Mchome ni Mungai mwingine

Mchome ni Mungai mwingine

MchunguZI

JF-Expert Member
Joined
Jun 14, 2008
Posts
4,038
Reaction score
2,224
Sijui ni kwa nini wizara ya elimu Ina bahati mbaya kiasi hiki. Ilikuwa Enzi ya Mungai, akiamua kuharibu elimu kana kwamba ni biashara binafsi. Sasa tuna timu mpya, akina Kawambwa, Mulugo na Mchome wao.

Huyu Mchome Hana tofauti na Mungai. Nahisi amepata nafasi hiyo bila kutegemea na anajaribu kuonyesha kwamba kichwa kiko safi. Siamini!

Wozara ya elimu ni zaidi ya Mchome na kufikiri kwake. Ilistahili atulie na kuwahusisha wadau badala ya kuita wanahabari na kit angalia div.5. Ha kuifanya hivyo na ndo maana wengi tunaona ni mtu mwenye vituko na binafsi namuona Hana tofauti na Mungai.

Najiuliza, ni nani anawatuhusu watu Kama Mchome kuchezea elimu yetu? Je, sera au mipango inapangwa n mtu mmoja ndani ya wizara?

Huyu Mchome asipoangaliwa kwa makini, anaiharibu tena elimu yetu kwa Mara ya pili.
 
kuna mtu alianzisha uzi hapa akiwa na evidence za kutosha akipinga kabisa Sifuni mchome kupelekwa wizara ya elimu !
 
Uteuzi wake umetokana na kazi ya Uenyekiti wa Tume ya matokeo ta K4 ambapo walipendekeza matokeo yafutwe na kupangwa upya. Kwa hiyo alichokifanya sasa ni kuhakikisha aibu ya kufuta matokeo na kuyapanga upya. Amekaa kisiasa zaidi hana uzoefu kwenye sekta ya elimu na atapwaya sana kwenye hicho kiti
 
Watanzania kwanini tunakuwa carried na emotion bila kujali objectivity wa hoja? Suala la mabadiliko ni suala ambalo lazma tulikubali, ila tunapaswa kulikubali kama lina facts za kisayansi. Na kama lina facts za kisayansi tulijadili kisayansi siyo ku attack personality as mtoa maada anavyofanya. Ni tabia mbaya.

Pengine hujaelewa mabadiliko katika mfumo wa elimu yamekusudia nini. Labda nitumie theory za mantiki (logic) kuangalia maamuzi ya wizara.

Wizara imefanya uchunguzi kugundua kw nini watoto wanafeli, ikashirikisha wadau wa elimu wakatoa maoni yao, waalimu wa shule za secondar wakaapewa mitihani wafanye wakafeli Big tyms. Lakini katika kupokea maoni ya wadau walitoa solutions za kupunguza kufeli na kuongeza ufaulu. Wakashauriwa kuboresha mazingira ya kusomea, vitabu,maabara,maslahi ya waalimu. Na pia wakashauriwa kuangalia upya upangaji wa madaaraja ya ufaulu.

Ikumbukwa wizara ina mandate ya kupanga gredi za ufaulu km jinsi ambavyo ilikuwa imezipanga zilizokuwepo. Kama wizara imeona kushusha A ianzie 81 na B ianzia 50 itasabbisha pawe na ufaulu mkubwa basi wana hoja kabisa. Kw sababu nia yao ni kuongeza ufaulu. Sisi kama watz tunachoweza kuquestion ni jinsi hii logic ilivyo, jee inasound?

Watu wanaponda kuitwa div 0 mpk dv V, naona ni sawa hivi kuna logic gan mtu kafanya mtihan na kapata 18 F katika mitihan yote alafu unasema kapata ziro? Hii haina mantic na haina maana. Na pia hakuna maana kuwepo kw dvs 1 mpaka iv then nyingine unaiita ziro it absurd.

Nakubaliana na ukweli kuwa mtihan wa mwisho uwe 60 percent. Huwezi kusoma miaka minne the unakuja kujaribiwa kwa mtihan wa masaa matatu na hapohapo tunatoa rulling kuwa wewe ndie una akili nakubaliana na continuous assesment.

