Mchakato Mahakama ya Mafisadi waanza

Mchakato Mahakama ya Mafisadi waanza

Cardinal06

JF-Expert Member
Joined
Jan 7, 2015
Posts
963
Reaction score
327
Dar es Salaam. Utekelezaji wa ahadi za Rais John Magufuli unazidi kushika kasi baada ya kuanza kwa mchakato wa kuanzisha mahakama maalumu ya kuwashughulikia mafisadi.

Jaji Kiongozi, Shaban Lila alisema jana kuwa tayari wadau mbalimbali wa haki jinai wameanza kukutana kuangalia namna ya kuanzisha mahakama hiyo kama sehemu ya utekejezaji wa ahadi ya Rais.

Akizungumza katika hafla ya kuhitimisha mafunzo ya kushughulikia mashauri nyeti ya jinai kwa majaji 12 wa Mahakama Kuu ya Tanzania, alisema juzi walikuwa na mazungumzo na Wizara ya Katiba na Sheria kuangalia mfumo wa uendeshaji wa mahakama hiyo.

"Tunaangalia tuianzishe kama mahakama huru au ifanywe ndani ya muundo wetu wa mahakama kwa kuipa kipaumbele maalumu. Lakini tunafikiria zaidi kama ingekuwa ni kitengo maalumu ndani ya Mahakama Kuu kitakachokuwa kikishughulikia mafisadi," alisema Jaji Lila.

Hata hivyo, Jaji Lila hakutaja muda maalumu utakaotumika kumaliza mchakato wa kuanzisha mahakama hiyo, huku akisema unahusisha wadau wengi na unyeti wake unahitaji maandalizi makubwa.

Jaji huyo bila kutaja takwimu, alieleza kuwa kesi za makosa makubwa ya jinai zinaongezeka nchini ukilinganisha na miaka ya nyuma hasa zile zinazohusu utakatishaji fedha, ugaidi, usafirishaji wa dawa za kulevya, usafirishaji wa nyara za Serikali hasa wanyama hai na mazao yake na ufisadi.

Balozi wa Uingereza nchini, Dianna Melrose alimpongeza Rais Magufuli kwa kuonyesha msimamo wa kupambana na makosa ya jinai yakiwamo ya dawa ya kulevya, usafirishaji wa nyara za Serikali na utakatishaji fedha.

"Nilikuwa nimeketi bungeni namsikiliza Rais siku alipokuwa akilihutubia Bunge, japo hotuba yake ilikuwa kwa Kiswahili lakini nilipata faraja kubwa nilipomuona akiwa mkali katika masuala hayo," alisema Balozi Melrose.

Chanzo: Mwananchi
 
vzr xana jpm but mahakama hyo lazma iwe huru na isiweze kuingiliwa na m2 yeyote na hata rais aweze kushtakiwa ikiwa itadhbitka kala rushwa na kiukwel iwe huru kwel kwel
 
kp25112015.jpg

Wafanye haraka kabla mtuhumiwa wa kwanza wa hiyo mahakama hajafa kwa parkinsonism
 
Mchakato wa Kuanzisha Mahakama ya MAFISADI Waanza
Utekelezaji wa ahadi za Rais John Magufuli unazidi kushika kasi baada ya kuanza kwa mchakato wa kuanzisha mahakama maalumu ya kuwashughulikia mafisadi.

Jaji Kiongozi, Shaban Lila alisema jana kuwa tayari wadau mbalimbali wa haki jinai wameanza kukutana kuangalia namna ya kuanzisha mahakama hiyo kama sehemu ya utekejezaji wa ahadi ya Rais.

Akizungumza katika hafla ya kuhitimisha mafunzo ya kushughulikia mashauri nyeti ya jinai kwa majaji 12 wa Mahakama Kuu ya Tanzania, alisema juzi walikuwa na mazungumzo na Wizara ya Katiba na Sheria kuangalia mfumo wa uendeshaji wa mahakama hiyo.

?Tunaangalia tuianzishe kama mahakama huru au ifanywe ndani ya muundo wetu wa mahakama kwa kuipa kipaumbele maalumu. Lakini tunafikiria zaidi kama ingekuwa ni kitengo maalumu ndani ya Mahakama Kuu kitakachokuwa kikishughulikia mafisadi,? alisema Jaji Lila.

Hata hivyo, Jaji Lila hakutaja muda maalumu utakaotumika kumaliza mchakato wa kuanzisha mahakama hiyo, huku akisema unahusisha wadau wengi na unyeti wake unahitaji maandalizi makubwa.

Jaji huyo bila kutaja takwimu, alieleza kuwa kesi za makosa makubwa ya jinai zinaongezeka nchini ukilinganisha na miaka ya nyuma hasa zile zinazohusu utakatishaji fedha, ugaidi, usafirishaji wa dawa za kulevya, usafirishaji wa nyara za Serikali hasa wanyama hai na mazao yake na ufisadi.
 
Safi ila Mkuu wa kaya alisema neno MCHAKATO halitakuepo....ngoja tusubiri huo mchakato
 
Hahahaaa hii kitu inanichekesha xana mana ni nzuri ila kuwakamata hao majiz na kuwafunga xaxa ndo itakua mtihani mana ndo hao hao waliomuweka pombe madarakani
 
Hiyo mahakama itahusu yule waziri ayeliuza nyumba za serikali kwa hawara zake ?
Wale wa Escorw itawahusu pia?
 
Hii ahadi ya Mh. Rais inatakiwa itekelezwe kwa weledi tu na siyo kitu cha ajabu.
Ufisadi ni jinai kama jinai nyingine zinazoshughulikiwa katika mahakama za kawaida. Tatizo la kutoshughulikia ufisadi linatokana na kukosa utashi wa kisiasa kwa sababu wanasiasa ni mafisadi au mafisadi ni washirika wao.
Kama Rais anataka kuwashughulikia mafisadi, aweke taratibu za kuwaondoa mafisadi kwenye siasa, asafishe Takukuru na DPP, halafu mahakama ifuate. Lini mahakama zilizopo zilishindwa kuwashughulikia mafisadi?
 
Back
Top Bottom