Blaki Womani
 
Last edited by a moderator:

Kwa sasa hatuishi wote maana tuko kwenye michakato ya ndoa lakini mara kadhaa anakuja na kukaa siku mbili tatu.

Kusema ukweli mimi nafanya almost vitu vyote, kwa mfano nina uhakika hajawahi kuosha vyombo!! Tukishakula(hata kama ni chips) ataacha sahani chafu mezani na kukaa sebuleni moviez. Either mimi nitoe na kupeleka kwenye sink au na mimi niache.

Mara nyingi napenda kukaa zangu chumbani au kwenye computer tu maana ananikera.
 

kwanza mie sio mtoa mada halafu sio me.vilevile hujajua raha ya ndoa ni pamoja na kutimiza majukumu na wajibu sidhani kama kuna mtu anayemfurahia mtu mchafu na mvivu
 
Last edited by a moderator:
Maoni yenu ninayafanyia kazi. Nitakaa nae chini kwa upole na kwa lolote nitaleta kilichojiri mnipe ushauri zaidi. I'm so confused.

Hakyanani mkuu kweli naona umekereka sana...Raha ya nyumba mwanamke awe msafi na mchapa kazi.
 

Similar Discussions

Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…