Mchumba amekuwa mbogo!

Mchumba amekuwa mbogo!

Nchaby

JF-Expert Member
Joined
Aug 12, 2013
Posts
797
Reaction score
259
Habari zenu wana jamvi.

Nakumbuka ilikuwa Juni 2012, nilipokutana na dada huyu aitwaye Apaikunda.


Kama ilivyo kawaida ya wanaume, siku hiyo nikamwomba namba yake ya simu, hakusita, akanipatia. Tulikuwa tukiongea kwenye simu mara kwa mara na kutumiana sms mara nyingi.


Siku moja wikendi nikamtafuta, hakusita kama ilivyokuwa mwanzo. Tukakutana sehemu moja ya wazi kwa minajiri ya kutaka kufahamiana zaidi.


Maongezi yetu ya kwanza yalichukua kama masaa matatu hivi na ndio yaliyopelekea kumfahamu dada huyo kuwa anaitwa Apaikunda na ni mwajiriwa wa kampuni moja hapa Jijini.


Ndani ya masaa hayo matatu nilimtolea yangu yote ya moyoni. Jibu lake lilikuwa "kaka nina mchumba wangu nimpendaye sana na tayari tumeshatambulishana kwa wazazi".


Kila nilipojaribu kumwonyesha nia yangu ya dhati, kwamba lengo na madhumuni yangu siyo kumpotezea muda, bali kwa uhakika ni kumtaka awe wangu wa kufa na kuzikana.


Jibu lake lilikuwa moja tu "pole kaka, ulishachelewa na sina namna yoyote ile ya kufanya kwani niliyenaye ananitosha na nampenda mno na siwezi kumwacha wala kumsariti".


Kiukweli huyo Apaikunda ana sifa zote za kuitwa dada mrembo. Ana kila kitu ambacho mwanaume yeyote yule anakihitaji kwa mwanamke.


Kiufupi yuko kwenye orodha ya wale akinadada wachache mno wenye umbo adimu, uso wenye sura ya upole na macho makubwa ya mviringo yanayotaka kama kudondoka hivi na yakusinziasinzia huku nyuma akiwa amefungashia mzigo mkubwa sana usiowiana na mwili wake!!!


Kikao chetu hicho kilimalizika siku hiyo pasipo kutozaa matunda yaliyotarajiwa, tuliagana siku hiyo, na kila mtu akachukua njia yake.


Baada yakama mwezi mmoja hivi kupita alinitumia sms kunijulia hali, kwani tangu siku ile mie nilikata tamaa kabisa na niliheshimu na kukubaliana na msimamo wake. Hivyo sikuwa namewasiliana naye tena.

Siku moja baada ya kama miezi miwili kupita, alinipigia simu na kusema anataka kuja kunitembelea nyumbani ninapoishi. Mie nikaona kama vile kuna kila dalili za mwanga wa matumaini kuchanua.


Haraka haraka nikamwambia karibu sana. Siku ya jumapili dada akatia timu nyumbani kwangu ninapoishi. Lakini cha kushangaza msimamo wake ukabakia vilevile. "Kaka ulishachelewa soon nitaolewa".

Nilichukia vibaya mno. Kila nilichojaribu, nilionekana kama mtoto mdogo ambaye yuko chekechea katika darasa la kushawishi, kubembeleza na kutongoza. Kila nilichojaribu nilijibiwa kabla ya kumaliza sentensi.

Hasira, machungu, huzuni na fadhaa nilivyokuwa navyo siku hiyo nilihisi kama vile moyo wangu unataka kupasuka na huku kijasho kikinitoka. Wakati fulani nilisahau kama pale palikuwa kwangu na kutaka kuuliza mahali toile ilipo!!!

Wiki kama tatu hivi baadae, Apaikunda alinipigia simu akasema anahitaji kuja tena kunitembelea nyumbani. Mie nikagoma, akasema hapana, anajambo anataka kuja kunieleza. Siku ikafika, akatia timu tena.

Akasema anakubali kuwa rafiki yangu, lakini hatutooana. Nilikubaliana naye kwa shingo upande. Mie nilimtaka jumla jumla, yeye ananitaka rejareja. Kweli hii ni sawa??

Lakini siku hiyo tofauti na siku yakwanza, tulikubaliana kugegedana.
Duuuuu!!! Kweli nimeona maumbo mengi ya hawa viumbe, lakini hili umbo lilikuwa balaaaaaa!!!!!

Tangu siku hiyo ikawa kama kawaida yetu mara kwa mara.

Sasa wanajamvi, nimempata mchumba harisi mwenye kutaka mme na aliye tayari kuishi na mimi kwa muda wa maisha yake yote.

Na habari hii nimeifikisha kwa Apaikunda kama ilivyo. Sikutegemea, dada kacharuka, kawa mkali mithili ya mbogo aliyejeruhiwa. Eti alishaachana na bwanake siku nyingi, nisithubutu kufanya hivyo.

