dragon chapter
Member
- May 4, 2017
- 78
- 46
By Inciter-In-Chief.
BAADHI YA WATU MAARUFU WALIOWAHI KUFUNGULIWA MASHTAKA YA UCHOCHEZI.
(1) Namo tarehe 3 April Mwaka 33, Yesu Kristo alifunguliwa mashtaka matatu ya jinai na kati ya hayo moja ya shitka lilikuwa ni shitka la "uchochezi" kwenye ili tunaweza kufanya rejea katika Kitabu cha LUKA, Sura ya 23, Msitari wa 2. Kuhusu shitka hili la uchochezi ilidaiwa kwamba Yesu aliwapotosha watu kwa kuwazuia wasilipe kodi kwa Kaizari na kujitangaza kuwa yeye ni mfalme. Yesu alikutwa na hatia ingawa kimagumashi yaani kwa kulazimisha kwa sababu, Pilato, J (as he then was) alisema kuwa haoni hatia kwa Yesu.
(2) Namo tarehe 5 August, 1962 Nelson Rolhalha Mandela alifunguliwa mashtaka mawili na moja likiwa ni la uchochezi. Tarehe 25 Oktoba, 1962, mahakama ilimkuta Mandela na hatia ya kosa la uchochezi na na kumpa adhabu ya kifungo cha miaka mitano (5) jela.
(3) Mzee (as fondly referred by Kenyans) Jomo Kenyatta mwaka 1952 alifunguliwa mashtaka na alikutwa na hatia ya kutenda kosa la uchochezi kwa kuchochea vita ya Mau Mau pamoja na kwamba Mzee Kenyatta alikata rufaa mpaka Mahakama ya Juu ya Kenya ya wakati huo lakini rufaa yake ilitupiliwa mbali na Jaji Rudd (as he then was) tarehe 15 Januari, 1954.
(4) Julius Kambarage Nyerere namo mwezi Juni, 1958 alifunguliwa mashtaka kadhaa moja wapo lilikuwa ni la uchochezi. Tarehe 11 August, 1958 alikutwa na hatia ya kutenda kosa la uchochezi na tarehe 13 August, 1958 akahukumiwa kwenda jela miezi 6 au kulipa faini ya Tshs. 3, 000 ndani ya siku tatu (3), alilipa faini na kuepuka jela.
(5) Tundu Lissu, huyu amepata kukabiliwa na kesi kadha za uchochezi ikiwemo Kesi ya Jinai No. 208 ya 2016 na Kesi ya Jinai No. 47 ya 2017, hatahivyo, hajawahi kutiwa hatiani kwa kosa la uchochezi.
Watu watano maarufu ambao nimewaangazi leo, wanne walitiwa hatiani na mahakama kwa kutenda kosa la uchochezi na mmoja tu ambaye ni Tundu Lissu ndo pekee hajawahi kutiwa hatiani, hatahivyo, bado kesi zinazomkabili hazijafanyiwa uamuzi na mahakama, hivyo, lolote laweza kutokea.
Uzoefu unaonesha kuwa karibu viongozi wengi ambao walipata kufunguliwa mashtaka ya uchochezi siku za mbeleni walitokea kuwa watu maarufu sana na wanaoheshimika ambao wakati mwingine ni vigumu kufuta majina yao katika historia ya Ulimwengu huu na wengine walibahatika kupata wadhifa wa Rais wa nchi zao kama vile Mandela na Kenyatta na kupata wafuasi wengi sana, kwa mfano Yesu Kristo anakadilwa kuwa na wafuasi Billion 2.2 takribani asilimia 31% ya watu wote duniani.
Mwandishi wa makala hii ni mchambuzi wa maswala ya uchochezi.
Sent using Jamii Forums mobile app