Mchepuko unakaribia kuvunja ndoa yangu

BILGERT

JF-Expert Member
Feb 27, 2015
6,535
10,974
Michepuko mna nini lakin?

Wakuu ninaandika kwa masikitiko na majonzi makubwa saana. Nimeoa takribani miezi Tisa sasa. Kama mjuavyo kwetu sisi wanaume hatuachi kuchepuka ikiwa ndo asili na hulka yetu.

Namshukuru Mungu,nimebahatika kupata mwanamke mzuri, mwenye upendo na pia Ni mcha Mungu. Tatizo ni huyu mchepuko niliye naye,anani control mnooo. Yaani ananifanyia visa sijapata kuona.

Inafikia nyakati Mke wangu simjali Wala kumheshimu tena, najikuta nguvu zote nazielekeza kwa mchepuko. Na mbaya zaidi mchepuko ananipeleka vile anavyo jisikia, namfanyia mambo mengi kuliko hata ninayo yafanya kwenye familia yangu

Lakini naambulia matokeo hasi kutoka kwa huyo mchepuko. Mchepuko anaweza kunihitaj hata saa tano usiku,ntajikuta nmedanganya kwa wife ili tu niweze kutoka

Kuna nyakati mchepuko atanifanyia vitimbi na vibweka kiasi kwamba napoteza kabisa mood ya kazi. Nkirudi nyumbani, mke wangu namdanganya then atanifariji na kunitia nguvu na maisha yanaendelea.

Imefikia hatua nataka niachane kabisa na mchepuko, nashindwa kabisa yaan nitampotezea Leo lakini kesho ntamtafuta Tena Bila kujali madhila anayo nifanyia.

Nimechoshwa na hii hali wakuu,natamani kujinasua katika hii Hali ninayo pitia. Nahitaji kujikita kwenye familia yangu. Kinacho niumiza zaidi naweza kukaa hata wiki sijapiga game nyumbani, ila nataka kupiga tu game na mchepuko.

Mke wangu anakuwa mnyonge mnoo. Najutia saana kuwa na mchepuko, najitahid kutafuta njia nzuri ya kutoka na hatimaye kuacha kabisa.

Ushauri wangu kwa vijana wenzangu ambao mmeoa. Kama unaweza please tulia na mke wako ili usipitie hali ambayo naipitia.

NB: Mke wangu ni mzuri na ametimia kila idara kuliko hata mchepuko.

Cc Extrovert
 
Stick na mke wako kenge ww. Kwenye statement yako unasema kuwa mke wako ni mke mzuri mcha Mungu.

Stick na huyo mcha Mungu. Mchepuko una nguvu sababu umeshakuwa addicted. Achana na mchepuko save ndoa yako.
Ukiendekeza tamaa hata hiyo ndoa utaikosa
 
Mwanaume wa kweli wala hawezi kuja kuomba kusikia juu ya hili toka kwa watu wengine

Acha utoto na uwe MWANAUME,unashindwa kumuacha mwanamke hawara na una mke mzuri zaidi ya huyo hawara,sasa maamuzi ya kiume kwako ni yapi?utakua umerogwa

Hakuna namna ya kukufundisha zaidi ya kumwambia sasa yatosha,una mke wako na umeona haifai tena atafute njia nyingine ,kisha unablock namba zake.

We unahisi atakufanya nini mpaka uogope,muendekeze utakujaga kujuta na kuturudia tena humu then ushauliwe ujinga uharibu maisha ya familia yako
 
Acha dhambi ya kumsingizia mchepuko wewe ndie unaevunja ndoa yako mwenyewe pumbavu kabisa hivi unaruhusu vipi mchepuko aivuruge ndoa yako?

Nilijua labda pengine mke wako ndie chanzo (mkorofi)cha Wewe kwenda kutafuta mchepuko huko nje.kumbe maskini ya Mungu mkeo anakupenda,mrembo na mcha Mungu.

Upewe nini sasa?au wacha Mungu hawanaga style za kiwendawazimu wanaihofia biblia eee si nakuuliza we mtu!!!

Shame on you mwamba.
 
Kwanza hebu tueleze ni kitu gani anachokupa mchepuko ambacho mke wako hakupatii?? Then kama mke wako pia anakupatia kwanini unashindwa kustick na mke wako?!
Nyie ndio mnaotutia aibu wanaume na mwisho wa siku tunaonekana wanaume wote tunapenda kuchepuka na hatuwezi kutulia na wake zetu endapo kama tukioa.

Amua moja basi kubaki na freezer au kuchukua deli la ice cream
 
Siku huyo mke anayekuheshimu akikugundua ataacha kujali na utakosa amani siku zote za ndoa, na ukifika uzeeni utelekezwe, mtu akikuheshimu na wewe jiheshimu, acha kujiendekeza na wewe anakuvumilia tena wewe sio kama ex wake so be careful
 
Niliwahi kuwa na mwanamke nikawa nawambia wenzangu kuwa najiona kabisa nikiwa nimekumbatia bomu ambalo linakaribia kulipuka lakini kulitupa siwezi.

Ila nilikuja kulitupa baada ya muda sana. Mkuu hakuna namna litupe usije kulipuka nalo
 
Brother umelogwa,mwambie ukweli mshenga wako akutoe kwenye hilo tatizo. Mwambie ukweli mshenga nina uhakika atakupa ushauri mzuri na huyo mchepuko anza kupunguza naye mazoea..mblock mazima.
Omba ruhusa ya ofisin likizo fupi nenda na wife vacation hata wiki mbili...tumia hiyo likizo kusali,kutubu.

Kwanini nakushauri hivi...huyo mkeo lazima atajua iwapo hutoachana na mchepuko then atabadilika Ogopa sana mwanamke akibadilika ni zaidi ya vampire. Mwanamke ana roho mbaya akiamua kukukomoa utajinyonga. So unayo nafasi ya kuachana na uhuni ukatulia na Ndoa yako kabla mambo hayajabadilika.


Ndoa ni institution
 
Tafuta mchepuko unaye mmudu kiutawala
8c62c08adecd4f7fa497481bf276d78a.jpg
 
Back
Top Bottom