Mchange awa gumzo Ubunge Kibaha mjini

Mchange awa gumzo Ubunge Kibaha mjini

Joined
Nov 10, 2014
Posts
48
Reaction score
19
Sera zake zakubalika kwa Vijana na Wakina Mama.

Mgombea Ubunge ambaye alikuwa mshindi wa pili katikauchaguzi wa Ubunge Kibaha mjini ameteka siasa za jimbo la kibaha mjini na kuwagumzo katika mji huo baada ya kuonekana katika shughuli mbalimbali za kijamiijimboni humo.
Habibu Mchange mwanasiasa aliyetokea kupendwa na wakazi waKibaha kutokana na sera zake ambazo zimekua zikilenga kuwawezesha wanyongendani ya jamii,ameonekana katika matukio matatu tofauti mwezi huu na kuibuahofu kwa wapinzani wake kuwa huenda ameanza harakati za kuja kugombea ubunge wakibaha mjini.

Katika tukio mojawapo lililofanyika Picha ya Ndege ambalolililenga kukusanya fedha kwa ajili ya ununuzi wa vifaa vya michezo kwa kikundicha vijana, Mchange alipokelewa kwa shangwe na vijana huku wakishangilia "Mbunge""Mbunge" ingawa Mchange alipoulizwakuhusu tukio hilo alijibu kwa kifupi kuwa "Muda utasema" akimaanisha muda ndioutakaoamua kama atagombea ubunge au la.

Endapo atagombea Mchange ana nafasi kubwa ya kushindakutokana na kukubalika katika siasa za Kibaha mjini hasa miongoni mwa wakina Mamana Vijana ambao wamekuwa wakimuunga mkono toka agombee Ubunge

2010.
attachment.php
 
Attachments

  • mchange.jpg
    mchange.jpg
    408.6 KB · Views: 3,413
  • hab.jpg
    hab.jpg
    50.6 KB · Views: 626
Muda wa siasa za ujanja uongo na uzushi umeshapita, Tunahitaji viongozi na si wanasiasa wasaka tonge. Mchange hawezi kuwa Mbunge Kibaha
 
Mchange Kibaha wanahasira nae sana baada ya kupokea mil200 na kuuza jimbo, kama sasa anafika kibaha nampongeza sana siku za nyuma alikuwa hathubutu maana walikuwa wanataka kumpa kichapo
 
Sina hakika unamzungumzia Mchange yupi, kama ni yule aliyekuwa Chadema,ambaye siku mmoja nilimuona star tv akifanya mahojiano akiwa pamoja na Mnyika nadiriki kusema unafanya utani!,, Ubunge!! bado sana
 
Mchange alifungua kesi ya kupinga kikiukwa kwa taratibu za uchaguzi Ndani ya Jimbo la kibaha chadema wakashindwa kumuwekea dhamana ya 15m mahakamani.
Chadema wakasababisha Mchange ashindwe kesi.
Waliouza kibaha ni chadema maana aliyeshinda ni mchaga mwenzao anaitwa Koka anatoka kijiji kimoja na ndesamburo na nyumba za wakazi wa Komu na Koka zinatazamana huko kijijini kwao.
 
ACT Wasaliti mnalo mwaka huu.Hicho kikundi chenu hakiwezi kupata mbunge zaidi ya mmoja. Kwa Hali ilivyo Ayatullah tu ndiyo ataingia bungeni. Mnaweza mkapata madiwani wawili au watatu kigoma Mjini lakini kwingineko msahau kabisa.
 
Mchange Mungu ndiye atampeleka bungeni kwa kupitia kura ya wanakibaha,nitashangaa kama kibaha nao wanamuacha kijana wao wanashabia chama cha biashara saccos
 
mchange huyu niliyesikia anagombea ubunge kuptia act kwa lengo la kuivuruga chadema na si kupata ubunge au mwingne mana kwa kibaha mji ni chadema ukawa ndo unaosikika
 
Mchange huyu anayema uongo mbele ya uma! Huyu ni mwongo sana na ni mnafki kupita kiasi, Anadiriki kuudanganya uma kwamba alikua anapanga mauaji na Chadema wakati alipokua mwanachama wa Chama hicho. Watu wajanja wajanja wa mtaani hawatakiwi kwenye uongozi! Huyu ni mchumia tumbo tunamjua hawezi kua mtetezi wa wananchi.Kwanza alishawahi kumkosea Mungu sana kusema Uongo kua alikua akipanga mauaji na viongozi wa Chadema na ndio maana hata polisi hawakutaka kupoteza muda kuchunguza kaulizake.
 
Uko sawa kaka . viongozi waongo na wasaliti hawana nia ya dhati kutuletea ukombozi . he is a reject
 
Na ile GPA yake ya 1.2 ya UDOM inaweza kumfanya Mbunge???
 
Back
Top Bottom