Mchango wa Mr.Blu kwenye Bongo Flava

Mtanzania Mkenya

JF-Expert Member
Feb 20, 2016
238
387
Kherry Sameer Rajab a.k.a Mr.Blu ni msanii wa Bongo Flava aliyewahi kuHit miaka ya 2003 na nyimbo yake ya Blue Blue na baadae mapozi akiwa na umri mdogo sana.

Ni msanii ambae ameweza kuMaintain kuwa kwenye chati kwa muda mrefu na hadhi yake pia kimuziki.

Wewe kama shabiki wa Bongo Flava, unahisi Mr.Blu amechangia nini kwenye mziki wa huu?
 
Mr blue yuko wapi mbona haonekani kabisa
Wewe uko wapi? Mbona yeye yupo Tz na bado anatupa mawe, na crew yake Team 20 micharazo wanasumbua sana,
......HAKUNA TENA KELELEEEEEEE.....kimya! Kimya! Shut up! ...hey Mr. Lazyman punguza ku-complain.....

Ila kiukweli, historia itawakumbuka kina Fid Q, J Nature, Mr two, etc zaidi ya huyu jamaa, mchango wake ni wa kawaida tu kwamba nae alikuwapo toka udogoni.
Hata Gwear R.I.P sidhani kama ana nafasi kubwa ktk historia kama wale wa zamani kina Gagwe Mod, Ile crew ya Diplomats nafikiri na wengine kina Inspecta Haruna.
 
Kiukweli mchango wa jamaa ni mdogo sana, hauna hata haja ya kuujadili. But props to him, at some point I was looking up to that negro(stigity-wise), back when I was a shortie. That I can't front.
 
jamaa kapambana na wakongwe ila bado yupo. Nadhani kwa sababu anaeza chana na kuimba pia. Ni kama kinyonga, style yoyote anachana
 
Wewe uko wapi? Mbona yeye yupo Tz na bado anatupa mawe hatari, na crew yake Team 20 micharazo wanasumbua sana,
......HAKUNA TENA KELELEEEEEEE.....kimya! Kimya! Shut up! ...hey Mr. Lazyman punguza ku-complain.....
Mkuuu mimi Nipo arusha sijamsikia cku nyingi au ndo wewe nini! Karibu arusha jombaa.
 
Mr. Blue hana mchango kiviiile kwenye music industry ya Bongo flavour labda ku-inspire watoto wadogo kufanya music coz hit song yake ya Blue Blue ilitoka akiwa na miaka 16
 
ndie msanii ninaemkubali kuliko wote! hajawahi kuniangusha hata akishirikishwa tu kweny nymbo atafunika......ana bonge la mchango
 
Mchango wa Mr. Blue ni mdogo sana, watu wafuatao kwa maoni yangu hawapaswi kusahauliwa kwenye historia ya Bongo fleva. 1. Saleh Jabri, Balozi, Sugu, kwanza unit n.k hili ni kundi LA waanzilishi (late 1980's up to 1990's) 2. Inspector Haroun na Prof J (late 1990's -early 2000's) hawa wawili walitoa mchango mkubwa katika kubadilisha mtazamo wa watu dhidi ya bongo fleva, wimbo wa Inspector mtoto wa geti Kali uliwafanya mabraza men na wanawake wengi waanze kuupenda mziki wa kizazi kipya, nikumbushe tu hakuna wimbo wa bongo flavour uliokaa kwenye chati kwa muda mrefu katika radio mbali mbali kama huu. Prof. J akijulikana kama Nigger J enzi hizo na kundi lake hard blasters na wimbo wao Mola nitoe roho ulileta mapinduzi katika ujumbe wa mziki. 3. MB doggy(Mid 2000's) Huyu alileta msisimo mkubwa na nyimbo yake ya Latifa, naweza kusema huyu ndie baba wa "wabana pua". Baada ya mafanikio makubwa ya Mb doggy taratibu mziki wa kufoka foka ukaanza kumezwa na wale wa kuimba, waimbaji wengi kama matonya, voice wonder n.k wakaibuka. kwa mtazamo wangu hao ndio watu wenye mchango mkubwa katika transformation ya bongo flavour.
n.b mods mnaweza kuanzishia Uzi mchango huu kama mtaona yafaa.
 
Waandishi wa habari wanataka habari mi sina habari niko beach napunga upepo wa baharii....
 
Back
Top Bottom