Mchawi wa TRA ni wafanyakazi wake | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Mchawi wa TRA ni wafanyakazi wake

Discussion in 'Habari na Hoja mchanganyiko' started by Pdidy, Oct 13, 2008.

 1. Pdidy

  Pdidy JF-Expert Member

  #1
  Oct 13, 2008
  Joined: Nov 22, 2007
  Messages: 33,585
  Likes Received: 5,771
  Trophy Points: 280
  Mchawi wa TRA ni wafanyakazi wake
  WIKI iliyopita Mamlaka ya Mapato Tanzania (TRA), ilitoa taarifa ya kufafanua sababu zilizosababisha kushuka kwa makusanyo ya kodi kwa mwezi.

  Taarifa hiyo ilieleza kwa undani kwamba sababu kubwa ya kushuka kwa mapato ni wafanyabiashara wasiokuwa waaminifu kukwepa kulipa kodi, hususan katika sekta ya mafuta.

  Ilieleza kwamba tatizo hilo walishalizungumza na serikali kupitia kwa Naibu Waziri wa Fedha na Uchumi, Jeremia Sumari aliyetembelea mamlaka hiyo hivi karibuni.

  TRA ikaeleza kwamba pamoja na kushuka mapato hayo, imeendelea kupata mafanikio makubwa ya kuweza kupandisha kiwango cha makusanyo yake kwa mwezi kutoka sh bilioni 25 mwaka 1995 hadi kufikia Sh300 bilioni kwa mwezi hivi sasa.

  Kwa hakika, taarifa hiyo ilishangaza sana kwa sababu, TRA haiwezi kutoa utetezi mwepesi kama huo wa kushuka mapato yake, kwa sababu kama inafanya kazi zake kikamilifu mwanya wa mfanyabiashara kukwepa kodi kiasi cha kudhoofisha mapato utatoka wapi?

  TRA ambayo ni roho ya uchumi wa nchi ina wafanyakazi wengi watalaaam na ina vitengo vingi vinavyoshughulikia kudhibiti watu wanaokwepa kulipa kodi.

  Moja ya vitengo hivyo ni Kitengo Maalum cha Kuzuia Magendo (FAST), ambacho ndiyo kinachofuatilia kuhakikisha kuwa bidhaa zinazoingizwa na kuchukuliwa na wateja bandarini vimefuata taratibu za kulipiwa ushuru na kuhakikisha kuwa mianya yote ya watu kukwepa kulipa kodi inazibwa.

  Kwa ujumla kitengo hiki na kile cha uchunguzi (Investigation Bureau) vina wafanyakazi wa kutosha wanaolipwa mishahara minono kwa ajili ya kazi hiyo, hivyo inashangaza tunaposikia kwamba TRA inalia kwamba mapato yameshuka kutokana na watu kukwepa kulipa ushuru wa forodha.

  Tatizo kubwa linaloisumbua TRA ni kwamba baadhi ya wafanyakazi wake wameigeuza mamlaka hiyo kuwa shamba lao la kujipatia utajiri.

  Kwa mfano, baadhi ya maafisa katika vitengo vya Fast sasa wamegeuka kuwa miungu watu ambao wanaweza kumkamata mteja aliyeingiza bidhaa kwa kufuata taratibu zote zinazotakiwa, ili kutengeneza mazingira ya kupewa rushwa.

  Mazingira haya ya kulazimishwa kutoa rushwa hata kama mtu amelipa mizigo yake vizuri ndiyo yamebadilisha mwelekeo na kuifanya TRA kupoteza mapato mengi, kwa sababu wafanyabiashara wengi wanalazimika kutafuta njia za mkato kuingiza bidhaa zao. Wanajua kwamba hata kama watatumia njia sahihi mwisho wa safari mizigo yao itakamatwa na kudaiwa rushwam ndiyo maana wanaona heri wakutane nao wakiwa wameshakwepa kulipa ushuru ili mmalizane.

  Sio jambo la siri kwamba leo maeneo ya Bagamoyo, Muhoro Rufiji, Pangani mkoani Tanga, yamegeuzwa kuwa bandari bubu zinazotumika kuingiza bidhaa mbalimbali kutoka nje bila ya ushuru kuingia TRA.