Watanzania tujifunze kukubaliana na mabadiliko. Na hata kama ni mabadiliko yamefanyw with political influence sioni tatizo coz politic ndio injini ya sera zote unazoziona.
 
Prof Mchome, Prof Bhalalusesa na boss wao Dr Shukuru Kawambwa ni majanga makubwa ya taifa na ni sumu kubwa ya maendeleo kwa nchi hii
 
Prof Mchome, Prof Bhalalusesa na boss wao Dr Shukuru Kawambwa ni majanga makubwa ya taifa na ni sumu kubwa ya maendeleo kwa nchi hii
Bhalalusesa ni mtaalamu wa elimu. Amebobea kwenye fani. Kawambwa na Mchome ndio majanga.
 
Sasa hivi Bhalalusesa amekuwa kidampa cha wanasiasa yeye ndiye aliyekuwa anaongoza vikao vya kushawishi watu kukubali upuuzi walioutangaza na Prof Mchome na alikuwa anatetea sana hasa suala la kuwapa wanafunzi. alama 40 za CA bila kufanya standardization ni yeye aliyelikomalia.

Alipata wakati mgumu sana kwenye baadhi ya vikao vya wadau alitakiwa aeleze jinsi shule ambazo hazina walimu kwenye baadhi ya masomo watakavyopata alama za CA akasema hilo litafanyiwa kazi baadae kwa kuwa serikali inatambua uhaba mkubwa wa walimu. Kama Bhalalusesa ni mtaalamu wa elimu ameuacha chuo kikuu tangu aende wizarani ni siasa tupu alipofika kitu cha kwanza alichofanya ni kupendekeza kushushwa kwa alama za kujiunga na Kidato cha I kuwa 28% badala ya 40%

Wote ni MAJANGA MAJANGA na sasa elimu ya Tanzania itaendelea kuwa Majanga
 
Sijui ni kwa nini wizara ya elimu Ina bahati mbaya kiasi hiki. Ilikuwa Enzi ya Mungai, akiamua kuharibu elimu kana kwamba ni biashara binafsi. Sasa tuna timu mpya, akina Kawambwa, Mulugo na Mchome wao.

Huyu Mchome Hana tofauti na Mungai. Nahisi amepata nafasi hiyo bila kutegemea na anajaribu kuonyesha kwamba kichwa kiko safi. Siamini!

Wozara ya elimu ni zaidi ya Mchome na kufikiri kwake. Ilistahili atulie na kuwahusisha wadau badala ya kuita wanahabari na kit angalia div.5. Ha kuifanya hivyo na ndo maana wengi tunaona ni mtu mwenye vituko na binafsi namuona Hana tofauti na Mungai.

Najiuliza, ni nani anawatuhusu watu Kama Mchome kuchezea elimu yetu? Je, sera au mipango inapangwa n mtu mmoja ndani ya wizara?

Huyu Mchome asipoangaliwa kwa makini, anaiharibu tena elimu yetu kwa Mara ya pili.

Mkuu kinachokushangaza hapa ni nini?kwa taarifa yako kama mtu aliweza kujifungia kwenye kajichumba na wanakamati wenzake na kufanya mazingaombwe yaliyowezesha wanafunzi waliofeli kufaulu bila kurudia mtihani...unatarjia atafanya nini...hizi tunazolalamika sasa ni rasharasha subiri za masika hii kitaalamu inaitwa BIG RESULTS NOW
 
Alichofanya Mchome na Bhalalusesa kutangaza huo UPUUZI inaonesha jinsi gani kuwa na elimu kubwa haina maana kuwa una maarifa na busara ya kupambanua lipi linafaa na lipi halilifai. Ni aibu sana kwa taifa. Naona Mungai ni afadhali kuliko Mchome, ukiangalia Maprofesa ndiyo wanaleta sera za kufikirika ni aibu sana kwao na wanwadhalilisha sana maprofesa wa nchi hii
 
Back
Top Bottom