Mch.Msingwa, Mnyika wamchefua Olesendeka

kilagalila

JF-Expert Member
Nov 8, 2018
320
154
1545501647233.jpeg
Mkuu wa mkoa wa Njombe Christopher olesendeka ametangaza vita dhidi ya mwanasiasa yeyote atakayeingia katika mkoa wa Njombe na kumjaribu kumtikisa kwa kuhubiri ndoa ya jinsia moja (ushoga) kama ambavyo baadhi ya wanasiasa na wanaharakati wanavyozungumza wakiwa katika maeneo mengine.

Olesendeka ameyasema hayo wakati akizungumza na wadau wa kodi katika kikao kilichofanyika katika ukumbi wa halmashauri ya mji wa Njombe huku akionyesha kukasilishwa na watanzania hususani wanasiasa ambao wamekuwa wakishabikia vitendo ambavyo vimekuwa vikipingwa hata katika vitabu vya Injili.

“Vipo vyama vya siasa na nimemsikia jana Msigwa alafu anajiita mchungaji,wanaongea mambo ya hovyo mchungaji yaani sisi utwambie hivyo, kama hilo ni jambo jema basi yeye angeanza kufunga ndoa na mmoja wa wanaume alio nao pale bungeni, yaani wewe mtanzani unaacha kusimamia misingi ya utu, misingi ya kusimamia taifa letu, na wewe kwasababu ya vijisenti unavyopewa huko nje unakuja na wewe kutaka kupanda mbegu eti na hiyo ni moja kati ya haki ya bina adamu ni haki gani hiyo” alizungumza olesendeka.

Aidha mkuu huyo wa mkoa ameongeza kusema kuwa uzalendo si swala la mtu mmoja, dini, wala halina chama bali ni ajenda ya kila mtanzania kwa kulipenda kulitii na kulilinda taifa mpaka damu yake ya mwisho.

“Ndugu zangu uzalendo kwa nchi si la mtu mmoja na katika jambo ambalo halihitaji kuangalia dini,wala chama cha mtu, wala eneo analotoka mtu ni swala la uzalendo kwa nchi yako tena wala haliangalii Mbowe, haliangalii Bashiru wala mlowe hili ni ajenda ya kila mtanzania kuilinda nchi yake mpaka damu yake ya mwisho,bahati mbaya nchi yetu imeingiliwa nataka niwaambieni kama nchi hatutaludi nyuma, siku moja atoke mtu afanye mkutano kwenye mkoa wa Njombe walau kwenye kipande hiki alichonipa Rais ahubiri mambo hayo ya hovyo wanayoyahubiri huko nitamshukia kama mwewe”aliongeza olesendeka.

Katika hatua nyingine Olesendeka ameonyesha kushangazwa na viongozi waliokula kiapo lakini bado wamekuwa wakiendelea kuvunja sheria.

“lengo la jamhuri ya serikali ya muungano wa Tanzania ni ustawi wa watu wake, wabunge na sisi wakuu wa mikoa tumekula kiapo cha uaminifu na kiapo cha kuilinda katiba ya nchi kwa hiyo leo unaposikia mtu amekula kiapo iwe bungeni uwe waziri halafu wewe mwenyewe unakwenda kinyume na kiapo ulichokula kuilinda katiba na kuilinda misingi ya sheria mama ya nchi, ndio maana juzi watu wote walimshangaa mbunge wa Kibamba rafiki yangu Mnyika sheria inasema kati ya mita hizi na hizi ni hifadhi ya barabara na nisheria ambayo ni katiba unamuomba Rais avunje sheria eti katika moyo wa huruma uvunje sheria ukiuke katiba uliokula kiapo cha kuilinda alaaaa!”olesendeka alionyesha kushangaa.

mc.amiri/mr.mtaani
 
Attachments

  • IMG-20181222-WA0119.jpg
    IMG-20181222-WA0119.jpg
    58.8 KB · Views: 27
  • IMG-20181222-WA0122.jpg
    IMG-20181222-WA0122.jpg
    77.5 KB · Views: 26
  • IMG-20181222-WA0124.jpg
    IMG-20181222-WA0124.jpg
    65.6 KB · Views: 27
  • IMG-20181222-WA0129.jpg
    IMG-20181222-WA0129.jpg
    66.4 KB · Views: 25
  • IMG-20181222-WA0130.jpg
    IMG-20181222-WA0130.jpg
    62.7 KB · Views: 26
Kama mchungaji Msingwa anahubiri ndoa za jinsia moja, sijui. Lakini nadhani CCM inayo nia ya dhati ya kutaka "kujisahaulisha" kuwa ilitia saini mikataba ya kulinda na kutetea haki za binadamu (in broader sense of human rights).
 
