Asee. Apumzike kwa amani. Kwa wakati wao kama KAOLE SANAA GROUP ! walitupa burudani kwa hakika , siyo maigizo au sinema za wakati huu ni mambo ya mapenzi tu
Mzee Yusufu Kaimu mchekeshaji mkongwe maarufu kama Pembe afariki dunia alasiri ya leo jijini Dar es Salaam. Taarifa zimethibitishwa na Msanii wa Filamu, Vincent Kigosi “Ray” na taratibu za mazishi zinafuat,pole kwa ndugu jamaa na marafiki wote
TANZIA Mchekeshaji mkongwe Tanzania Mzee Yusuph Kaimu maarufu kwa jina la Pembe amefariki dunia muda wa alasiri ya leo Oktoba 20, 2024.
Taarifa ya kifo chake imethibitishwa na baadhi ya wachekeshaji wenzie na wasanii wa filamu aliowahi kufanya nao kazi enzi za uhai wake na taratibu za mazishi zinafuata.