  Ina maana TRA haina taarifa na watu hawa? Ni wazi kwamba wanajua, lakini baadhi ya watumishi wake wamegeuza maeneo hayo kuwa miradi yao ya kujipatia fedha au wanaendeleza falsafa ya watanzania wengi ya mbuzi hula kulingana na urefu wa kamba yake.

  Hata hili suala la wafanyabiashra wa mafuta kukwepa kulipa ushuru nalo lipo wazi kwamba baadhi ya maafisa wa TRA wakiwamo wa vitengo hivi vya Fast na IB, wanajua magari ya mafuta yanayokwenda nchi jirani yanashusha katika vituo gani vya mafuta vilivyopo jijini Dar es Salaam na mikoani.

  Ni wazi kwamba TRA yenyewe ndiyo imetegeneza mazingira ya wafanyabiashra kukwepa kulipa kodi na mapato makubwa yanaishia katika mifuko ya baadhi ya wafanyakazi wake.

  Tunajua kamba wapo baadhi ya wafanyabiashara nchini wanaotaka kujipatia utajiri wa haraka kwa kukwepa kulipa kodi hususan ushuru wa forodha, lakini kama wafanyakazi wa Fast na IB wangetanguliza mbele maslahi ya chini hakuna mfanyabiashara ambaye angekwepa kulipa kodi.

  Kwa mwendo huu tusipokuwa makini mapato yetu yatazidi kupotea kwa wateja wetu kuikimbia bandari yetu. Mfano mzuri ni wa nchi kama Namibia ambayo hivi sasa imeweka mkakati wa kuwateka wateja wao kwa kuondoa urasimu katika badari yao na sasa inakusudia kuhudumi mizigo ya nchi wanachama wa Jumuia ya Uchumi wa Nchi za Kusini mwa Afrika (SADC) ifikapo mwaka 2015.

  Bila ya kuisafisha TRA, uchumi wa nchi yetu hauwezi kuendelea na tutaendelea kupiga kelele kila siku kwamba wafanyabiashara wanakwepa kulipa kod, wakati mbaya wetu ni watu wachache waliopo ndani ya mamlaka hii.

  Mwandishi wa safu hii anapatikana kupitia baruapepe; juliusmagodi@yahoo.com

  Simu; 0754 304336
   
 2. P

  PauliMasao JF-Expert Member

  #2
  Oct 14, 2008
  Joined: Nov 26, 2007
  Messages: 286
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 33
  Asilimia kubwa ya wafanyikazi wa TRA ni corrupt na sijawahi kusikia au kusoma mahali popote kuwa mfanyakazi wa TRA ameshikwa na TAKUKURU. Ukienda kwenye ofisi za TRA kila Mkoa utakuta karibu kila mfanyakazi ana gari na kila mmoja wao ana nyumba moja au mbili. Ni kiwango kipi cha mshahara TRA mfanyakazi unaweza kujenga nyumba na kununua gari kwa muda mfupi wa kufanya kazi? Ninavyjua mimi, mishahara ya wafanyakazi kwenye nchi zilizoendelea ni mikubwa lakini utakuta asilimia 100 ya wafanyakazi walioajiriwa wanaishi kwenye nyumba za kupangisha kwa kuwa ni impossible kujenga nyumba kama wewe siyo celebrity. Kwa nini hawa TAKUKURU wamekuwa wakiwafumbia macho wafanyakazi wa TRA? Uchumi wetu unategemea sana TRA safi na siyo walaghai. TAKUKURU get off your butts!
   
 3. Bowbow

  Bowbow JF-Expert Member

  #3
  Oct 14, 2008
  Joined: Oct 20, 2007
  Messages: 545
  Likes Received: 4
  Trophy Points: 0
  Wasi wasi wangu ni hela za EPA zimerudishwa kwa kutumia mapato yetu halali huku wakisingizia mafisadi wamerudisha.

  Subiri mwisho wa mwezi huuu (October Surprise) jinsi mafisadi walivyorudisha hela wakati tuliambiwa nyingi zipo nje ya nchi.
   
Loading...