Mchakato uagizaji treni za umeme waanza

mkiluvya

JF-Expert Member
May 23, 2019
802
725
1567413489264.png

MSEMAJI Mkuu wa Serikali, Dk. Hassan Abbas, amesema Serikali imeagiza treni tano za kisasa ambazo kila moja itakuwa na mabehewa nane ambayo yatasafirisha abiria kutoka Dar es Salaam hadi Dodoma.

Pia alisema Serikali haitarudi nyuma wala kusalimu amri, licha ya uwepo wa hujuma zinazofanyika kutaka kurudisha nyuma kasi ya maendeleo.

Akizungumza na waandishi wa habari jijini hapa jana kuhusu utekelezaji wa miradi mikubwa ya kimaendeleo nchini, Dk. Abbas alisema Serikali imeanza zabuni ya kuagiza vichwa 22, vitano vya mafuta yaani dizeli na 17 vya umeme na mabehewa ya abiria 60 na ya mizigo.

“Serikali imeanza zabuni ya treni tano zilizokamilika za abiria zenye mabehewa nane kila moja na vichwa viwili kwa ajili ya uendeshaji wa treni za abiria kwa kipande cha Dar– Moro na kisha Dodoma,” alieleza Dk. Abbasi.
 
View attachment 1195673

Nimeshtuka kusikia kuna hujuma. La kushangaza yanafanyika maamuzi ya kuwapa moyo wapinga maendeleo. Mkisema kuna kesi za kubambikiza eti zifutwe mnavivunja mioyo vyombo vyetu vya usalama kuonekana vimebandikia watu kesi. Kesi zenyewe za mafisadi wakubwa ndio wapinzani watasema ndio zimebambikwa kwa hiyo zifutwe. Vita vya kiuchumi huendeshwa kimapinduzi hasa kama ni kwa maslahi ya umma sio tabaka la kinyonyaji.
 
Kwani anayesema Kuna kesi za kumbambikia watu ni Raisi mwenyewe
Kwa hiyo wewe ndiyo unajua zaidi ya Raisi
 
Back
Top Bottom