Mchoro wa fly over ya Tazara itakavyokuwa

Mchoro wa fly over ya Tazara itakavyokuwa

Kwani fly over ni ya safari kabisa au inakua kwenye makutano tu?
Hiyo inakuwa kwenye makutano tu inasaidia kuondoa keroo ya kusubiri taa zikuruhusu na mala nyingi fly over huchukua nafasi kubwa ili iweze kurahisisha magari kupita upande wowote lakini hapo Tazara haiwezekani ni padogo saaana magari yanayo toka mjini kuelekea Buguruni yatahitaji mzunguko mkubwa hichoo ndoo kikwazo na hivo hivo upande wa magari yanayotoka airport kuelekea bandari
 
Sishangai hiyo michoro ikifanyiwe kazi 2070 maana hata daraja la kigamboni na Malagarasi yalichorwa kipindi cha Mwalimu.
 
Sishangai hiyo michoro ikifanyiwe kazi 2070 maana hata daraja la kigamboni na Malagarasi yalichorwa kipindi cha Mwalimu.
Daraja la Kigamboni la kuombea kura, nafikiri hata hio fly over itajengwa mwaka 2019
 
mchoro wenyewe haujakamilika unaonekana upande upande tu halafu haueleweki
 
Wakimaliza kujenga hiyo wanajenga hii Morogoro
article-0-04E3828D0000044D-979_468x286.jpg
 
Mipango ya kuambiwa
Ile DART morogoro road tayari imeshafeli hata haija maliza.
TRL walitoa ushauri ijengwe metro sehemu ile lakini wakasikiliza WB.
Leo tumejengewa road kama inapita train.gari ikiharibika siku hio hakuna safari.yaami akili zetu sio zile za kuchanganya na zetu bali ni zao tu...huu ni msiba
metro isingewezekana umeme wenyewe wa kuunga unga labda zingejengwa barabara 4 kwenda na kurudi au hata 3 tu kutoka town hadi kibamba
 
serikali ya tanzania imeanza kutekeleza ujenzi mkubwa wa barabara za juu na chini (fly overs) katika jiji la DSM ambapo fly over ya TAZARA imeanza kujengwa rasmi.

Taarifa zilizotolewa na wizara ya ujenzi zimesema kuwa mkandarasi wa ujenzi huo yuko site hivi sasa ambapo ujenzi wa daraja hilo umeanza jumatatu tarehe 14 july 2014 na utakamilika baada ya mwaka mmoja. Hii ni hatua ya kupongezwa katika kutatua tatizo la msongamano wa magari jijini dsm.

Imeelezwa kuwa barabara hiyo ni ya kistrategia kwa sababu magari yote makubwa yanayotoka na kuingia bandarini sasa yatapita kwa urahisi. aidha watumiaji wa barabara wa kawaida wa mjini dsm wataepukana na kero ya foleni.
ikikamilika inatarajiwa kuwa hivi.
tazara-flying-over-jan26-2013.jpg


IMG_2837.JPG
 
Kaanza kweli au yupo tayari site.Sababu kuwa site na kuanza kazi ni vitu 2 tofauti sana.Ila tusubiri yaliyomo yamo?
 
Weka picha, acha porojo zako makufuli!
 
Kaanza kweli au yupo tayari site.Sababu kuwa site na kuanza kazi ni vitu 2 tofauti sana.Ila tusubiri yaliyomo yamo?

ujenzi umeanza mkuu,wakati taarifa inarushwa mitambo ilikuwa inanguruma ikiwa ni pamoja na magreda,na mabuldoza yakiendelea na kazi
 
Fly over moja tu kwa hali tuliyo nayo haitoshi. Tujenge pia makutano ya Morogoro na Mandela, Morogoro na Kawawa na Nyerere na Kawawa pia Mandela na Tabata.
Barabara za mzunguko (ring roads) nazo zipewe kipaumbele: Mbezi Beach - Goba - Mbezi Louis - Kinyerezi-Uwanja wa ndege na Bunju - Magohe- Morogoro- Kwembe-Kisarawe.
 
Back
Top Bottom