Mchezo huu mlikuwa mkiuitaje?

Hahahaaaa, mie mara zote nilikuwa nakuwa "tandiboi"
 
Hii picha imenikumbusha mbali aiseee daaa,jana katika pitapita zangu niliona watoto wanacheza huu mchezo,zamani kule kwetu tulikuwa tukiita "bleki nyau"sababu kulikuwa na basi maarufu sana likiitwa"black nyau"kipindi hicho lazima niwe dereva, hadi msosi unashau...
 
Duh! Umenikumbusha mbali sana. Mchezo ni mzuri shida yake ni kama huna mbio lazima utaburuzwa
 
Hahahaaaa, mie mara zote nilikuwa nakuwa "tandiboi"
Baba V hiyo terminology uliyoitumuia imenikumbusha mbali sana, enzi za mabasi ya keria....
Kulikuwa na mijitu na nguvu, inabeba magunia mawili na kupanda nayo juu kwenye keria
 
Last edited by a moderator:
...kalikuwa kamchezo kazuri sana, nilikacheza aisee...siku hizi watoto hawana kabisa mambo haya jamani!
 
ilikua mkifika kwenye kona mnanepa kabisa, dereva ndo' anapotafutia sifa utasikia jiiiiimmmm.... jiiiimmmmmm.... vuuuuu............ ziiiiiiiiiii......!!

hahahahaaaa! Mkuu we acha tu, unakuta dereva analala upande huku akinyonga mikono kama kashika usukani wa fiat Mbaula!
 
Tulikua tukiuita kigali gali. Haui dereva mpaka uwe mtemi (sio milambo)
 
ilikua mkifika kwenye kona mnanepa kabisa, dereva ndo' anapotafutia sifa utasikia jiiiiimmmm.... jiiiimmmmmm.... vuuuuu............ ziiiiiiiiiii......!!

Hahahaha wewe ulikua sana sana ni dereva eeeeh...
 
Bus..... kuna kipindi zile honi za vuvuzela za kuimba ''honi ya kwanza ya pili nipo morogoro'' au ''Fungua geti fungua geti msela anapita'' ndio mchezo ukawa unaishia zake hii michezo hadi ukimkuta mtu mbele unampigia horn

jamiif hii michezo bado ipo sana mbona hii mikitu ni kama urithi wa Dunia haiwezi potea nilikuta watoto wanacheza ukuti nikashngaa wamejuaje!!! ila sijasikia wakicheza ''Maji ndimu sagagaa funika funua'' na ile kitu niliyokuwa siipendi ''Mbata'' unainamisha kichwa mtu anakupiga then unakisia ni nani aliyekupiga kuna watu walikuwa wanakupiga haswa chini ya Kisogo
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…