Mchumba amepata mimba na mimi najenga

Nakushauri, anza maisha mara moja. Maji yameshamwagika. Kujenga mtajenga mkiwa pamoja. Tena ni vizuri kusaidiana kwenye majukumu kama hayo ya ujenzi na malezi ya ujauzito na kijacho.... Hata mkianza kuishi nyumba ya kupanga, sio mbaya, muhimu na uzuri mna pa kujenga na mtaji.
 

nnashkuru
 

kama ndo ivo,na wewe ungesubiri, usingemdinya kwanza hadi umalize kujenga, nadhani hapo utakuwa umeelewa cha kufanya,
 

mchumba wako kivipi?Wakati hata mahari ujamtolea?
 
sio kwamba nashindwa kumuoa ila nikimuoa kujenga ni baadae sana mana plus mahari na kulipa kodi na garama za kuendesha maisha zitakua tofauti

Umesema hapo mahali bado ujalipa so huyo so mchumba.
 

Hebu kaka nionyeshe hilo andiko hapa..walawi sura ya ngapi mstari wa ngapi??na binti hata hujamlipia mahari unamhalalisha eti mchumbako??lea matunda ya uzinzi wako..mungu kakataza kufanya mapenzi kabla ya ndoa we unahalalisha kama nani???!!!

Nyau wewe!!"
 
sio kwamba nashindwa kumuoa ila nikimuoa kujenga ni baadae sana mana plus mahari na kulipa kodi na garama za kuendesha maisha zitakua tofauti

Usijitoe ufahamu wewe mimba imeshaingia tayari unaanza kujiulizia, maisha tunayoishi ni uchaguzi wetu wenyewe maana mwanzo ulichagua kujenga nyumba lakini ukashindwa kuendelea na program hiyo ukaamua kuchagua kumpa mimba hivyo itabidi option ya pili ya mimba ndio uifanyie kazi kwa kuwa imewezekana kupatikana hata bila ya kuwa na nyumba. na isitoshe watu kibao wana watoto kibao lakini hata chumba na sebule hawana
 

kumbukumbu LA torati 22:28
 
mchumba wako kivipi?Wakati hata mahari ujamtolea?

ukijitambulisha kwao na mkapanga mahari na mibaraka yote mkapewa ikabaki tu kuitoa hiyo mahari bado hajawa mchumba au mpaka pesa ikae mezani
 

Lol! Mdogo wangu unachanganya mada! Mara mimba mara ujenzi! Mm nadhani ujenzi uendelee na mimba iendelee kuwepo, maana mimba cyo ugonjwa! Y haukuvumilia mpaka mfunge ndoa!?
 
sio kwamba nashindwa kumuoa ila nikimuoa kujenga ni baadae sana mana plus mahari na kulipa kodi na garama za kuendesha maisha zitakua tofauti
Dogo acha uoga, panga chumba fasta na ufunge ndoa. Siku hizi hakuna mambo ya mahari labda useme huna hela ya kodi kitu ambacho ni uvivu.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…