Nadhani utakuwa unawajua wadudu wanaoitwa mchwa....ni wadudu wanaoishi katika mfumo wa kifalme.
Si mchwa tu wenye kuishi katika mtindo huu, wapo wadudu wengi wanyama na hata wanadamu pia.
Sasa kumbikumbi ni jamii ya mchwa ambao wapo katika hatua ya ukuaji kuelekea either Malkia au Mfalme.
Kwa kawaida katika life cycle ya wadudu huwa wana hatua kuu nne ( eggs, larva, nymph 'buubuu', mdudu kamili).
Sasa kwa termites "jamii ya mchwa", wanapofikia stage ya nymph, hii ni stage muhimu kwao kwani hapa ndipo mgawanyiko wa majukumu hutokea kwa mchwa ku-develop katika aina tatu tofauti.
1. Aina ya kwanza ni "Workers" au wafanyakazi...hawa ndio wale mchwa wasumbufu ambao kutwa huwa wanakula hata vitu vyetu majumbani.
2. Aina ya pili ni "Solders" au wapiganaji...hawa kazi yao ni kumlinda malkia ndani ya kichuguu na wakati wa vita hupigana na wadudu wengine kama siafu n.k (siafu ni adui mkubwa sana wa mchwa).
3. Aina ya tatu ni "Alate" au kumbikumbi....hawa kazi yao ni kuendeleza kizazi kwanu huendelea kukua na baadaye huwa Malkia na Mfalme.
Tofauti na aina mbili za mwanzo wao huwa na mabawa yanayowafanya watoke nje ya kichuguu na kusafiri kwenda mahali pengine kuanzisha kichuguu kingine (huenda kuanzisha ufalme mwingine).
Picha hii chini yaonesha mzunguko wa maisha ya mchwa "termites"
CC:
mimi49