Mchumba kadhoofisha ujamaa wetu

markbusega

JF-Expert Member
Oct 12, 2015
826
847
Habari wanajf!

Ni hivi huyu ni jamaa yangu sababu mjomba wake alimuoa shangazi, na pia tumesoma darasa moja O level na tuliunda group discussion moja.

Tumekuja kumpenda dada mmoja kwa nyakati tofauti mimi nilikuwa wa kwanza kutangaza nia mwenzangu kumbe alikuwa na nia akawa anashindwa kumwambia huyu dada ila alipenda tu kumtembelea kupiga tu story naye.

Toka niwe na huyu dada huyu jamaa yangu tumefarakana kiaina amebaki mnafiki tu kwangu yuko passive sana mbaya zaidi anawatangazia marafiki zangu kwamba nilimnyang'anya mke.

Hajaacha tabia ya kumfuatilia mchumba wangu huenda nyumbani kwao mchumba wangu wanamchora tu anahangaika kweli, huyu jamaa mimi mwanzoni nilichukulia anahangaika tu atazoea na kumuacha mchumba wangu sasa naona ndo anazidi mchumba wangu amenishauri nikae naye mbali sio mtu mzuri

Niko njia panda nipeni ushauri juu ya hili wakuu
 
Ulishawahi kumtambulisha au ndio unategemea yeye ni mtu mzima atajiongeza??
 
teh... umesema vema...et jamaa anamfata fata huyo msichana alafu msichana anakwambia wewe mwanaume kaa nae mbali..

dah
Ukute huyo msichana ndo anayeendekeza ukaribu na huyo mshkaji zen akiwa na jamaa yake anajifanya kuponda..

Heri ya siku ya wapendanao mkuu
 
Ukute huyo msichana ndo anayeendekeza ukaribu na huyo mshkaji zen akiwa na jamaa yake anajifanya kuponda..

Heri ya siku ya wapendanao mkuu
asante...
sikukuuu wap br..

msichana anawachezeaa akili..
 
Mkuu sikukuu naianzia kwa Raimundo ..Kuna sherehe ya siku ya kuzaliwa ya mwanae..Zen usiku ntaenda Bilz na wife kushangaa mimba ya Wema teh

mimba si jecha kaitengua mkuuu...

mtoto wa Raimundo ni wakike.. hivi anaumri gani?...teh nipo single...

ila nitatoka na mchepuko..late night
 
mimba si jecha kaitengua mkuuu...

mtoto wa Raimundo ni wakike.. hivi anaumri gani?...teh nipo single...

ila nitatoka na mchepuko..late night
Ndo nataka nikaakikishe mkuu..Kama ipo au imetenguliwa kweli...

Nilimuuliza jinsia ya mtt wake akasema amesahau..Nadhani leo atatupa jibu..Tusije kujichanganya kwenye zawadi

Vipi Cute b umempiga chini?
 
Acha roho mbaya mkuu...muache mwenzie naye aonje aupoze mtima wake....kwani anaondoka nayo.....huo ni ubinafsi....
 
Ndo nataka nikaakikishe mkuu..Kama ipo au imetenguliwa kweli...

Nilimuuliza jinsia ya mtt wake akasema amesahau..Nadhani leo atatupa jibu..Tusije kujichanganya kwenye zawadi

Vipi Cute b umempiga chini?
teh kaamua kusema....jinsi ya mtoto...

japo hilo jibu sinA uhakika nalo...nenda kahakikishe ulete mrejesho mkuu..

taanzaje kumpiga chin...mkuu
 
Back
Top Bottom