View attachment 974806Mkuu wa mkoa wa Njombe Christopher olesendeka ametangaza vita dhidi ya mwanasiasa yeyote atakayeingia katika mkoa wa Njombe na kumjaribu kumtikisa kwa kuhubiri ndoa ya jinsia moja (ushoga) kama ambavyo baadhi ya wanasiasa na wanaharakati wanavyozungumza wakiwa katika maeneo mengine.

Olesendeka ameyasema hayo wakati akizungumza na wadau wa kodi katika kikao kilichofanyika katika ukumbi wa halmashauri ya mji wa Njombe huku akionyesha kukasilishwa na watanzania hususani wanasiasa ambao wamekuwa wakishabikia vitendo ambavyo vimekuwa vikipingwa hata katika vitabu vya Injili.

“Vipo vyama vya siasa na nimemsikia jana Msigwa alafu anajiita mchungaji,wanaongea mambo ya hovyo mchungaji yaani sisi utwambie hivyo, kama hilo ni jambo jema basi yeye angeanza kufunga ndoa na mmoja wa wanaume alio nao pale bungeni, yaani wewe mtanzani unaacha kusimamia misingi ya utu, misingi ya kusimamia taifa letu, na wewe kwasababu ya vijisenti unavyopewa huko nje unakuja na wewe kutaka kupanda mbegu eti na hiyo ni moja kati ya haki ya bina adamu ni haki gani hiyo” alizungumza olesendeka.

Aidha mkuu huyo wa mkoa ameongeza kusema kuwa uzalendo si swala la mtu mmoja, dini, wala halina chama bali ni ajenda ya kila mtanzania kwa kulipenda kulitii na kulilinda taifa mpaka damu yake ya mwisho.

“Ndugu zangu uzalendo kwa nchi si la mtu mmoja na katika jambo ambalo halihitaji kuangalia dini,wala chama cha mtu, wala eneo analotoka mtu ni swala la uzalendo kwa nchi yako tena wala haliangalii Mbowe, haliangalii Bashiru wala mlowe hili ni ajenda ya kila mtanzania kuilinda nchi yake mpaka damu yake ya mwisho,bahati mbaya nchi yetu imeingiliwa nataka niwaambieni kama nchi hatutaludi nyuma, siku moja atoke mtu afanye mkutano kwenye mkoa wa Njombe walau kwenye kipande hiki alichonipa Rais ahubiri mambo hayo ya hovyo wanayoyahubiri huko nitamshukia kama mwewe”aliongeza olesendeka.

Katika hatua nyingine Olesendeka ameonyesha kushangazwa na viongozi waliokula kiapo lakini bado wamekuwa wakiendelea kuvunja sheria.

“lengo la jamhuri ya serikali ya muungano wa Tanzania ni ustawi wa watu wake, wabunge na sisi wakuu wa mikoa tumekula kiapo cha uaminifu na kiapo cha kuilinda katiba ya nchi kwa hiyo leo unaposikia mtu amekula kiapo iwe bungeni uwe waziri halafu wewe mwenyewe unakwenda kinyume na kiapo ulichokula kuilinda katiba na kuilinda misingi ya sheria mama ya nchi, ndio maana juzi watu wote walimshangaa mbunge wa Kibamba rafiki yangu Mnyika sheria inasema kati ya mita hizi na hizi ni hifadhi ya barabara na nisheria ambayo ni katiba unamuomba Rais avunje sheria eti katika moyo wa huruma uvunje sheria ukiuke katiba uliokula kiapo cha kuilinda alaaaa!”olesendeka alionyesha kushangaa.

mc.amiri/mr.mtaani
Sendeka angeanza na Makonda na kumhoji swala la kupambana na ushoga liliishia wapi?? Au ndo mshirika mkubwa wa laana Hiyo??
 
Back
Top Bottom