Hivi karibuni zimetoka ajira mpya Serikalini kwa kada za Afya na Elimu. Kitu kilichonishangaza kuna vijana wengi walioomba wenye Shahada wameachwa, badala yake wamechukuliwa wenye vyeti (Astashahada)!
Tatizo ni kwamba, hawa wote wenye vyeti wanapopata ajira kinachofuatia wanaomba ruhusa ya kwenda kusoma ili kupata Stashahada, Shahada n.k, muda huo upungufu wa walimu huwa unaendelea.
Sasa kwanini tunawaacha hawa wenye Shahada ya ualimu ambao walau wanakuwa wamepiga hatua kubwa ya masomo? Hivi hawa wafanya maamuzi huwa wanawaza nini?