Mchakato wa kubadilisha Director kwenye kampuni

Nov 3, 2019
47
32
Habari,

Kutokana na umbali nilipo nimeshindwa kufika Brela kuulizia hili jambo. Imani yangu hapa JF kuna watu wanajua jambo hili.

Je ni hatua zipi niweze kuzifuata ili kujitoa kuwa Director kwenye kampuni na kumuingiza mke wangu ndio awe mmoja wa Director?

Ndio kwanza kampuni imeanza shughuli zake, ila nimeona mimi nijitoe niendelee na mambo mengine.

Asanteni
 
Kama hiyo kampuni ilikuwa limited (by share) company na huyo Director unayetaka kumuondoa alikuwa na share itabidi uanzie TRA kuhusu hizo share zake lazima zilipiwe kodi kama unazitransfer kwa director mpya.

Baada ya hapo nenda kwenye Brela website tafuta form inayoitwa "Appointment and Termination of Director". Mkurugenzi anayebaki ndo azijaze hizo form kwa yule anayemuappoint na kwa yule anayemterminate na kuziupload kwenye mtandao wa Brela.

Kwa ufupi ndo hivyo ila kuna kamchakato fulani. Kama utahitaji msaada zaidi Njoo PM kwasababu mimi mwenyewe nimewahi kubadilisha wakurugenzi
 
Haina haja ya wewe kujitoa! Swala la Msingi ni kuongeza mkurugenzi ili akusaidie kukamilisha majukumu ambayo yanamhusu Mkurugenzi! Siku ukiamua kurudi unaendelea na majukumu yako kama mkurugenzi bila kuathiri upande wowote!

Ukisema ujiondoe; lazima ujaze form ya kutransfer share/contract ya mauziano ya share; igongwe mhuri na Wakili (kama company ni limited by share), baada ya hapo utaenda TRA kupewa Tax clearance certificate baada ya kulipia kodi ya 10% ya gharama zote za share ambazo umetransfer!

Baada ya hapo utaingia online kwenye account yako brela na kujaza hayo mabadiliko yaani unaongeza mkurugenzi, halafu utatakiwa download consolidation form of company ambayo inakuwa signed na directors wote. Kisha utai_upload pamoja na copy ya Tax clearance certificate kutoka TRA na Share transfer form/contract ya mauziano ya share.

Kifupi ndio hivyo
 
Mtu anayeelezea hatua za kufata hapa ni rahisi kufatwa inbox kuliko anaye sema "njoo ibox" au anayetoa namba ya simu...
 
Mtu anayeelezea hatua za kufata hapa ni rahisi kufatwa inbox kuliko anaye sema "njoo ibox" au anayetoa namba ya simu...
Yan kila threads ukianzisha watu hawaangalii wakusadieje kulingana na shida uliyosema ila wanangalia ni vipi watakupiga chochote kusogeza siku
 
Back
Top Bottom