GE2025 Mchengerwa: Bilioni 23.5 zitajenga vituo vipya vya afya nchini

GE2025 Mchengerwa: Bilioni 23.5 zitajenga vituo vipya vya afya nchini

Matukio, Taarifa, Habari na Mijadala ya Wananchi WAKATI wa Mchakato wa Uchaguzi Mkuu 2025

Mkalukungone Mwamba

JF-Expert Member
Joined
Aug 29, 2022
Posts
2,437
Reaction score
5,235
Waziri wa Nchi, Ofisi ya Rais- Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa (TAMISEMI), Mohamed Mchengerwa, amesema kuwa serikali imetenga kiasi cha Shilingi bilioni 23.5 kwa ajili ya ujenzi wa vituo vipya vya afya katika majimbo mbalimbali nchini, ikiwa ni sehemu ya utekelezaji wa awamu ya pili ya mpango huo.

Mchengerwa ametoa taarifa hiyo, Jumamosi Julai 12, 2025, jijini Dodoma, wakati wa Mkutano wa Mwaka wa Waganga Wakuu wa Mikoa na Halmashauri kwa mwaka 2025, wenye kaulimbiu isemayo: “Wajibu wa Waganga Wakuu wa Mikoa na Halmashauri katika Kuimarisha Ubora wa Huduma za Afya kuelekea Bima ya Afya kwa Wote.”

Aidha, Waziri Mchengerwa amesema kuwa Serikali pia imetoa Shilingi bilioni 17.36 kwa ajili ya kukamilisha maboma ya zahanati 346 ambayo yalikuwa yameanzishwa na wananchi katika maeneo mbalimbali lakini hayajakamilika.
 
Na mtoe leseni Kwa vijana walio maliza elimu ya udaktari waweze kujifungulia vituo vya afya Ili kufanyia kazi taaluma walio somea c muwarundike uko mahosoitalin na mishahara ya kukadiriana ingali Kuna vijana wanaweza kuungana na kufungua kituo Cha afya na nyie km serikali mkawasimamia na kuwapa pia mikopo ya bei nafuu...hii itawaponguzia pia serikali mizigo ya Kila mwaka kuimbaa kujenga vituo vya afya.....
 
Back
Top Bottom