PreGE2025 Mchengerwa achukua fomu ya ubunge jimbo la Rufiji

PreGE2025 Mchengerwa achukua fomu ya ubunge jimbo la Rufiji

Mijadala ya Uchaguzi Mkuu wa Tanzania 2025 (Kabla)

DuaZaMama

JF-Expert Member
Joined
Jun 2, 2025
Posts
1,882
Reaction score
4,129
Waziri wa Nchi Ofisi ya Rais- TAMISEMI na aliyekuwa Mbunge wa Rufiji Mhe. Mohamed Mchengerwa leo Juni 30, 2025 amejitokeza kuomba ridhaa ya Chama cha Mapinduzi (CCM) kuchaguliwa kuwa mgombea ubunge la Rufiji katika Uchaguzi Mkuu wa Mwezi Oktoba mwaka huu.

Mhe. Mchengerwa amefika kwenye ofisi ya Wilaya ya Chama Cha Mapinduzi (CCM) Rufiji katika Mji wa Utete na kukabidhiwa fomu ya kuomba ridhaa kutoka kwa Katibu wa CCM Wilaya ya Rufiji na baada ya kukamilisha taratibu zote akairejesha.

Mhe. Mchengerwa aliambatana na mama yake mzazi, ambapo baada ya kuwasilisha fomu asema ameamua kutumia haki ya kuchagua na kuchaguliwa ili aendelee kuwaletea maendeleo wananchi wa Rufiji.
1751282808296.png
 
Back
Top Bottom