Mchakato wa kuwalipa wenye vyeti feki wakwama

Kwani sheria ya kazi inasemaje kuhusu kuondolewa kazini kwa misconduct?Kama serikali inaamua mtu akifanya makosa ya kinidhamu ana haki ya kulipwa stahiki zake basi iwahusu wote hata wale waliopigana makazini,kuiba nk....
 
Taarifa za Serikali ya Tanzania zilieleza kwamba, Rais Samia aliagiza wenye vyeti feki walioondolewa kazini na serikali ya awamu ya 5, walipwe stahiki zao kuanzia Novemba mosi.

Vyombo vya habari vilivyonunuliwa na vile vile vilivyojipendekeza vikaripoti habari hiyo kwa mashamsham.

View attachment 2433982

Bali uchunguzi wetu umebaini kwamba hadi kufikia leo, zaidi ya mwezi tangu tamko la Rais, hakuna mhanga yoyote aliyelipwa chochote, na kuna taarifa kwamba hawatolipwa milele.

Ikumbukwe kwamba wahanga hawa idadi yao ni kama elfu 10 na ushee tu, kisingizio chochote cha sijui kuna mchakato yakinifu ni sawa na uongo wa mchana.

Watanzania siyo wajinga kihivyo, kama Magufuli aliwadhalilisha na waliridhika kwanini nyie muwadanganye?

Mmawia amelipwa????
 
Sheria za Nchi zinasemaje juu ya mtu alipata ajira kwa njia za udanganyifu?
Hoja yako imepitwa na wakati , kwenye uzi huu tunazungumzia amri iliyotolewa na Rais ya kuwalipa wenye vyeti feki
 
Taarifa za Serikali ya Tanzania zilieleza kwamba, Rais Samia aliagiza wenye vyeti feki walioondolewa kazini na serikali ya awamu ya 5, walipwe stahiki zao kuanzia Novemba mosi.

Vyombo vya habari vilivyonunuliwa na vile vile vilivyojipendekeza vikaripoti habari hiyo kwa mashamsham.

View attachment 2433982

Bali uchunguzi wetu umebaini kwamba hadi kufikia leo, zaidi ya mwezi tangu tamko la Rais, hakuna mhanga yoyote aliyelipwa chochote, na kuna taarifa kwamba hawatolipwa milele.

Ikumbukwe kwamba wahanga hawa idadi yao ni kama elfu 10 na ushee tu, kisingizio chochote cha sijui kuna mchakato yakinifu ni sawa na uongo wa mchana.

Watanzania siyo wajinga kihivyo, kama Magufuli aliwadhalilisha na waliridhika kwanini nyie muwadanganye?
Kwa kwawaida kama unadai mafao ukikamilisha kujaza fomu unasubiri takriban mwez 1 hadi miwili ndio ulipwe...wao wamejaza fomu kuanzia Nov 1 sasa hawa watalipwa kuanzia january ...kwenye kudai mafao haujaz fomu leo ukalipwa kesho lazma usubiri wahakiki kwanza ndio ulipwe
 
Mbona kwenye kuwatimua hakukuwa na mlolongo ?
Mlolongo ulikuepo..walifanya uhakikia wa vyeti kwa mud mrefu tu,wakawabaini ,tar 1/5/2017 kupitia hotuba ya mheshimiwa rais wakaamriwa kuacha kaz mara moja kwa ridhaa yao wenyew...au unazungumzia mlolongo upi
 
Watanzania siyo wajinga kihivyo, kama Magufuli aliwadhalilisha na waliridhika kwanini nyie muwadanganye?
Kama sio wajinga msingekubali kuaminishwa kwamba kufoji elimu haina tatizo.

Ungejisikiaje kutibiwa na daktari aliyefoji vyeti ?

Mtu aliyepindisha sheria na taratibu za ajira akaja akakamatwa na kuchukuliwa hatua huwezi kusema amedhalilishwa. Mtu aliyekutwa na hatia ya kumwibia mwajiri, akafukuzwa, akawekwa gazetini huwezi kusema amedhalilishwa.

Magufulii aliwawajibisha watu waliodhulumu haki za wenzao ambao kaya zao, nyingi masikini, zilijiitoa na kujinyima ili watoto wasome na wapate ajira za haki. Kwa nini umlipe mhalifu? Pombe Magufuli alikuwa kiongozi wa kipekee.
 
Mlolongo ulikuepo..walifanya uhakikia wa vyeti kwa mud mrefu tu,wakawabaini ,tar 1/5/2017 kupitia hotuba ya mheshimiwa rais wakaamriwa kuacha kaz mara moja kwa ridhaa yao wenyew...au unazungumzia mlolongo upi
Uongo utakusaidia nini ?
 
Back
Top Bottom