Hivi ni kwa nioi waandishi wa habari wanadharauliwa kiasi hki? Hao waandishi wanaowasikiliza vichaa kama hawa huwa wanauliza na maswali magumu pia?
Cc:
Pasco
Mkuu Matola, kwanza asante kuzungumzia jinsi waandishi wanavyodharauliwa kiasi hiki!, kazi ya uandishi ni noble profession kama noble professions nyingine zote, ni kazi ya wito na ni kujitolea kama ualimu, udaktari na kazi za kanisa!, waandishi ni watumishi wa watu wakifanya kazi ya kutumikia jamii, ila kwa upande mwingine, katika jukumu lao la kukusanya habari, watu wote wanakuwa ni abiria wao, huwezi kuchagua!, wazima, vichaa, lunatics, etc, wote kwetu ni source.
Ukiisha kusanya, wewe mkusanyaji ndio chujio la kwanza kupima if it makes any sense, ndipo unaandika kuhabarisha jamii!, unamkabidhi mhariri wako nae anaipitia na kuiaproove itoke au isitoke, au kuipunguza, kuichinja na hata kuipotezea!.
Mfano habari hii kwenye magazeti ya kesho, itakuwa ni big news kwenye magazeti ya Uhuru, Mzalendo,itakandiwa sana Tanzania Daima, ila kwenye magazeti kama Citizen na Mwananchi sijui kama inaweza kupita kwa sababu wahariri wataweza kunote insanity ya mtuoa habari, ambayo ameyazungumzia matukio bila coherence wala correlation, na Tanzania ingekuwa ni nchi inayofuata utawala wa sheria "the rule of law", saa hizi jamaa ni zamani, angelikuwa ananye. debe!.
Kwenye noble profession zote kudharaulika ni kawaida sana, hata kwenye fani ya udaktari, Madaktari ndio wanaoheshimika, lakini manesi wale wafunga vidonda etc, wee acha tuu!, kwenye fani ya uandishi, madakitari wetu ndio wahariri, hawa wanaheshikika sana, ila sisi ndio wafunga vidonda wao, kudharaurika ni kawaida!.
Ila nasi tunao msimu wa kuheshimika na kunyenyekewa kama walivyo waalimu kipindi cha mitihani,hivyo nasi mwaka 2015, kuelekea kile kipindi, huwa tunaheshimiwa sana, tunathaminiwa sana, tuna nyenyekewa sana, na kwa wengine wetu, ndio kipindi cha mavuno!.
Thanks.
Pasco.