Mchumba na michepuko

Mchumba na michepuko

Naamini mko salama sana wanajukwaa hili pendwa.
Humu nafurahi kwani nakutana na mengi ya kufunza hasa kwa sisi tunaotazamia kuja kuwa wanandoa

Hapa nina tatizo kidogo na mchumba wangu nilifuma text za madada kama wa3 hivi na wote anachati nao kama wapenzi wake.

Nilichofanya nilimuonesha zile text akachanganyikiwa.akatoka akajifungia kwa gari yake then akarudi rum akalala mie wala sikumuhoji nikalala pia.
Kesho yake nikaenda job kama kawaida wala hatukuongea lolote.jioni tukalala pia hatukuongea baada ya kuona hivyo nikaamka asubuhi sana nikamwambia imetosha ndo mwisho wangu na yeye akanipigia magoti na kuanza kulia anaomba msamaha.
Akawapigia hao watu mbele yangu akawaambia wasijuane then alikuwa na safari akasafiri
Toka aondoke hii ni siku ya nne sipokei Simu yake bado namfikiria

Emu wakuu mtu kama huyu ni husband material kweli au nimekuwa nae kwa mda mrefu kidogo

Ushauri wenu wakuu,

yeah ni husband material,kwako amefika hao wengine alikuwa anafanya mazoezi,
 
kazi ipo ndoa oct pole yako kwa kuingia ktk ndoa iloanz misukosuko mpm ndo bc tn keshakuw mchumba pokea cm
 
Achana na hao wadada wa mitandaoni anao chat nao wesikumize kichwa. Cha muhimu ni nani yupo nae kila siku, ni wewe hapo. Kwa hiyo wewe ndiyo wake hao wengine ni danganya toto. Na haya mambo ya kuchat na watu tofauti yanatokeaga kama sehemu ya kupoteza muda.
 
"Hata Mimi sikuhukumu nenda zako na usitende dhambi tena". Kama kwenye vitabu vya mapokeo wanasamehewa itakuwa wewe? Wanamke unatakiwa kuwa faraja, ngao na kinga ya mwenza wako. Kila wakati uwe moyoni mwake kwa kupitia Matendo mema unayomfanyia. Kwa kisa ulichosimulia nakusihi ubadili"approach"ya kuzikabili changamoto za kwenye mahusiano vinginevyo ndoa yako haitadumu.
 
Bado siko happy na yeye nafikiri japo ajue ni kiasi gani nimeumia .hawezi kunywa sumu

Ndiyo upokee simu sasa umueleze hayo, binadamu akifikia yield point huwa hatabiriki
 
Samahani wakuu naomba tu-reverse kidogo hii Habari. ....tufanye mkaka ndio kakuta hizo sms then mdada kalia sana na kuomba msamaha na ndio huyo "mke mtarajiwa" wa mkaka.......ingekuaje? ???
 
Back
Top Bottom