Na amenitamukia wazi kwa macho makavu kabisa kwamba nisipomuoa yeye mwaka huu sitaumaliza!!

Wanajamvi, kuna usalama kweli hapa??


Angalizo: kama huna cha kuchangia, pita kimyakimya.
 
Japo jukwaa hili si mahali pa hoja yako, lakini kwa ufupi nitakujibu kwamba, ulikosea pale ulipokubaliana na yeye kuwa na urafiki wa rejareja kiasi cha kuwa mnagegedana mara kwa mara. Kama kweli shida yako ilikuwa ni kuoa, ungelisimamia msimamo wako huo huo na yeye angekuheshimu. Lakini sasa umeshachemka. Kwa taarifa yako usalama haupo. Ni heri kabisa umuoe.
 
Kwa maneno machache kabisa, umelikoroga na sasa unalinywa.

Huenda mwanzoni zile sitaki nataka zilikuwa ni kupima upendo wako kwake.

Hatimaye ukanasa kwenye mtego wake na bibiye akajua ndio kakumiliki mazima.
 
Kweli sio mahalipake -- ila na mie naomba tu nimsaidie kiaina yake. Uwe na hakika sio bogo -- badae ya ndoa akukimbya miaka 2 na kurudi then anatumia pesa zako kuhonga wavijana nakuibiwa gesti. Alafu mitaani unaitwa mume -----
 
Siyo lazima umwoe kwa sababu kwa makubaliano yenu ya awali hamkuwa wachumba, just friends with no vision wala mission yeyote for future , mnabomoana tu, pia yeye hakuwa mwazi kwako partly alikuwa in and other part kwa mshikaji!
Tuachane na hayo, mapenzi is very wide issue, chukua hizi changanya na zako!
 
Genye mbaya sana,uliwezaje kumla mzigo mtu ambaye hakuwa na mahusiano nawe?
Mbali na hivyo,ukakubali kabisa kushare penzi na mwanaume mwenzio.Sasa umepewa hati miliki unajifanya unataka kuoa kwingine.
Sasa huyo kakupa onyo,R.I.P brother kama huyo demu ni unne wa saro.

"Nlikuwepo":bolt:
 
Mkuu! Uliwah kumuuliza "Apaikunda" maana yake ni nini?

Maana majina yetu haya mengine ukiambiwa maana, ndio utajua maana..
 
  • Thanks
Reactions: y-n
Kwa maelezo yalivyo uhusiano wenu una kama mwaka na nusu hivi, kweli kwa muda wote huo usijue kwamba kaachana na bwana yake?(kama alikuwepo). Kwa kipindi chote hiki asigusie kumove to the next step kama kweli alikuwa/ana na mpango wa kuolewa na wewe?!
 
dada mkali...kwa kuwa hisia zake keshazitoa,,soo kuwa makin mkuu....mwaka huu bado mrefu...tuna zaid ya miez tisa mbele mwaka uishe,,,,,angalia asee
 
Mbona huku sio jukwaa lake..........umechepuka ndugu...
 
Huyo uliyempata amemzidi Apaikunda umbo na hayo macho au? maana ulivyomsifia wakati hata mm ninavyo sema tu nimevifungia kwenye bag..!
 
pole we! Hyo inaitwa the game of love,ama zako ama zake,halafu inaonyesha haukumjua vzr huyo bint kmb usijue km yuko na mume kwel au lah?,kosa kubwa ulilofanya ni kukubal kujiingza kny uhusiano na mke wa mtu fek,hapo umelikoroga we linywe tu.
 
Ujinga unaona tamu sasa linywe Urafiki Hadi kugegedana acha akukomeshe
 
Mkumbushie ahadi yake kuwa mtagegedana lakini hamtaoana, nadhani atakuwa ameshasahau

Mkuu kapalamsenga, nimemkumbusha sana na naendelea kumkumbusha, haelewi kabisa. Na hata anaposema kuwa aliachana na huyo mchumba wake hakuwahi kuniambia hata siku moja.
 
Ujinga unaona tamu sasa linywe Urafiki Hadi kugegedana acha akukomeshe

Kaja kwani kosa langu nini mpaka anikomeshe? Kugegedana ilikuwa makubaliano ya wazi kabisa yasiyo na lengo la kuoana.
 
yupi kati yao yuko moyoni?mana uzuri sio sura,pozi na umbile ila abia,hekima na ukarimu.nadhani wewe ulipenda vinavyoonekana bali si vya moyoni.sasa umiza kichwa utatokaje hapo.
 
Huyo uliyempata amemzidi Apaikunda umbo na hayo macho au? maana ulivyomsifia wakati hata mm ninavyo sema tu nimevifungia kwenye bag..!

Nimempata dada mmoja very simple and woman material ninachokiwaza, ndicho na yeye huwaza.
 

Similar Discussions

Back
Top Bottom