Mchanganuo wa uimara kati ya tofali za kuchoma na tofali za saruji

Shukrani Mkuu.
Kama uko Dar es Salaam, nenda pale Mwenge kuna ofisi ya NHC wana wataalamu wa ujenzi , watakupa taarifa nzuri. Pia unaweza kwenda UDSM, ARU, DIT wana architects wenye uelewa wa udongo na masuala ya ujenzi kwa ujumla.
 
Nenda Kwa wataalamu wa udongo vyuo vya Ujenzi,au Kilimo au wataalamu wa barabara wanajua ubora na uimara wa udongo sehemu husika
Hivi hawa Wataalamu hujificha wapi, ni mpaka watafutwe?.

Hivi wakitoka kwenye vyombo vya habari au kwa vipeperushi kuelimisha Watu ni kosa?, maana kuna Watu wengi tu mitaani wanafyatua matofali ya kuchoma na tunanunua na kuyatumia bila ufahamu wowote wa ziada.
 
Hakuna anayeongelea tofali za udongo zilizoshindiliwa (interlocking compressed earth blocks)
tofali 2.png
 
Natamani kujua zaidi kuhusu hizi interlockings, zimetokea kunishawishi kiaina.
Hizi ni tofali za udongo (ila sio kila aina ya udongo utakupa matokeo chanya), huweza pia kuchanganywa na cement kidogo (stablizng)...na kubonyezwa/kigandamizwa kisawasawa kwa mashine ya mkono au umeme.
 
Hizi ni tofali za udongo (ila sio kila aina ya udongo utakupa matokeo chanya), huweza pia kuchanganywa na cement kidogo (stablizng)...na kubonyezwa/kigandamizwa kisawasawa kwa mashine ya mkono au umeme.

Asante sana mkuu, kuna jamaa nimeongea naye... anayo mashine yake na anaweza kufanya kazi.

Pia Job Richard anazo mashine anaziuza na kufundisha jinsi ya kutumia.
 
Back
Top Bottom