Mchawi wa Bongo Movie ni Wanabongo Movie Wenyewe

figganigga

JF-Expert Member
Oct 17, 2010
25,720
55,859
Bongo movie nadhani mnajifanya hamjui mchawi wenu ni nyinyi wenyewe na hamjiulizi kwanini siku hizi bongo fleva inafunika nyimbo za magharibi maeneo ya starehe na kitaa kijumla.
Mbali na hayo tukubaliane yafuatayo ili mimi niache kabisa kuangalia movie za nje;

1.Muwe mnatunga stori zenye kuakisi matatizo na mambo yanayotokea katika jamii sio kila siku stori za tajiri kampenda maskini.

2.Muache habari za kutuonesha maaskari wanavaa ki-modal,wana wave,wana timber akati kitaa tunakutana na askari wanaovaa suruali zina celebrations na hawana habari kuna kitu kinaitwa wave

3. Muache habari ya kutuaminisha kila mlinzi ni comedian akati kitaa tunakutana na walinzi makauzu kiasi kwamba kama ulikuwa unamuulizia Zahoro unaweza jikuta unajitambulisha ni "shoe shiner"

4.Mazungumzo kama ngonjera sitaki pia,eti mtu mmoja anaongea anasubiriwa amalize ndo mwingine aongee,aisee hamnaga mazungumzo ya hivo zaidi ya kitabuni

5. Habari ya stori za binti wa kitajiri kumpenda houseboy au mwanaume choka mbaya tena kwa binti kulazimisha penzi ni fiksi mchana kweupe. Hao waigizaji wa kike wenyewe maisha halisi wana mahusiano na watu wenye uwezo mkubwa.

6. Muache habari ya kuhadaa watafutaji kwa kuonesha mfanyakazi wa kawaida tu anamiliki magari na jumba la kifahari.

7.Sijasahau habari ya mama mweusi tii baba mweusi tii hafu wana mtoto shombe shombe,siwaelewagi mjue.

8. Hafu zile huruma za kwenye movie zenu hazipo kitaa,zile huruma za mtu kulazimisha kumsaidia mwingine kisa walisoma pamoja huku anayetakiwa kusaidiwa hamkumbuki mtoa msaada na anaanza kwa kukataa hapana aisee

9. Muache habari ya kutuletea "flashback" ya miaka ya 90 au 2000 hafu tunaona wahusika wanaendesha IST na wana Iphone

10. Muache habari ya kutengeneza stori za maisha ya kichifu hafu wahusika wanaongea Kiswahili cha Daslam akati inajulikana tawala za kichifu lugha iliyokuwa inatumika ni ya kabila la eneo husika.

Mkishindwa hayo niache niendelee kuangalia movie za kina Komandoo Kipensi japo kiingereza hakipandi ila naelewa vitendo tu na nakusimulia movie mwanzo mwisho.
dbc31bcae3d6a818967245ad40ab2dc9.jpg

Jambazi wa Bongo Movie akiwa amevua viatu
 

Similar Discussions

Back
Top Bottom