Mchapalo maalumu ulioandaliwa kwa ajili Mawaziri wa Michezo wa Baraza la Michezo la Umoja wa Afrika Kanda ya Nne (AUSC)

Ojuolegbha

JF-Expert Member
Sep 6, 2020
627
413
Waziri wa Utamaduni, Sanaa na Michezo Balozi Dkt. Pindi Chana ameongoza mchapalo maalumu ulioandaliwa kwa ajili Mawaziri wa Michezo wa Baraza la Michezo la Umoja wa Afrika Kanda ya Nne (AUSC) pamoja na Wageni waalikwa kutoka nchi takriban 14 za kanda hiyo ya Afrika ambao wanaodhuria Mkutano wa Baraza la Umoja wa Afrika Kanda ya Nne (AUSC) unaofanyika jijini Arusha kuanzia Mei, 2-4, 2023.

Akizugumza katika mchapalo huo usiku wa Mei 3, 2023 Mhe. Chana amewakaribisha Wageni hao wafurahie kuwepo hapa nchini muda wote watakapokuwa kwenye mkutano huo, na kuwahakikishia kuwa Tanzania ipo tayari kuendesha mikutano ya Umoja wa Baraza hilo, kwakuwa historia ya Tanzania katika Umoja wa Afrika inatambulika kwa Amani, Upendo, Umoja na Mshikamano.

Hafla hiyo imehudhuriwa pia na Naibu Waziri wa Utamaduni, Sanaa na Michezo Mhe. Hamis Mwinjuma, Katibu Mkuu Said Yakubu, wajumbe wa mkutano huo kutoka nchi nane wa nchi za kanda ya nne, Watendaji wa Wizara pamoja na wageni waalikwa.

IMG-20230504-WA0001.jpg
 
0 Reactions
Reply
Back
Top Bottom